sábado, 20 de outubro de 2018

UKUU WA KWELI NI KUTUMIKIA KWA UNYENYEKEVU NA UKARIMU



Kutafakari kutoka Is 53, 10-11; Waeb 4, 14-16; Mk 10, 35-45

     Maisha ya yule ambaye anamtumikia Bwana yana maana kubwa. Yote ambayo anafanya yalenga kufunua mapenzi ya Yule ambaye alimwalika kuwa mtumishi wake. Kwa sababu ya kujisalimisha kwake kwa upendo watu wengi wataokolewa (andiko la kwanza). Huyo ndiye Kuhani mkuu ambaye tunahitaji, yaani mtu kama sisi, ambaye anachukua hali yetu ya udhaifu - ila dhambi – ili kutuonyesha njia kamili ya kushinda hali hii na majaribu yote yanayotuzuia kuonja neema ya Mungu na kuishi kulingana na mapenzi yake (andiko la pili).

         Katika injili, ndugu wawili, yaani Yakobo na Yohane walimwendea Yesu na kumwomba kitu. Walitaka kuketi mmoja mkono wake wa kuume na mwingine mkono wake wa kushoto katika utukufu wake. Ombi hili linadhihirisha kwamba wanafunzi wake walishindwa kufahamu utambulisho na utume wa Mwalimu wao. Ni muhimu kukumbuka kwamba hali hii ilitokea baada ya ufunuo wa Yesu kuhusu mambo yatakayomtokea yeye katika Yerusalemu, yaani mateso, kifo na kisha kufufuka. Katika kipindi kingine, wakati Yesu alipoongea kuhusu matukio muhimu hayo, wanafunzi walijadiliana kuhusu ni nani ndiye mkuu kati yao, wakionyesha kwamba mawazo na matarajio yao yalikuwapo bado mbali sana na pendekezo la Mwalimu Yesu. Hivyo, yeye alipaswa kuwa na uvumilivu sana mbele ya ugumu wa wale aliowachagua kama washirika. Hata hivyo, aliweka halisi daima masharti ya kumfuata. 

         Kwa wanafunzi wa Yesu, sehemu muhimu ya tangazo lake ndio utukufu kwa sababu walitafuta kuwa wahusika wakuu. Wengine kumi walikasirika kwa sababu walitafuta mambo sawa na wote wawili nao hawakukubali kubaki nyuma. Kwa maneno mengine, wote walikuwa wazi katika kutafuta kwao, yaani walitafuta msimamo, umaarufu na upendeleo, lakini walichagua Mtu sio kamili wa kumfuata ili kutimiza lengo hili kwa sababu mantiki ya Yesu ni tofauti. Mbele ya hali hii ya mgawanyiko kwa sababu ya ghasia ya rejeo la maisha, Yesu aliwaalika tena kama mara ya kwanza na kusahihisha matarajio yao potovu: “anaondosha fikra zao walizojijengea wenyewe.” Njia ya maisha yake ina mwelekeo tofauti na wa dunia. “Katika ufalme wa Yesu, wale walio viongozi hawapo ili kuwanyonya wengine au kutegemea heshima na utumishi kutoka kwa watu wao, bali viongozi ndiyo huwa watumishi wa watu.”

       Basi, mantiki ya Yesu ndiyo mantiki ya utumishi unaokuta katika maisha yake rejeo lake: “Mwana wa Mtu hakuja kutumikiwa, bali kutumikia na kutoa maisha yake kuwa fidia ya watu wengi.” Hali hii ambayo ilishirikisha maisha yake wakati wote inakuwa ni rejeo kwa maisha ya wale ambao wanatamani kumfuata kwa uaminifu: “Yeyote anayetaka kuwa mkuu kati yenu sharti awe mtumishi wa wote; na anayetaka kuwa wa kwanza kati yenu sharti awe mtumishi wenu.” Hakuna njia nyingine ili mtu aweze kupata maana kamili ya maisha. Yeyote anayeamua kumfuata Yesu hawezi kuendelea kufikiri na kutenda kama mtu wa zamani.

        “Yesu anakumbana na upinzani mkali huko Yerusalemu na kumfanya apoteze maisha yake. Lakini jambo hilo Yesu anaona ni huduma ya upendo kwa watu wake (Mk 10:45).” Ndiyo kupitia imani katika Kristo na msukumo kutoka Neno lake kwamba yeyote anaweza kukabiliana na taabu, kukataa na mateso bila kukata tamaa. Hivyo, kuishi au kulima wito wa mtumishi kwa uaminifu sio rahisi kwa sababu kuna vitu vingi dhidi ya uamuzi wetu, yaani mawazo kandokando yetu kwa kawaida ni tofauti na pendekezo la injili; upinzani kutoka kwa wengine hata familia; mwelekeo wa kibinadamu ambao ndani yetu unatuimarisha kutafuta kutumikiwa badala ya kutumikia; kutokuwa na imani yenye nguvu na kosa la uvumilivu katika matendo mazuri, n.k.

        Vitu hivi vyote ni sehemu ya safari yetu pamoja na hamu yetu ya kumfuata Yesu kwa uaminifu. Lakini hatusahau kwamba hatutembei peke yetu. Yule aliyekubali “kujitoa kama zawadi kwa watu wote” ndiye mfano wetu na kutuhakikishia msaada wake ili tudumu katika utumishi kwa ajili ya wengine hata mbele ya kutokuelewana na taabu. Ikiwa ndio upendo ambao unatoa maana ya maisha, hakuna njia nyingine ya kuishi kwa maana ila kupitia utumishi kwa unyenyekevu na kwa ukarimu kwa wengine ulio maonyesho halisi ya upendo na utambulisho na Yule ambaye “alikufa na kufufuka kwa ajili yetu, inatoa mwenyewe kwa uhuru wetu na kuuimarisha kutafuta, kugundua na kutangaza maana hii ya kweli na kamili.”

Fr Ndega


Nenhum comentário: