quarta-feira, 17 de setembro de 2014

MUNGU HAWACHANI NA WALE AMBAO WANATESEKA



Tafakari kutoka Yohana 19, 25-27

Andiko hili linatualika kutafakari kuhusu mshikamano wa Mama Maria kabla ya mateso ya mwana wake ambaye ni Mwana wa Mungu.
Kati ya tabia kadhaa ya Bikira Maria, andiko hili la Injili ya Yohana linaleta kwetu ushahidi wake wa kimya kama wa Kwanza na mwanafunzi Mwaminifu wa Mwanawe. Yeye alichukua jukumo lake hadi mwisho matokeo. Wakati wanafunzi wengine wakaenda zao, Maria anabaki amesimama kando ya msalaba. Pamoja naye, wanawake wengine watatu na mwanafunzi aliyependwa na Yesu wanabaki pia. Upendo tu unaweza kueleza nguvu na uvumilivu wa wanawake katika wakati huu haswa wa maisha ya Mwalimu. Kweli, walijifunza somo la uanafunzi wa ukarimu katika bure jumla. Wakajikana, wakabeba msalaba wao na wakawa wenye huruma katika kufuata nyayo za Mwalimu.
Tunatafakari katika onyesho hili la ishara kuu ya upendo wa Mwana wa Mungu, ambaye anasalimisha nafsi yake kwa maisha ya binadamu mwenye dhambi. Mateso yake ni mwanzo wa ushindi wake juu ya kifo, na kufanya kufufua matumaini yote ya watu. Kwa upande wake, hakuna upendo mkubwa kuliko kutoa maisha kwa ajili ya wema wa marafiki. Kabla ya mateso ya Mwana, tunatafakari huruma ya Mother, ambaye anajua jinsi ya kupenda na jinsi ya kuteseka kwa mtu unayempenda. Mary anachukua katika moyo wake huzuni zote za mwanawe. Kama hii ilitimizwa katika unabii wa Simeoni katika Hekalu wakati yeye alichukua mtoto mdogo Yesu mikononi mwake: "Upanga utachoma roho yako mwenyewe".
Wote Mwana na Mama wanatusaidia kutafakari hali halisi ngumu ya mateso ya binadamu na kuamini kwamba Mungu hawachani na wale ambao wanateseka. Wote wanatufundisha jinsi ya kukaribisha mateso kwa utulivu na uwepo imara katika maisha ya watu ambao wanateseka. Hebu mfano huu wa Maria, Mama wa huzuni, utuhamasishe sisi kuishi kwa uaminifu utambulisho wetu wa wanafunzi wa Mwana wake Yesu na kuchukua kwa ujasiri na msalaba wetu kila siku, kuwa na uwezo wa kujisalimisha maisha yetu kama Yesu kwa wema wa wengine.

Fr. Ndega
Mapitio: Rose Mong’are na Mwalimu Patrick

sábado, 13 de setembro de 2014

ABOUT THE JESUS LIFE’S PLAN




A reflection from Luke 4,16-30


Jesus shares with his hometown friends his life’s plan. He chose a liturgical moment to reveal solemnly the priority of his mission. He declare to be guided by the Holy Spirit to proclaim good news to the poor and liberation to those who are oppressed, reviving his hope and returning to them the joy of living.
Jesus lives the joy and the enthusiasm of being chosen to reveal the plan of love and salvation of his Father. God loves everybody and want to reach to everyone with his love. However, he has some preferred people who need special care, because are rejected by society.
Jesus as salvation of God, is fulfilment of the Scripture, but in his sharing is rejected for those who say they know the Scriptures. Maybe they were habituated to accept only what is convenient to them, adapting the Word of God to his way of living, without good disposition to live the appeals and requirements which come from this Word.
Like the people from Nazareth, we also have resisted to the Word of Jesus which questions about the quality of our daily welcome and it requires major commitment with the reality of others, especially the poor people. We cannot think that the information we have received about Jesus is enough for our journey. It is necessary to allow that he reveals himself to us with all power of his love.  Let us welcome this revelation of Jesus today as invitation we think better about our priorities and sense of solidarity with others.

Fr. Ndega

KUHUSU MPANGO WA MAISHA YA YESU



Kutafakari toka Luka - aya 4, sura 16-30

Yesu anashiriki na marafiki mji zake mpango wake wa maisha. Alichagua kufanya hivyo wakati wa kiliturujia ili kutangaza kipaumbele cha kazi yake. Yeye akiongozwa na Roho Mtakatifu, alitangaza habari njema kwa maskini na ukombozi kwa wanaoonewa, anayafufua matumaini yake na kuwarudishia furaha ya maisha yao.
Yesu anaishi kwa furaha na shauku utambulisho wake kama aliyechaguliwa kutangaza mpango wa upendo na wokovu wa Baba yake. Mungu anapenda kila mtu na kutaka kufikia kila mtu kwa upendo wake. Hata hivyo, ana mahangaiko makubwa kwa baadhi ya watu ambao wanahitaji huduma maalum, kwa sababu wanakataliwa na jamii.
Yesu kama wokovu wa Mungu, yeye ni utimizaji wa Maandiko, lakini katika jumuiya yake alikataliwa kwa wale walijiona waliojua Maandiko. Labda walizoea kukubali tu kile ambacho ni kulingana na mawazo yao, akirekebisha Neno la Mungu kwa njia yao ya maisha, bila tabia nzuri ya kuishi mapendekezo yanayotokana na Neno hili.
Kama watu kutoka Nazareti, mara nyingi sisi pia tumelipinga Neno la Yesu linalouliza maswali kuhusu njia yetu ya kuishi na kudai ahadi kubwa kuhusu hali ya wengine, hasa maskini. Hatuwezi kufikiri kwamba habari tumepokea kuhusu Yesu inatosha kwa safari yetu ya wito. Ni muhimu kuruhusu kwamba yeye mwenyewe aweze kujidhihirisha kwetu kwa nguvu yote ya upendo wake. Tukaribishe ufunuo huu wa Yesu leo ​​kama mwaliko ili tufikiri vizuri kuhusu vipambele vyetu vya thamani na kuchukua ahadi ya mshikamano kwa ajili ya wengine.

Fr. Ndega

quarta-feira, 10 de setembro de 2014

KUHUSU NCHI YANGU BRAZIL




            Brazil ni nchi kubwa zaidi katika Latin Amerika na ni ya sita uchumi kubwa wa Ulimwengu. Lakini inashika mahali themanini na nne wa dunia katika kukuza mwanadamu. Brazil inamilika Majimbo 26 na Wilaya ya Shirikisho moja.  Majimbo yamesambazwa katika mikoa mi tano: Kaskazini, Kaskazini-Mashariki, Mashariki, Kusini na Magharibi-Yakati. Nchi hiyo ina msitu mkubwa na mto mkubwa katika Ulimwengu. Mwaka wa elfu mbili kumi na tatu idadi ya wakazi wa Brazil ilikuwa watu 200,674,130. Kutoka kiasi hicho, Watu Weusi walikuwa 106,000,000, weupe walikuwa 91,000,000, Watu Asia walikuwa milioni 2 na Wahindi walikuwa 896,900.  
            Kuhusu dini, Brazil ina karibu sana dini zote za ulimwengu. Lakini watu wengi ni wakristu (90%): Wakatoliki ni 73% na Waprotestanti ni 17%. Wabrazil wanapenda sana sikukuu. Sikukuu zaidi maarufu ni Kanivali za mchezo wa mpira. Ingawa wanapenda mchezo wa mpira, mchezo wa mfano hasa ni “Capoeira”.  Sahani ya taifa ya Brazil ni “Feijoada”, kwamba inafanywa kwa maharage na nyama ya nguruwe. Kuhusu siasa, Brazil inatawalwa na mwanamke anaitwa Dilma Rousseff ambaye amefanya kazi kizuri. Katika jamii, Nchi yangu ina matatizo mengi: usawa wa vijamii, ukatili wa kijana, trafiki ya madawa ya kuleya, asili janga, nk.  Lakini ninaipenda Nch hiyo.

Fr. Ndega
Mapitio: Mwalimu Patrick
           
                       

quinta-feira, 4 de setembro de 2014

KUHUSU MAISHA YANGU



Mimi ni Josuel dos Santos Boaventura, lakini ninapenda zaidi kuitwa Ndega kwamba inaazimu “Mtu mwema”. Nilizaliwa tarehe ishirini na sita mwezi wa saba mwaka wa elfu moja mia tisa sabini na tatu. Nimetoka Brazil. Jimbo langu ni Bahia na Jina la mji nilipozaliwa ni “Cachoeira”, lakini niliishi daima katika “Conceição da Feira”, kwamba unaitwa pia “Cidade Ternura”, ni kwamba, “Mji wa Huruma”. Niliishi Utoto wangu wote Mjini huo mpaka kwenda seminarini katika mji mwingine, unaoitwa “Feira de Santana”. Shule yangu ya msingi iliitwa “Grupo Escolar Hermilo Cardoso” na Centro Educacional Yeda Barradas Carneiro. Shule yangu ya sekondari iliitwa “Colegio Estadual”. Nilianza kuenda shuleni kuandamana na binamu yangu. Baada ya wakati huo, nikaweza kuenda peke yangu. Nilisoma na nilifanya kazi ngumu sana. Hata hivyo nilipata muda pia kujifunza na kucheza mchezo wa “capoeira”.
Nina familia kubwa kwamba inaitwa “familia ya kasisi”. Baba yangu anaitwa Martins Santos Boaventura. Kazi yake ni kuviweka tayari vyuma kwa kujenga nyumba kubwa. Yeye anapenda kucheza “capoeira” na anacheza ala za muziki vizuri sana. Mama yangu anaitwa Clementina dos Santos Boaventura na anapenda kushona na kutumikia kanisani. Wazazi wangu wangaliendelea wenye nguvu na wananiangalia na upendo muhimu. Nina dada mmoja na kaka sita. Dada yangu anaitwa Joelma na anafanya kazi mkahawani. Kaka yangu mkubwa anaitwa Jose Roque na anafanya kazi kama bawabu wa benki. Kaka yangu Josemir ni polisi. Kaka yangu Josafaa ni mwalimu wa mchezo wa “capoeira” na mchezo wa ndondi. Kaka yangu Josival anafanya kazi katika kiwanda cha karatasi. Kaka yangu Juvandro anafanya kazi katika jiko la watawala wa mji wetu. Mzaliwa wa mwisho Josias ni bawabu wa Kampuni inayochukua pesa.
Katika familia yangu nilikuwa daima mtu maarufu katika sanaa, hasa sanaa ya muziki na kusoma. Kaka zangu na dada yangu walisoma mpaka shule ya sekondari. Nilitaka kuendelea kusoma zaidi ya kaka na dada zangu kwa sababu tangu mtoto mdogo wito wangu ukawa kuwa kasisi, na ili kuwa kasisi ni lazima kusoma sana. Jumapili nikapenda kuenda kanisani kwa misa na kutumikia kama mvulana wa madhabahu. Kama hii, niligundua wito wangu. Wakati mkuu wa maisha yangu ulikuwa nilipoingia seminarini. Kabla ya kuingia seminarini, Nilikuwa nimesitawi tayari vipaji vingi vya muziki kama kuimba na kupiga ngoma. Katika seminari nilipata nafasi kujifunza ujuzi mwingine ambao umenisaidia katika kazi yangu halisi.
Mimi ni kasisi wa Shirika “Poor Servants of Divine Providence”. Nilikuwa kasisi katika terehe ishirini na sita mwezi wa kwanza mwaka wa elfu mbili na mbili. Niliondoka kutoka kwa familia yangu katika Brazil na ninaishi katika Ongata Rongai tangu terehe kumi na nane mwezi wa kuanza mwaka wa elfu mbili kumi na tatu. Nilikuja hapa kwa kufanya kazi katika nyumba ya malezi. Jiukumu hilo linanihitajia busara na uangalivu daima. Zaidi ya jukumu hilo, ninapenda muziki na “capoeira” kwa sababu inafaa kwa afya, mizani na fikira.

Fr. Ndega
Mapitio: Mwalimu Patrick