sábado, 18 de setembro de 2021

NJIA YA UKUU WA KWELI

 

Hek 2:12.17; Yak 3: 16-4:3; Mk 9,30-37

 



 

    Katika ulimwengu wa sasa ambao mbio wa kuchukua nafasi za kwanza, utafutaji wa vyeo na upendeleo, na mwelekeo wa kutaka kuchukua faida juu ya wengine zinaongezeka kila wakati, Neno la Mungu linatukumbusha kwamba ni muhimu kutenda kwa busara na kutafuta maadili ya kweli; hii ni njia ya kipekee ya kupata furaha ya kweli. Mwaliko wa kubadili mawazo na tabia zetu ili tuweze kumfuata Yesu ni wazi kabisa.

    Andiko la kitabu cha Hekima ya Sulemani linaongea kuhusu ushuhuda muhimu wa mtu mwenye haki na upinzani wa wale ambao hawaukubali ushuhuda wake na kumtendea vibaya, hata kwa kupanga kifo chake. Hali hii inatokea kwa sababu ya uaminifu yake kwa Mungu. Mambo yote ambayo washtaki wanasema dhidi ya mwenye haki yanakuwa uthibitisho wa utambulisho wa mtu huyo aliye mwana wa Mungu naye Mungu mwenyewe atamtegemeza na kumtetea dhidi ya adui zake. Huu ndio mfano wa Kristo ambaye aliteseka sana kwa sababu ya uaminifu wake kwa mpango wa Mungu na kwa kujisalimisha kwake aliupata wokovu hata kwa wale waliomkandamiza.  

    Andiko la pili linasema kuwa hekima ambayo inasababisha kujua kamili inatoka kwa juu kwa sababu ni Mungu mwenyewe chanzo cha hekima ya kweli. Mtu anayeongozwa na hekima hii anaweza kuchagua vizuri na kuwa chombo cha amani, cha umoja na cha ushirika katika jumuiya, tena anaweza kuwa tayari kusikiliza maneno ya wengine na kutenda mema kwa ajili yao.

    Injili ni mwendelezo wa tangazo la Petro kuhusu utambulisho wa Yesu na mwaliko wa Yesu mwenyewe ili wafuasi wake wamfuate katika kujisalimisha kwake ili wapate uzima. Yesu alitambua kwamba walihitaji kujua maana kamili ya utambulisho wake kama Masihi na kuyafahamu vizuri mapendekezo yake. Kwa hivyo alitumia nafasi maalum katika mahali pa faragha ili kuwafundisha. Kwa nini hakutaka watu wafahamu alipo pamoja na wanafunzi wake? Kwa sababu wazo wa Masihi ambao watu walikuwa nao ulikuwa mbali sana na utambulisho wake na kwa hivyo lilikuwa hatari kwa malezi ya wanafunzi wa Yesu.  

    Basi, bila kusukumwa na uwepo wa watu, Yesu alijiona mwenye heri kabisa ili kuwaongelea wanafunzi wake kwa uwazi kuhusu mateso, kifo na ufufuko wake, lakini walionekana mbali sana na mwalimu. Hawakuelewa tena kwa sababu walishughulika kwa mawazo na nia tofauti. Kwao ilikuwa muhimu kujadiliana juu ya msimamo na upendeleo kuliko kuandamana na mwalimu wao kwenye kujisalimisha. Hivyo tunaona kwamba hata wanafunzi waliingia nyumbani pamoja na Yesu, inaonekana wanaendelea nje. Kwa hivyo Yesu anawaita kwako kama ilivyotokea mara ya kwanza, yaani anawalika ili waweze kuishi kwa ushirika nawe na hisia yake na mawazo yake na kupata kufahamu maana ya kujitolea kwake hadi upeo.

    Kwa uvumilivu na kwa kutumia mtoto kama mfano, yeye aliwasaidia kufahamu ufunuo wake na masharti ya kumfuata. Yule anayeamua kumfuata Yesu anapaswa kuongoza maisha yake kulingana na njia tofauti na mawazo wa dunia. Ikiwa katika nafasi iliyopita Yesu aliwaomba kuyatoa maisha ili kuyaokoa, hapo aliwaomba kuwa wa mwisho na mtumishi ili kuwa wa kwanza.

    Yesu anadhihirisha utambulisho wake kama Mwana wa Adamu (mtu). Katika Agano la Kale tunakuta maneno haya katika vitabu vya nabii Danieli na Ezekieli. Kulingana na Danieli maneno haya yaongea kuhusu hali ya utukufu wa yule ambaye atakuja siku ya mwisho (Dan 7:13). Kulingana na toleo la Ezekieli maneno Mwana wa Mtu yanatumiwa na Mungu kwa uhusiano na nabii wake na kuonyesha hali ya udhaifu na kifu cha binadamu (Ezk 2:1, 3:1.25, 17:2). Basi, hii ni maana iliyotumiwa na Yesu ili kuongea kuhusu utambulisho wake kwa uhusiano na hali ya binadamu na fumbo la mateso, kifo na ufufuko wake ambalo lilisababisha ubinadamu mpya. Hivyo, tunafahamu maana ya ufundishaji wa uvumilivu  wa Yesu ili kuwasaidia wanafunzi wake walio na ujinga na udhaifu wa akili.

    Watoto wadogo wana nafasi maalum moyoni mwa Yesu. Alisema kwamba Ufalme ni wao naye mtu anayetaka kuingia katika Ufalme huu anapaswa kuwa kama watoto. Mfano wa watoto wadogo ni maalum kwetu kwa sababu hao wanatusaidia kutafuta muhimu zaidi ya maisha, yaani ukweli, unyenyekevu wa moyo, kuamini, n.k. Kama vile wanafunzi wa kwanza sisi pia tuko na ugumu wa kufahamu mambo yote kumhusu Yesu na mapendekezo yake, lakini tukimruhusu, yeye anaweza kufungua akili zetu na kubadilisha moyo wetu ulingane na matarajio yake. Siku ya leo yeye anatualika kwa uhusiano wa kibinafsi naye. Kupitia uhusiano huu peke yake tunaweza kuingiza utambulisho wake na kufahamu maana ya ushiriki wetu katika kazi yake ya ukombozi. Mfano wa watoto wadogo utusaidie kufahamu nia ya Yesu kuhusu maisha yetu na kukubali mapendekezo yake kwa kutumia nguvu zetu kwa ajili yake “mpaka kifo, mpaka uzima”.

 Fr Ndega

Nenhum comentário: