sábado, 10 de novembro de 2018

ISHARA KUU INATOKANA NA MOYO WA UKARIMU



Kutafakari kutoka 1 Waf 17, 10-16; Waeb 9, 24-28; Mk 12: 38-44


       Mungu hawezi kushindwa katika ukarimu. Yeyote anayetenda kwa ukarimu atapokea ukarimu mwingi zaidi kutoka kwake. Hilo ndilo ambalo wajane wa Liturjia ya leo wanatufundisha. Katika andiko la kwanza, Eliya alitumwa kwa mjane katika Sarepta. Kukutana na mtu huyo wa Mungu matarajio ya maisha ya mama mjane na mtoto wake yalibadilisha kabisa. Hao walikuwa wanaishi mazingira magumu sana, yaani: “tuweze kula na kufa”. Jibu lake la ukarimu kwa ombi la nabii linaonyesha tabia ya kuamini katika riziki ya Mungu ambaye hakuna kisichowezekana. Mwishoni muujiza ulitokea kwa njia ya ajabu. Sisi twalikwa kuwa na tabia hii ili tendo la neema ya Mungu maishani mwetu liwe ufanisi.

     Kifungu cha waraka wa Waebrania kinaongea kwamba Kristo alikatisha dhambi zake kwa kujisalimisha mwenyewe msalabani. Hili ndilo fumbo ambalo ametuokoa nasi tunaguswa kwa njia mpya daima katika kila Ekaristi ambayo tunasherehekea. Hili silo tukio la kihistoria tu bali nafasi ya kushiriki katika maisha ya Kristo mwenyewe ambayo inatuimarisha kuendelea kazi yake kwa kuyatoa maisha yetu kama yeye alivyo.

     Sehemu ya kwanza ya Injili inajulisha upinzani wa Yesu dhidi ya njia ya waalimu wa sheria ya kuishi. Hao wanapenda sana kujiinua na kupendezwa. Wanasali kwa muda mrefu lakini bila kusudi kamili. Wanajihisi bora kuliko wengine na kudhulumu wajane. Yesu ana wasiwasi kuhusu njia hii ya unafiki kwa sababu inalipinga pendekezo lake kwa wanafunzi wake.

      Watu walijua kwamba kuna tofauti hasa mfarakano kati ya mafundisho ya Yesu na ya waalimu wa sheria. Yesu aliwafundisha watu kwa mamlaka aliyopokea kutoka kwa Baba. Kuhusu mamlaka ya walimu wa sheria, yakosa ukweli. Baada ya uhuru kutoka utumwani Babeli walimu walikuwa viongozi muhimu kwa ajili ya Wayahudi kwa sababu waliandika Vitabu Vitano via mwanzo wa biblia vinavyojulikana kama Vitabu vya Musa, yaani Toraa na hao peke yao waliweza kuhukumu na kujulisha sentensi kulingana na sheria. Hao waliwasisitiza Wayahudi kuzingatia agano kwa kuzishika sheria za Mungu kama msingi wa taifa lao jipya. Lakini ingawa waliwafundisha watu waishi sheria, tabia yao ilikuwa mbali sana na mafundisho yao.

     Utumiaji mbaya wa mamlaka ni majaribu daima katika maisha ya walio na jukumu la kuwaongoza watu katika jumuiya zetu za Kikristu na pia katika jamii. Lakini sio hao tu ambao wanaguswa na majaribu haya. Hata sisi pia tuko na mwelekeo huu. Majaribu ya kawaida ni yaani kujiona bora kuliko wengine, kutaka kutumikiwa badala ya kutumikia, kuwanyonya wengine na kadhalika. Yeyote ambaye anataka kuwaongoza wengine anapaswa kuiga mfano wa Yesu aliyekuwa na mawazo tofauti na kujua njia kamili ya kushinda majaribio yote. Hatuwezi kumpendeza Mungu wala kuwa wenye furaha ikiwa hatuishi majukumu yetu kama utumishi.  

     Lakini katika sehemu ya pili ya injili hii tuko na njia kamili ya kuwa mwanafunzi wa Yesu, yaani mfano wa mama mmoja mjane maskini aliyeenda hekaluni kutoa sadaka yake. Yesu alikuwa ameketi karibu na sanduku la hazina pamoja na wanafunzi wake. Alitazama jinsi watu walivyoweka pesa sandukuni. Yeye aliweza kuona moyo na kusudi kwa kila mmoja alipotoa sadaka. Alipotazama mjane akiweka fedha sandukuni yeye alitambua kwamba mama huyo alitoa zaidi kuliko wengine kwa sababu sadaka zao zilikuwa ziada ya matajiri bila kusudi kamili kwa moyo. Sadaka ya mjane ilimpendeza Mungu kwa sababu alitoa kila alicho nacho cha kuishi, yaani alitoa maisha yake kama zawadi, kama sadaka. 

     Mama mjane maskini hakumjua Yesu, lakini alimpendeza kwa sababu alitenda kulingana na pendekezo la binadamu mpya.  Mtu anakuta maana ya kweli ya maisha wakati anapoweza kutenda kama Mungu katika ukarimu wake, yaani zaidi kuliko kutoa kitu, mtu anaweza kujitoa mwenyewe kama sadaka yote kwa kuonyesha kwamba maisha yake ya kila siku yanamtegemea Mungu. Tuko na tabia ambayo inadhihirisha ukuu wa moyo wa mtu fulani.

    Tunaalikwa kwa macho kwa ishara halisi ndogo zinazotoka kwa watu unyenyekevu tunaowakutana kwa kawaida na kujifunza kutoka kwao tabia kamili mbele ya Mungu. Yeye hupendezwa sio na wingi wa vitu ambavyo tunatoa bali na ukarimu wa moyo wetu. Thamani ya sadaka yetu hupimwa kulingana na ukarimu wetu. Ukuu wa mtu hautokana na kipimo cha zawadi ambayo anatoa bali na uzuri wa ishara yake na upendo wake. Kweli, ndizo ishara ndogo zinazofanya tofauti. Msaada mkubwa ambao ninaweza kumpa wengine ndimi ninayealikwa nilivyo. Zaidi ya hilo ndio unafiki ambao unanizuia kuwa na uhusiano mwema na wengine. Tunaweza kushinda hali mbaya hii kwa msaada wa watu wanyenyekevu ambao wanajenga undugu kandokando yetu na kuwa maonyesho ya ukarimu wa Mungu.

Fr Nega

Nenhum comentário: