sábado, 29 de setembro de 2018

WANAFUNZI WENGINE WA YESU



Kutafakari kutoka Hes 11:25-29; Mk 9:38-43, 45, 47-48

Mungu hawabagui watu kwa maana anapenda na katika upendo hakuna ubaguzi. Matarajio yake ni watu wake wote wawe manabii, wakisikiliza neno lake na kuongea katika jina lake. Kupitia Roho wake Mtakatifu, anatuimarisha tuwatendee wote mema kulingana na mapenzi yake, akidhibitisha kwamba upendo wake hauna mpaka. Mbele ya Mungu hakuna mtu wa heshima kuliko wengine. Yeye hakubali umaarufu au ubaguzi, bali anatarajia ahadi kwa njia yake ya kufikiri na kutenda. Anatenda hivyo kwa sababu ya upendo Wake mkubwa.

Mtakatifu Yakobo anakosoa kwa nguvu watu wanaokuwa tajiri kwa njia ya udhalimu kwa kukanusha mishahara kwa wafanya kazi. Mungu anapinga hali ya udhalimu na kosa la usawa kati ya watu. Yeye ndiye tayari kutenda kwa ajili ya walio waathirika wa udhalimu na kumwomba kwa imani. Ukosoaji huu unatumika pia kwa wote ambao wajikabidhi katika mali ambayo anayo kuliko riziki ya Mungu. Mtu anapokufa hawawezi kuchukua mali chochote pamoja naye; kwa hivyo tabia ya kuongeza mali kwa nafasi yake mwenyewe haina maana.

Wanafunzi wa kwanza walijaribu kumkataza mtu fulani ya kufanya mwujiza kwa jina la Yesu kwa sababu hakuwa mmoja wao. Walifanya hivyo kwa mamlaka gani? Yesu hakukubaliana na tabia hii na kuwaambia kwamba mtu anayetenda mema kwa jina lake (Yesu) hawezi kumtendea vibaya. Kisha akiendelea kwa mafundisho yake, alisema kwamba watu wanaosaidia wafuasi wake watapokea tuzo kwa sababu ya utambulisho wake na wale waliotumiwa kwa jina lake. Yesu anawakumbusha pia kwamba mambo yote wanayofanya wale wanaomfuata yapaswa kuwaimarisha watu kumwamini Kristo. Ni lazima kuepuka Kashfa kwa sababu tabia hii inavuruga imani na kukana utambulisho wa wanaomfuata Yesu.

Tumetafakari kuhusu ugumu wa wanafunzi wa Yesu kuelewa na kuyapokea mafundisho yake. Kujaribu kumkataza mtu fulani ambaye alifanya mema kwa jina la Yesu ni ishara ya ugumu ya kumfahamu Yesu na mapendekezo yake. Maana ya kuwa mfuasi wa kweli wa Yesu siyo maneno tu, bali ni matendo mema hata kama yeyote hahudhurii kikundi. Badala ya kuwakataa wengine ambao wanatenda mema kwa jina la Yesu, wanafunzi wake wanapaswa kujikataa wenyewe. Kuwa mwanafunzi wa Yesu kunamaanisha kuishi imani iliyoonyeshwa kwa matendo. Kwa Yesu wale wanaosikiliza Neno la Mungu na kuweka vitendoni ndio mama na ndugu zake na wanafunzi wake. Hivyo yule aliyetenda mema kwa jina la Yesu anaweza kufikiriwa kama mwanafunzi wake. Mtazamo wa wanafunzi ndio tofauti na ule wa mwalimu wao kwa sababu lengo lao sio kukaribisha bado bali ubaguzi.

Kitu muhimu katika dini au imani ni matendo na siyo maneno tu. Matendo husema zaidi kuliko maneno. Wakristo wa kwanza ndio mfano halisi kwa sababu waliweza kuwavutia wengine si kwa maneno, bali kwa njia yao ya maisha. Kuhusu hao watu walisema: “Mwone kama wanavyopendana”! hali hii iliwezekana kwa sababu ya upendo wao ulionyeshwa kupitia ridhaa wao kwa wao, kushiriki pamoja, uvumilivu katika maombi pamoja na unyenyekevu wa moyo. Kuhusu hayo Sinodi ya Afrika imesema: “Sharti muhimu la kuhubiri ni ushuhuda wa maisha”. Mwanafunzi wa kweli wa Yesu hawezi kuwa na ubaguzi na kuamini kuwa watu wa kundi lake pekee ama kanisa lake ndiyo wanafunzi pekee wa Yesu na kwamba ndio hao peke yao ambao wameokolewa.

Hatuwezi kufikiri kwamba Yesu ni mali yetu. Ikiwa tunahisi karibu na Yesu, hatuwezi kuishi mbali sana na ndugu zetu, kufungwa kabisa kwa hali kandokando yetu na hata kufikiri kwamba tunakuwa na mamlaka ya kuwazuia wengine watende kwa jina la Yesu. Tuko mbele ya kosa kubwa. Tuwe macho kuhusu baadhi ya uzoefu ambao unatufungua kwa Mungu lakini unatufunga kwa wengine. Ikiwa imani yetu haituongozi kukutana na wengine na kutambua mema ambayo wanaweza kufanya imani yetu ni utenganisho. Basi, ili Mungu atufundishe kutambua mwendelezo wa kazi zake mbele ya matendo mema ya Wakristo na kusaidiana kwa wema wa wote.

Fr Ndega

Nenhum comentário: