sábado, 15 de setembro de 2018

UAMINIFU WA MUNGU NI NGUVU YETU


Kutafakari kuhusu Isa 50:5-9; Yak 2,14-18 Mk 8:27-35


     Mtumishi wa Bwana anajiona kuimarishwa kwa sababu ya uhakika wa upendo na utunzaji wa Mungu daima maishani mwake. Uhakika huu unamfanya imara mbele ya mateso mengi. Yule ambaye anamtumainia Bwana habaki kuchanganyikiwa na mwenye udanganyifu kwa sababu “uaminifu wa Bwana ndio nguvu yetu”. Mtakatifu Yakobo anawaomba Wakristo wawe walio halisi katika njia ya kuamini. Imani inayoonyeshwa kwa maneno peke yake siyo kweli. “Maneno yatoweka hata ikiwa yanaonekana yawe na imani. Matendo yanaiweka halisi kwa kuifanya iwe iko na sasisha”. Basi, ndiyo matendo mema ambayo yadhihirisha ukweli wa imani yetu. Madre Teresa wa Kaukuta alikuwa na haya ya kusema: “Kila tendo la upendo linalofanyika kwa moyo linaweka halisi imani kwa kumkaribia Mungu”.

      Yesu alikuwa anatembea pamoja na wanafunzi wake. Walipofika karibu na Kaisaria Filipi aliwauliza maswali kuhusu utambulisho wake kulingana na mtazamo wa watu. Majibu yalikuwa ishara ya kwamba mawazo kuhusu Yesu hayakuwa wazi sana kwa upande wa watu. Ingawa hayakuwa wazi kwa watu, ni lazima kuwa tofauti kwa mitume kumi na wawili, kwa sababu kwa Yesu haikuwa muhimu sana yale ambayo watu walifikiri, bali imani na kukiri kwa wafuasi wake. Petro alidhihirisha yale ambayo wanafunzi wengine kumi na mmoja walijua pia: Yesu ni Masiya wa Mungu. Lakini hawakuweza kuitangaza habari hii kwa sababu ya kosa la maana kamili. Yesu alitambua kwamba wafuasi wake walihitaji kujua kwa kina maana ya utume wake kama Masiha na masharti kwa kumfuata kwa kweli.

        Mawazo ya wafuasi wa Yesu kuhusu Masiya yalifuata matarajio ya Wayahudi wengine, yaani, Masiya wa kisiasa atakayetumia nguvu zake za kimungu ili kuwakomboa Wayahudi toka ukoloni wa Warumi. Bila shaka Yesu alikataa mawazo hayo kwa kuonyesha njia tofauti ya kutimiza mpango wa Mungu, yaani kupitia mateso, kifo na kufufuka. Njia aliyochagua Yesu ni ile ya mtumishi wa Bwana wa nabii Isaya. Utambulisho wa mtumishi huyo ni kuwa makini kwa sauti ya Mungu ili aweze kufanya mapenzi yake kwa kutumikia kabisa. Kwa kufanya mapenzi ya Mungu mtumishi huyo alipaswa kuteseka na kufa, lakini alisimama upande wa Mungu ambaye alimsaidia akimfanya mshindi. Itikio la Petro lilidhihirisha upinzani dhidi ya njia ya maisha Yesu aliyochagua ili atimize mapenzi ya Mungu. Uamuzi wa Yesu ulikuwa katika ushirika na Baba yake na upinzani dhidi ya njia hii ni upinzani dhidi ya mapenzi ya Mungu.

        Wanafunzi wa kwanza walihitaji mwendo wa muda mrefu ili kujifunza kumhusu Yesu na kuyafahamu mapendekezo yake sawasawa. Yesu alimkemea Petro lakini alimwalika afuate mtazamo wa Mungu ili awe mwanafunzi wa kweli. Kidogo kidogo wote walitambua kwamba kwa kujitoa kama Yesu alivyo, walipaswa kuzifuata hatua tatu, yaani, kujikana wenyewe, kuichukwa misalaba yao na kumfuata Yesu. Kwa maneno mengine, walipaswa kuyabadilisha maisha yao kabisa. Wale ambao hukutana na Yesu hawakubaki walivyo na hawawezi kumwomba Yesu atende kulingana na mapendekezo yao. Mwendo wapaswa kuwa tofauti. Kwa kumfuata Yesu kweli tunapaswa kupatikana kwa mambo yote kwa ajili ya ufalme wa Mungu kwa kuyaingiza mapendekezo ya Yesu. Tunapaswa kufananisha maisha yetu kulingana na njia ya Yesu ya kuishi  na kuchukua msalaba kama yeye alivyo.


     Injili siku ya leo inatusaidia kutafakari kuhusu njia ambayo tumechagua ili kumfuata Yesu. Je, hii ni njia ya kweli? Tunatambua kwamba Kumfuata Yesu hakuuleti upendeleo au hadhi, bali mateso na kujisalimisha kwa ajili ya injili. Basi, yeyote ambaye anataka kuishi kwa shwari na bila ahadi hawezi kumfuata Yesu. Yeyote ambaye anatamani kumfuata Kristo bila msalaba hatamfuata Kristo kwa kweli kamwe. Kupitia mambo hayo tunaweza kujiuliza maswali: Je, Kristo gani tumemfuata? Mawazo au kitu gani tunahitaji kujinyima bado ili tuweze kumfuata Yesu kikamilifu? Maisha yetu ya kawaida ni ishara ya kwamba tumekuta hazina yetu ya kweli? Tuishi wito wetu wa wanafunzi wa Yesu kwa shauku na furaha kwa sababu Mungu ndiye mwaminifu na kuwa tayari daima kutusaidia hasa wakati tuko na ugumu wa kubeba msalaba wetu. Tumwaminie yeye kwa sababu uaminifu wake ni nguvu yetu.

Fr Ndega

Nenhum comentário: