sábado, 27 de janeiro de 2018

HAJA YA MAFUNDISHO MAPYA


Kutafakari kutoka Kumbukumbu la Sheria 18: 15-20; 1Wak 7: 32-35; Marko 1: 21-28



Masomo haya ni mwaliko ili tukaribishe mafundisho ya Neno la Mungu ambalo lina uwezo wa kubadilisha maisha ya watu kwa kuwapa uwezo ili wawe wajumbe wa wakati mpya. Andiko la linataja mfano wa nabii atakayechukua nafasi ya Musa na kuzungumza na watu kwa jina la Mungu. Nabii ndiye mtu anayechukuliwa na hali ya watu ili kuongea nao yale ambayo Mungu anamwuliza kusema tu. Msukumo wa Mungu, pamoja na upatikanaji wa nabii, ulifanya tofauti kubwa maishani mwa Waisraeli, ukiwaongoza kuyaona maisha mapya. Mt. Paulo anaonyesha tamani yako ili watu wa jumuiya ya Kikristo waweze kuishi bila wasiwasi kwa sababu tabia hii ndiyo matokeo ya hofu nayo inazuia ushuhuda wa kweli. Jumuiya inaalikwa kufanya upya ahadi yake ya imani katika Bwana Yesu Kristo, ndiye mfano yetu ya kujisalimisha mikononi mwa Mungu.

Baada ya ubatizo na uzoefu jangwani, Yesu alianza kazi yake akitangaza Ufalme wa Mungu na kuwaalika watu watubu. Yeye hupenda kutembelea na kufundisha katika masinagogi kwa sababu katika mahali hapo kwa kawaida watu hukusanya wasikilize Neno la Mungu na kuyakubali mapenzi yake. Mamlaka aliyopokea Yesu kutoka kwa Baba yanaonyesha kwamba mafundisho yake ni vizuri kuliko waandishi. Kidogo kidogo watu walielewa kwamba mtu huyo Yesu, ambaye alizungumza kwa upendo na ukweli, alikuwa mjumbe wa Mungu. Maneno yake yana uhai kabisa na kuongoza kwa mabadiliko ya maisha. Wale ambao wana kazi ya kuwaongoza watu, wanapaswa kuisikiliza sauti yake.

Hata pepo wachafu wanautambua utambulisho na mamlaka ya Yesu, lakini hawashiriki hisia zake na ahadi yake kwa ajili ya watu. Kwa hivyo, Yesu hazungumzi nao; yeye anawaamuru wanyamaze tu. Pepo wachafu hawa ni ishara ya upinzani dhidi ya mpango wa Mungu, kuwadhoofisha watu na kuwazuia kuishi uwezo wao kikamilifu. Mbele ya nguvu hizi, Yesu anaweka mamlaka na kutenda kama Mkombozi.

Uwepo wa Yesu kati ya binadamu unaanzisha wakati mpya, yaani wakati wa wokovu wa Mungu. Kupitia matendo ya Yesu, Mungu anaonyesha upendo na utunzaji kuhusu maisha ya watu wake. Yale ambayo Yesu anatenda ndiyo kulingana na maneno anayosema. Kwa hivyo mafundisho yake yanafikiriwa mapya sana. Yeye ni Masiya wa Mungu anayetabiriwa na manabi wengi na kutarajiwa kwa muda mrefu sana. Lakini haitoshi kuutambua utambulisho wa Yesu kama Masihi wa Mungu, kwa sababu hata pepo wachafu walivyo. Mtakatifu Agustino alisema: “Usijiridhishe kwa kumwamini Mungu; hata pepo wachafu walivyo.” Ni muhimu kukubali pendekezo la Yesu la toba na kuweka juhudi kwa kufanya uhusiano mwema na Mungu na wengine. Upinzani dhidi ya Yesu ni upinzani kwa mafanikio wa Ufalme wa Mungu. Yesu wakati alipotangaza habari njema ya Ufalme, akawaomba watu ushiriki kwa hiari. Jibu ambalo anatarajia kutoka kwetu ndilo kutafuta kwa Ufalme huu kama kipaumbele, kwa sababu hii ni maana ya maisha na kazi zetu.


Ujumbe wa injili hii ni pendekezo la uanafunzi upya. Ni mwaliko kwetu ya kujisalimisha kwa ajili ya Yule ambaye ametuita na kutaka tuwe wajumbe wake. Yeye hujitambulisha na wale waliomfuata. Yesu anaendelea kutenda dhidi ya nguvu zote au mawazo ambayo yanayaogopesha maisha ya watu. Kwa maneno mengine, kupitia matendo yetu, ishara za ukombozi wa Kristo bado zinatokea katika maisha ya watu wengi. Kutoka kwake tunaupokea uwezo ili tuwe mashahidi wa kweli kwa kutangaza ukweli wa ufalme wake kupitia tabia zaidi kuliko maneno. Hakika Yesu anaandamana nasi katika safari yetu, kutuhamasisha kupigana dhidi ya maovu na dhambi ambayo inatuzuia kumtumikia Mungu kwa ukarimu na hiari. Neno lake ni pendekezo ambalo tunataka kuchukua kama sheria ya maisha. Neema yake itusaidie kuchukua ahadi hii. 

Fr Ndega

Nenhum comentário: