terça-feira, 27 de setembro de 2016

HALI YA MASKINI INATUHUSU SISI


Kutafakari kuhusu Lk 16, 19-31

     Mungu anashutumu kutofautiana na unafiki katika safari ya watu wake na anapendekeza njia tofauti. Kulingana na somo la kwanza, utumwa katika safari ya Waisraeli ulikuwa matokeo ya kosa la uhusiano mwema na Mungu na la ahadi ya kuujenga undugu. Ibada yao ilibadilika kuwa jambo bila maana, yaani haikuonyesha tena ukarimu wa moyo wala haikusababisha mabadiliko katika uhusiano miongoni mwa watu na katika jamii. Walio na nguvu waliishi kwa kutofautiana mbele ya hali ya wengine na matendo ya nje hayakuihusu tabia ya ndani. Wakitenda hivi walivutia hali mbaya kwa maisha yao. Lakini tunajua kwamba Mungu hakuwaacha watu hawa, akitenda kwa uaminifu hasa kuhusu hali ya maskini na wasio na nguvu kwa maana maisha yao yanathamini sana kwa Bwana. Somo la pili linaonyesha ushuhuda wa Mtakatifu Paulo kuhusu Timotheo. Kulingana na ushuhuda huu haiwezekani kuwa mtu wa Mungu kwa kulitumia jina tu. Utambulisho wa mtu wa Mungu wa kweli unaonyeshwa kupitia kufuata haki, utawa, imani, upendo, uvumilivu na upole.   

       Kama tujuavyo, mifano ni sehemu ya ajabu ya ufundishaji wa Yesu. Kupitia mfano yeye anaweka rahisi na kupatikana kwa wote siri za Ufalme wa Mungu. Katika andiko hili, Yesu anasimulia mfano wa mtu tajiri na Lazaro maskini anawaonya wasikilizaji wake kuhusu hali ijayo iliyo matokeo ya chaguzi za watu katika wakati huu. Mtu tajiri ni ishara ya walio na mazoea ya kuitumainia mali bila kuguswa na hisia kuhusu kile kinachotokea kandokando yao. Hao walichagua kwa nafsi yao njia ambayo itawaongozea mauti. Lazaro ni ishara ya walio maskini ambao wameachwa bila ulinzi na utunzaji; wanapiga kelele ili wapate nafasi ya kuishi kwa heshima. Tena Lazaro ni pendekezo la kuishi tofauti, kuyalenga maisha katika thamani za kweli. Huyo ni ishara ya uvumilivu, ya mapigano na mwaliko wa kumtumainia Mungu ambaye katika riziki yake hawaachi wale ambao wanamwamini.

       Kupitia mfano huu Yesu anatukumbusha kuhusu hali ya kikatili ambayo ipo katika jamii yetu, yaani kutokuwa na usawa kati ya watu. Katika mafundisho yake, Kanisa limeshutumu hali hii mara nyingi kwa kusema, “Hali mbaya ya jeuri imezaa matajiri walio na utajiri zaidi daima juu ya maskini walio maskini zaidi daima.” Hali hii ni tofauti kabisa na matarajio ya Mungu ambaye, kulingana na wema wake, ananyesha mvua kwa wenye haki na wasio na haki, tena kwa walio wema na kwa wabaya ili vitu vyote alivyoumba kwa wote vipatikane kwa wote. Mfano mzuri tunapata katika Wimbo wa Bikira Maria ambao unaishuhudia njia ya ajabu ya Mungu ya kutenda, yaani yeye huwashusha wakuu na kuwapandisha wadogo ili waweze kuishi pamoja kama ndugu na kwa usawa wa haki na wa heshima. Mungu anajitambulisha na hali ngumu ya wasio na nguvu na ya maskini. Udhalimu wote unaofanyika kwao unamgusa Mungu ndiye kuwepo katika upande yao. Katika wakati ujao, baada ya hali ya dunia, hali itakuwa tofauti, yaani waliopokea mambo mema katika maisha yao bila ahadi na hisia kuhusu hali ya wengine wataumizwa na wale waliopata mabaya kama Lazaro alivyo, watafarijiwa. Yeyote ambaye anatumia mali yake ili awadharau wengine anatupa maisha yake takatakani kwa sababu maisha hayamaanishi mali mengi bali uwezo wa kutenda mema. Kuhusu mambo haya Mt. Yohana Calabria alikuwa na haya ya kusema: “Maskini wako ili matajiri waokoke/waokolewe”. 

     Hali ya maskini ina uhusiano na sisi sote, kwa sababu “dhambi ya jamii ni matokeo ya kiasi cha dhambi za kibinafsi”. Basi, ni lazima toba/mabadiliko sio kwa ajili ya dhambi za kibinafsi tu, bali pia kuchukua jukumu kuhusu dhambi ya kijamii. Mwendo huu unaweza kwanza kupitia tabia ya kuacha njia ya ukusanyaji ambayo kwa kawaida inatuongoza kuwa na kutofautiana kuhusu hali ya wengine. Tunaalikwa kuchukua njia ya unyenyekevu inayokihusu kitu kidogo na kutufanya kuguswa na hisia kuhusu wale wasio na kitu. Mungu anatuokoa maana ya upendo wake, lakini anathamini sana juhudi zetu kama alivyosema Baba Mt. Benedito wa kumi na sita: “kwa kweli, wokovu ni zawadi iliyo neema ya Mungu, lakini ili uwe ufanisi katika maisha yangu unadai ridhaa yangu, ambayo inaonyeshwa kupitia matendo, yaani kupitia utayari wa kuishi kama Yesu alivyo kwa kuufuata mfano wake.” 

Fr Ndega

Nenhum comentário: