domingo, 24 de maio de 2015

NGUVU KUTOKA JUU


Mdo 2: 1-11; 1Wak 12: 3b-7, 12-13; Yo 20: 19-23

       Tunaadhimisha sikukuu ya Pentekoste, hitimisho ya siku hamsini za muda ya Paska  na ukamilifu wake. Sikukuu hii inasherehekea ujio wa Roho Mtakatifu juu ya wanafunzi wa kwanza na mwanzo wa ujumbe wa Kanisa, Jumuiya ya Agano Jipya. Pentekoste inasherehekea pia uhakika wa uwepo wa Roho kanisani na ndani yetu. Hiyo ni Roho ya Yesu na Baba; huyo ni Roho ya Faraja kwa wale wanaohisi kutokuwako kwa Yesu; ni Roho ya Nguvu kwa wale wanaohitaji ujasiri ili kuwa mashahidi wa kweli wa Yesu kwa wote; ni Roho ya umoja ili ushahidi kuhusu Yesu uwe wa kuaminika.
           
           Masomo, hasa somo la kwanza na somo la tatu, yanaanzisha kuongea kuhusu baadhi ya mahali ambapo wafuasi walikuwa wamekusanyika, kushiriki pamoja matarajio yao na ahadi, lakini si kwa msukumu sana kwa sababu ya upinzani wa jamii ya Wayahudi dhidi ya mafundisho ya Yesu na wafuasi wake. Yesu aliahidi kuwa pamoja nao siku zote na aliwashauri kusubiri nguvu kutoka juu, ambayo angekuja juu yao karibuni. Hivyo waliimarisha imani yao katika neno la Yesu na wakasubiri kwa uvumilivu, wakimwomba Mungu ili wapate nguvu hii. Ghafla, kwa mujibu wa muda na mapenzi ya Mungu, Roho akaja akijaa wote na mahali mote. Kulingana na Injili ya Yohana zawadi hii kuu ya Roho Mtakatifu ilitolewa katika siku moja ya Ufufuko kama maonyesho ya maisha mapya ya Yesu kwa wote. Sikukuu ya Pentekoste ya Wayahudi ikawa Sikukuu ya uumbaji mpya kupitia ya kitendo cha Roho ya Yesu. Wote walibadilishwa na kuumbwa tena. Kama hii, kanisa, jumuiya ya wafuasi wa Yesu, lilianza safari lake kwa umoja, kwa nguvu na linalofunguliwa kwa dunia nzima.

       Yesu aliivuvia Roho yake juu ya wanafunzi wake. Kupitia tendo la Roho wake Mtakatifu jumuiya ya kikristo alipokea zawadi ya amani na furaha ili kutangaza matendo ya ajabu ya Mungu, ikisaidia maridhiano kati ya watu. Zawadi ya lugha tofauti inaonyesha kwamba Kanisa linaitwa ili kuwa uwepo katika hali halisi ya watu na kuongea nao kutumia lugha rahisi, ambayo inajenga ufahamu na ushirika. Kupitia tendo la Roho Mtakatifu watu wote wameitwa kwa ushirika na udugu, ni kwamba, kutoka lugha nyingi kwa lugha ya kipekee, lugha ya upendo. Lugha za binadamu na upendo wa Mungu ni mchanganyiko ili kutokea, kutokana na tamaduni zote, watu wamoja tu, watu wapya kabisa wakitangaza maajabu ya Bwana kwa njia tofauti.

        Liturujia hii ni mwaliko kwa umoja na upendo wa Kristo. Kama wakristo sisi ni sehemu za mwili wake. Mwili huu unahitaji kutenda vizuri ili kufikia lengo lake. watu wanahitaji si tu kusikiliza mambo mema kuhusu Yesu, lakini wanahitaji pia kuona ukweli wa tangazo hili kupitia  ushuhuda wa ushirika wa Wakristu. Mtakatifu Yohane Paulo wa II aliandika katika waraka Ut Unum Sint kwamba kutafuta umoja na ushirika kamili miongoni mwa Wakristo sio shughuli huria, lakini ni sehemu ya ujumbe wa Kanisa kama mtumishi wa Kristo (UUS, 20). Kama jumuiya ya kikristo tunahitaji kuchukua ahadi hii kwa njia ya Kristo, kwa mujibu njia yake ya kufikiri, kuhisi, kutenda. Ingawa siku za nyuma zilikuwa chungu kwa Ukristo na inaendelea kusababisha majeraha mengi miongoni mwa Wakristo, sisi tunahamasishwa kwa upendo na neema ya Roho Mtakatifu kusameheana na tuishi kwa kurudiana. Maridhiano ni zawadi iliyopewa jumuiya ya kikristo kama ujumbe na kigezo kwa umoja, kulingana na matarajio ya Kristu, “ili wao wawe kitu kimoja”. Roho Mtakatifu atusaidie katika lengo hili.

Fr Ndega

Mapitio: Sara

Nenhum comentário: