domingo, 24 de maio de 2015

INGILI HAINA MPAKA


Mtdo 1, 1-11; Waef 4, 1-13; Marko 16, 15-20

       Sikukuu ya leo inatufafanulia fumbo la uwepo wa Yesu. Yesu hakuiacha mbingu alipokuja kwetu na hakutuacha alipochukuliwa mbinguni. Kupaa kwake Yesu kunaongea kuhusu njia mpya ya uwepo wake miongoni mwetu, kutangaza hatua mpya ya kazi yake. Huu ni wakati wa Kanisa, jumuiya ya wanafunzi wa Yesu. Ujumbe muhimu kuhusu huo ni wazi sana katika maandiko mawili ya Luka, Injili na Matendo ya Mitume. Katika Injili anazawadisha vitendo ya Yesu, na andiko la Matendo ya Mitume anazawadisha vitendo ya wanafunzi wake waliosaidiwa na Roho wake, aliye njia mpya ya uwepo wa Mungu miongoni mwao.    

        Mizimu ya Yesu kwa baadhi ya muda iliwahamasisha wanafunzi wake kujipatia maana ya uanafunzi, wakishinda hofu na mashaka kuhusu hali ya ufufuko wake. Uzoefu huo wote ulikuwa mpya sana kwao na Yesu alifahamu kwamba ilikuwa lazima kuwa na utulivu kwa sababu imani yao ndogo. Mwendo ulikuwa mrefu, lakini ufanisi sana, ukisababisha mabadiliko makubwa maishani mwa wanafunzi: kutokana na wanaume wenye hofu kwa mashahidi wenye ujasiri. Katika maneno ya mwisho kwao, Yesu aliwasaidia kufahamu uhusiano kati ya kila kitu alichotenda na kufundisha na hali halisi ya Ufalme wa Mungu. Hali halisi ya Ufalme wa Mungu ilidhihirishwa kupitia ishara za Yesu na inaendeleza kupitia matendo ya wale wanaouchukua ujumbe wako mpaka miisho ya ardhi. Kuongoja kujaa na nguvu kutoka kwa juu ni kujisalimisha kwa tendo la Mungu kama vyombo vya wokovu wake. Kazi hii haitoki kwa binadamu, bali inatoka kwa Mungu. Roho ilikuwapo katika mwanzo wa uumbaji, katika mwanzo wa ujumbe wa Yesu na lazima kuongoza kazi ya jamii ya wanafunzi wake.

          Ushahidi wa kwanza wa jamii ya wanafunzi ya Yesu ni umoja uliodhaminiwa na Roho ya Yesu. Kila mtu anaitwa kufanya bora ya mwenyewe ili kuhifadhi umoja huu kama maana ya utambulisho. Katika jamii tumezipokea zawadi kutoka kwa Mungu ili tuwe zawadi sisi kwa sisi, kujiunga nguvu ili kuchangia kwa kuendeleza kujenga kwa mwili mmoja, ambao ni takatifu na hai kwa sababu ni Roho moja inayotenda ndani yake. Kama hii fumbo la uwepo wa Yesu linadhihirishwa, kwa maana hatuwezi kutenganisha mwili kutoka kichwa.

          Yesu ni peke yake na mamlaka iliyopewa moja kwa moja kutoka kwa Baba ili kudhihirisha mpango wake wa wokovu. Alishiriki mamlaka hii na wanafunzi wake ili watumikie watu, wakidhamini maisha mengi kwa wote. Kigezo kupitia maisha mengi haya ni imani, ambayo huja kwetu kupitia hali ya ubatizo. Wanafunzi  walitumwa kama wajumbe wa habari njema kwa wanadamu wote kwa sababu injili haina mpaka. Yesu alikuwa amewaahidia kuandamana safary yao mpaka upeo. Ingawa uwepo wake wa mwili usionekana zaidi, Roho wake inadhaminiwa ili kuwahamasisha katika kazi yao. Uwepo wa Roho ya Yesu daima katika safari ya mitume yake na maishani ya wote waliomwamini umeyafanya maneno yao ufanisi kupitia ishara ningi na matendo mazuri.


         Malaika waliwaambia wanafunzi wa kwanza na wanatuambia siko ya leo: “mbona mmesimama mkitazama mbinguni?” hakika kama Wakristo tunahitaji kurudisha mtazamo wetu kwa Yesu, modeli yetu na kichwa chetu ili tuendeleze kazi yake kwa uaminifu, lakini hatuezi Kubaki komwa kutazama mbinguni. Hali halisi hii inaweza kumaanisha utazamaji na upooza. Bwana anatutaka wenye uangalifu na watendaji. “Wabarikiwa watumishi wale ambao watakuwa wakitumikia Bwana wao atakaporudi”. Maisha ya Kikristu ni tafakari na kitendo, imani na matendo. Ishara za uwepo utenzaji wa Yesu ni mapendo ya wale wanaomwamini na wanayofuata nyayo yake. Kitendo cha Roho Mtakatifu kifanye uzoefu wetu wa Yesu ufanisi katika maisha yetu ya kila siku, kuonyesha ishara za ahadi yetu naye na ujumbe wake.   

Fr. Ndega
Mapitio: Sara

Nenhum comentário: