Mdo. 10: 25-26, 34-35, 44-48; 1Yoh.
4: 7-10; Yo 15: 9-17
Mungu hawabagui watu kwa maana anapenda na katika
upendo hakuna ubaguzi. Mungu anawakaribisha wale wanaomwabudu na wanaishi kwa
udugu. Kuabudu na udugu ni uhusiano na wale ambao wanamwabudu kwa njia hii,
wanaabudu kwa Roho na ukweli. Roho Mtakatifu aliwashukia wale ambao
wakalisikiliza Neno la Mungu kupitia kinywa chake Petro, akidhibitisha kwamba
Mungu anawatendea wote kwa usawa. Mbele ya Mungu hakuna mtu wa heshima zaidi
kuliko mwingine. Mungu hakuzi upendeleo na hakubali umaarufu, bali anatarajia
ahadi kwa njia yake ya kufikiri na kutenda. Maana kwa njia hii ni upendo wake wa
uhuru kwa wote.
Mtakatifu Yohana katika waraka wake anawaalika
watu kupendana kwa sababu upendo kutoka kwa Mungu na wale wanaopenda wanamjua
Mungu. Basi, kupenda ni kujua. Kujua katika Biblia si uzoefu wa akili, lakini
ni uzoefu wa ndani. Mungu anajua kwa sababu anapenda. Kumjua Mungu ni kumpenda,
kufanya naye uzoefu wa ndani. Mungu ni upendo na aliwapenda sana wanadamu
kwamba alimtuma Mwanawe pekee kama maonyesho makuu ya upendo huu ili
kuwafundisha watu jinsi ya kupenda kwa kweli. Kutokana uzoefu huu tulipata
maisha kwa maana upendo tu unayazaa maisha na wale ambao wanakubali kuhusishwa
katika uhusiano wa upendo kati ya Baba na Mwana, wanaishi maisha mapya.
“Mwana
alitupenda kama Baba anavyompenda”. Andiko hili la injili ni sehemu ya ujumbe
wa maagano ya Yesu. Yaliyomo ya ujumbe huu ni urithi wake Mwalimu, aliokuwa na
kama muhimu zaidi ili kuacha kwa wale ambao lazima waendeleze kazi yake.
Umuhimu wa mafundisho ya Yesu ni kupenda. Upendo una chanzo chake katika Mungu
kwa sababu Mungu ni upendo na anampenda Mwana. Uwepo wa Mwana miongoni mwa wanadamu
uliufanya upendo huu kujulikana. Upendo ni ndani ya Mungu; ni maana ya
ushirikiano wake. Wanadamu ni matokeo ya ushirikiano huu na wanaalikwa
kujihusisha katika ushirikiano huu sawa, kukaa katika upendo wa Kristu. Kigezo
ili kukaa katika upendo wake ni kuishi mafundisho yake, ni kwamba, kupendana
kama alivyotupenda na akajitoa kwetu. Yesu halazimishwi kutupenda. Upendo wake
ni maonyesho ya furaha yake yote: furaha ya ushirikiano wake na Baba, furaha ya
kuwa miongoni mwa wanadamu, furaha ya kuwachagua wanadamu kama washirika katika
kazi yake, furaha ya kuutoa uhai kwao. Kuushiriki upendo wake nasi, Yesu
anayajaa maisha yetu kwa furaha kubwa kwa sababu kwa yeye upendo na furaha
inatembea pamoja. Kama hii, mtu tu anayependa kwa kweli ni wenye furaha ya
kweli.
Upendo ni maana ya wokovu wa ulimwengu, kwa
sababu ilikuwa kwa upendo kwamba Mwana wa Mungu aliutoa uhai wake. Kulingana na
Yesu thamani ya urafiki wa kweli hupimwa kwa uwezo wa kuyasalimisha maisha kwa
upendo. Yesu ni rafiki yetu kwa sababu alifanya hivyo vizuri sana. Alituchagua
na alituteua kuenda na kuyazaa matunda, na matunda yanayodumu. Tutakuwa
marafiki zake ikiwa tuna ujasiri wa kupenda kama yeye alivyopenda. Anajitambua
na wale wanaotumwa katika jina lake. Utambulisho huu ni matokeo ya upendo wake
ndani yetu kwa sababu ni sahihi/tabia ya upendo kuumba utambulisho na hisia ya
miliki. Ikiwa tunakaa pamoja naye tutakuwa watu wa ushirika na tutaweza
kusaidia ushirika katika jumuiya zetu. Huu ni ushahidi wetu wa kwanza: Mwone kama wanavyopendana”! Ilikuwa
maoni kuhusu Wakristu wa Kwanza. Upendo wao ulionyeshwa kupitia ridhaa wao kwa
wao, kushiriki pamoja, uvumilivu katika maombi pamoja na unyenyekevu wa moyo.
Je, maisha yako ni maonyesho ya yale wewe huamini? Itawezekanaje jumuiya zetu
kuonyesha hali halisi hii ya Jumuiya za Kwanza?
Badala ya kuuzaa ushirikiano katika
jumuiya, upendo hutufungua kwa watu wengine nje, wanaohitaji kukaribishwa pia. Wale
wanaopenda kweli hawabagui watu na ni makini kwa hali halisi maalum, kujifunza
kutoka kwa Mungu, anayewapenda wote, lakini anapendelea maskini na wale hawana
nguvu. Kama hii pia mama, anawapenda watoto wake wote, lakini ana utunzaji
maalum kwa mtoto mgonjwa. Basi, tufikiri kuhusu upendo wetu kwa wale
wanaohitaji zaidi katika jumuiya.
Fr Ndega
Mapitio: Sara
Nenhum comentário:
Postar um comentário