sexta-feira, 1 de maio de 2015

FURAHA YA WITO


Kutafakari kutoka Matendo 4, 8-12; 1Yohana 3,1-2; Yohana 10,11-18

          Tunaadhimisha Jumapili ya Mchungaji mwema na Jumapili ya miito. Jumapili hii ni mwaliko kumshukuru Mungu kwa zawadi kuu ya wito na kumwomba ili kuendelee kulibariki Kanisa lake kwa kuongezeka kwa miito. Pendekezo hili lilianzishwa na baba mtakatifu Paulo wa VI, katika mwaka elfu moja mia tisa sitini na nne, likihamasisha Kanisa lote kwa ahadi kwa ajili ya wito. Maombi kwa miito ni pia utii kwa mavutio ya Yesu ya kuomba kwa mwenyeji wa mavuno ili atume wafanyakazi kufanyika mavunoni mwake kwa sababu mavuno ni makubwa, lakini wafanyakazi ni wachache (cf. Mt 10, 37-38). Wito ni zawadi, mwito wa Mungu. Huu ni mahitaji ya Kanisa na utambulisho wa ubatizo. Kilimo cha wito huanza katika familia na mtu anayealika hutarajia jibu kwa ukarimu daima kutoka wale ambao wanaalikwa. Tutafakari kuhusu hali halisi hii kupitia utajiri wa masomo ya liturujia hii ili tuuishi wito wetu kwa shauku.  
          Katika Somo la kwanza mitume wanakamatwa na wanaulizwa maswali kuhusu miujiza iliyofanywa kwa mtu aliyepoozwa. Jibu lao kabla ya viongozi vya wayahudi linathibitisha nguvu ya Roho Mtakatifu ikitenda maishani mwao. Kwao kila kipindi kilikuwa nafasi mpya kushuhudia maisha mapya yaliyotolewa na Yesu kwa wote wanaoamini kwake. Kazi ya Yesu ilielekezwa kwa watu wote. Yeye ni ukamilifu wa ufunuo wa Mungu na kupitia yeye tu watu wanaweza kupata wokovu. Kulingana na Mtakatifu Yohana, kupitia kazi ya Yesu watu walikuwa watoto wa Mungu na wanaalikwa kufanya uhusiano wa ndani naye jinsi Mwana alivyofanya na Baba. Maana ya utambulisho huo wa watoto ni upendo wake kwa ubinadamu. Upendo tu unazalisha kifamilia na uhusiano wa ndani. Kupitia upendo tu inawezekana kuishi kama watoto wa Mungu na kuyatumia maisha kwa ajili ya Kristu na ujumbe wake wa wokovu. Mtu anayependa tu huweza kushinda upinzani, ushindani, ukabila na ubaguzi, kutumia nguvu zake kwa muhimu zaidi.
          Katika injili ya Yohana tuna ufunuo wa Yesu kama Mchungaji Mwema. Yeye ni Mchungaji Mwema kwa sababu anawapenda kondoo wake naye yuko tayari kufa kwa ajili yao. Anawatendea na anazitumia nguvu zake kwa ajili ya maisha yao. Uhusiano wa ndani kati ya Mwana na Baba ni rejea kwa uhusiano kati ya Yesu na kondoo wake. Uhuru wa Mwana ni maonyesho ya upendo kwa nguvu aliopokea kutoka kwa Baba. Katika ukarimu na bure ya ishara yake ya kujisalimisha kwake upendo wake unaonyeshwa kwa ajili ya kondoo wake. Kuwa kondoo wa kundi la Mchungaji Mwema Yesu ni kuwa tayari kuisikiliza sauti yake na kuzifuata mafundisho yake kwa sababu yeye hutarajia mema tu ya kundi. Kusudi lake linafikia pia wale ambao hawamjui, lakini siku moja wataisikiliza sauti yake na watatembea katika umoja pamoja naye. Kosa la ahadi ya wale ambao si wachungaji husababisha usambazaji wa kundi. Kundi linahitaji wachungaji wema.
          Katika Yesu, Mchungaji Mwema, Mungu anaonyesha ulinzi wake kwa watu wake kwa njia yenye hamu, kuutoa upande haki kwa maisha yao. Upinzani dhidi ya sauti ya Yesu ni upinzani ili kuifanya mapenzi ya Mungu na kuishi uhusiano wa familia naye. Jibu haki kwa mwito wake siku hizi ni tabia nzuri kuishi Maneno yake, makini sana kwa msukumo zake ili kutenda kwa busara katika hali halisi kandokando yetu. Kutoka kwa mfano wa Mungu sisi hujifunza kuutendea miito, hasa miongoni mwa vijana.

          Kanisa lina mahitaji ya miito mizuri ili kuendelea kwa uaminifu kazi ilipokewa kutoka kwa Yesu, Mchungaji Mwema. Tunaalikwa kutenda kama wanafunzi wa kwanza, ambao waliuchukua wito na kazi iliyowakabidhiwa kwa furaha na shauku. Utambulisho upya uliishi kama wafuasi wa Yesu unatukumbusha kuhusu umuhimu wa wito uliopokewa katika ubatizo wetu kupitia huo tulikuwa makuhani, manabii na wachungaji. Kuishi kwa kweli kwa wito lazima kuwa uigaji wa ishara  na hisia za Mchungaji Mwema katika ulinzi wake kwa kondoo, kuchukua kwa wajibu kazi ya uongozi kwa wema wa watu wa Mungu ambao ni kundi la Yesu.

Fr Ndega
Mapitio: Rose Mong'are

Nenhum comentário: