sexta-feira, 27 de março de 2015

NIKO HAPA ILI KUFANYA MAPENZI YAKO

Kutafakari kutoka Mk 11: 1-10; Isa 50: 4-7; Flp 2: 6-11; Mk14: 1-15: 47

Yesu, anayechukua kuwa Masihi mnyenyekevu na maskini, anatangazwa kama mfalme na mshindi katika kuingia kwake Yerusalemu. Anakubali ishara hii ya umati wa watu hata kujua kwamba ataachwa peke yake kwa kunywa kikombe cha mateso na huzuni ili kufanya mapenzi ya Mungu. Yeye ni mtumishi wa Bwana kwa ubora, ambaye hata anahisi kuachwa, alibaki mwaminifu kwa mpango wa Mungu, akiisalimisha maisha yake kwa imani jumla mikononi mwake.
Kulingana na somo la kwanza, mtumishi wa Bwana ni mwaminifu kwa kazi ambayo Bwana alimkabidhi. Mtumishi anaishi wito wake kwa shauku, kuchukua matokeo ya uamuzi wake. Yeye lazima kuvumilia matusi, mateso, mshangao na kukataliwa, lakini dhamana ya mafanikio katika kazi yake ni uwepo wa Bwana daima na mwaminifu. Katika kilimo ya utambulisho wake wa mtumishi, yeye ni wazi kabisa kwa mapenzi ya Mungu ambaye anamwongea kila siku ili, kwa njia ya uzoefu wa Neno hilo, aweze kutenda kama mwanafunzi. Ni hayo ambayo Mtakatifu Paulo anaomba kwa jumuiya ya Wafilipi, kuonyesha mfano wa Kristo aliyechagua kuwa mtumishi, akikubali fedheha na mateso ili kufanya mapenzi ya Mungu. Hii ilikuwa njia ya utukufu wa Mwana wa Mungu na pendekezo ya kiradikali kwa wale ambao wanataka kumfuata kwa uaminifu.
Andiko la mateso kulingana na Marko ni mwanzo simulizi na linaonyesha maelezo muhimu kwa safari yetu kama wafuasi wa Yesu. Tuanze kuhusu uwepo wa mwanamke katika mwanzo na mwisho wa andiko hili. Wakati wa maisha yake ya umma, Yesu aliruhusu uwepo wa wanawake daima na kikamilifu katika kazi yake. Kupitia ishara yake ya mwaliko na kuthamini ya uwepo wao katika kazi yake, alijipatia heshima yao na anawazawadisha kama rejea katika mwendo wa uinjilishaji. Katika mwanzo wa andiko hili, tunaalikwa kutafakari kuhusu ishara ya kushangaza ya upendo na heshima ya mwanamke kwa Yesu, akitumia marashi ghali, kubadilisha mawazo na hali nyumbani pale. Kwa ishara hii, anafundisha kwamba kumfuata Yesu ni kutumia bora ya mwenyewe kwa upendo. Katika mwisho wa simulizi hii wanawake hawana hofu ya matokeo ya utambulisho wao na Mwalimu. Ushahidi wao ni mwaliko kwa kuendeleza uamuzi wa kumfuata Yesu hadi mwisho.
Yesu alisalitiwa, akaachwa, akapigwa, akaaibishwa, akatukanwa na akabaki kimya. Kupitia ukimya huu anaonyesha nguvu yake. Anaamua kusema tu ili kuthibitisha utambulisho wake wa Masihi na uhusiano ndani na Mungu Baba yake. Kupitia uhusiano huu ndani, ulioonyeshwa kwa maombi yake katika Bustani Gethsemane, anajihamasisha kukubaliana na msalaba na kufanya mapenzi ya Mungu, kujisalimisha mikononi mwake kwa tabia ya imani na upendo jumla. Kifo chake hakikutakwa kwa Baba yake, lakini ishara yake ya upendo hadi matokeo ya mwisho ilikubaliwa na ikajibiwa kupitia ufufuo mtukufu kutoka kwa wafu.
Kabla ya ukatili ya wale ambao walimsulubisha, Yesu hakuitikia, akijidhihirisha mfano wa mtu asiyekuwa na fujo, akitangaza kwamba wafuasi wake hawangepigana kwa sababu ufalme wake si wa dunia hii. Kama hii analaumu kila aina ya ukatili. Kama chembe ya ngano ambayo inakufa ili kuzaa matunda mengi, Yesu alikubali kuteseka na kufa kwa utambulisho na mshikamano wake na wanaosumbuka na waliosulubiwa wa ulimwengu huu ili kuwapa maisha mapya. Hivyo, ishara yake inaendeleza kuhamasisha wanaume na wanawake kujikataa, kuichukua misalaba yao na kuzifuata nyayo zake, kuwa wapatikana kwa kila kitu kwa ajili ya Ufalme wa Mungu. Kwa maadhimisho haya ya Ekaristi tunaalikwa kuanza Wiki hii takatifu kuhamasishwa sana kumtambua na kumtangaza Yesu kama Mwokozi wetu, kumwandama katika uaminifu wake kwa mpango wa Mungu na kushinda majaribu ya usaliti na kanusho kuwepo katika safari yetu daima. Mfano wake wa unyenyekevu, utupu na kujisalimisha mikononi mwa Mungu kutuhamasishe kuisalimisha maisha kabisa kwa mema ya wengine.

Fr. Ndega
Mapitio: Rose Mong'are

Nenhum comentário: