terça-feira, 3 de março de 2015

MUHIMU ZAIDI YA SHERIA NI KUPENDANA


Utu uili muhimu wa biblia unatusaidia kuelewa vizuri ujumbe wa Kristo kama kuhani wa agano jipya na milele, kama vile Melkizedeki na Ibrahimu. Kuhusu Melkizedeki, alikuwa mfalme na kuhani, mfalme wa haki na amani. Hakuna mtu anaijua asili yake, lakini wote hukubali ukuhani wake. Kwa uhakika zaidi tunaalikwa kukubali ukuhani wa Kristo ambao una asili ya Mungu. Ukuhani wa Kristo ni rejeo kwa huduma yetu, kwa sababu kwa njia ya ubatizo wetu tulifungwa kwake kama sehemu za Mwili wake na tunaitwa kushiriki katika ukuhani wa pamoja ili kuwatumikia Watu wa Mungu.

Ibrahimu, katika uzoefu wake wa kujisalimisha anatumotisha kushukuru Mungu. Tabia ya kujisalimisha ni kurudisha kwa Bwana ambayo ni miliki yake. Kulingana na andiko hili, kuhani mkuu Melkizedeki anakutana na Ibrahimu na anambariki. Hivyo, baraka inatokea kabla ya sadaka ya Ibrahimu. Kama hii ni hatua ya neema ya Mungu katika maisha yetu; hutokea hata bila ufahamu kutoka kwetu na kabla ishara yoyote ya binadamu. Kama tunamtolea kitu hakiongezi chochote kwa Mungu, lakini kinaonyesha kutambua kwetu na shukrani yetu kabla ya zawadi nyingi ambazo tumepokea. Sadaka na kujisalimisha ni sehemu ya maisha yetu na maisha yetu ni kuwepo kwa sadaka ambayo tunatoa kwa Bwana. Sadaka yote hupata maana yake ya kweli katika sadaka ya Kristo, ambaye anajitoa kwa Mungu kwa wokovu wa wote.

Yesu ni Kuhani Mkuu ambaye anahisi huruma kabla ya hali halisi ya mateso ya watu. Yeye anahisi pia hasira kwa sababu ya kutojali na ukosefu wa haki kuhusu hali halisi hiyo. Yeye anapinga sheria ambayo iliishiwa kwa njia rasmi, kuzuia kuona mahitaji karibu. Kwake muhimu zaidi si sheria yenyewe, lakini roho ambayo ilimotisha sheria na tabia iliyochukuliwa kabla yake. Sheria inapoteza maana yake ya kweli wakati inatumika tu kuonea, kukuza maslahi ya binafsi. Kwa Yesu, sheria ya kweli inaikuza maisha na inawaongoza watu kufanya mambo mema kwa wengine. Wakati mwingine yeye anasema kwamba muhimu zaidi ya sheria ni kupendana. Yeyote amfuataye Yesu hafuati sheria au mafundisho, lakini anamfuata Mtu Yesu. Mtu Huyo hutufundisha kutumia kila sheria kama chombo cha udugu, ambacho upendo kwa Mungu na upendo kwa jirani unashuhudiwa kwa nguvu.

Fr. Ndega

Mapitio: Rose Mong’are

Nenhum comentário: