quarta-feira, 25 de março de 2015

KUFA ILI KUZAA MATUNDA MENGI

 Kutafakari kutoka Yeremia 31:31-34; Waebrania 5:7-9; Yohana 12:20-23

Liturujia hii inatuandaa kuingia na juhudi katika maadhimisho ya fumbo la “Saa” ya Yesu, ambayo inajumuisha mateso, kifo na ufufuko wake, kupitia hiyo atatukuza Baba na atamaliza kazi yake. Kazi ya Mwana ni Agano Jipya lililoandikwa moyoni mwetu kupitia ubatizo wetu. Katika upya wa ahadi yetu kwa Agano hili tukaribishe nguvu ya chembe ya ngano ambayo inakufa ili nyingine iweze kuishi.   

Somo la kwanza linaongea kuhusu Agano jipya, ambalo Mungu ataanzisha na Watu wake. Itakuwa tofauti sana ya Agano la kwanza lililoandikwa katika mawe na likakubali kwa jibu la juu juu. Tabia kuu ya agano hili jipya ni uhusiano udani kati ya Mungu na watu wanaoalikwa kuendeleza Neno la Mungu lililoandikwa moyoni mwao. Basi, Mungu anaongea na watu wake kutoka moyo kwa moyo ili wahisi kuhimizwa na kubadilishwa kwa upendo wa huruma. Bila msamaha hakuna maridhiano, hakuna upya pia. Uaminifu na hisia ya miliki kwa Mungu itakuwa utambulisho upya wa watu hawa: “Nitakuwa Mungu wao na watakuwa watu wangu”, asema Bwana. Kulingana na mwandishi wa Waraka wa Waebrania, kupitia utii kwa mapenzi ya Mungu, Yesu alifanya Agano hili Jipya na ufafanuzi, kukubali kuteseka na kutoa maana mpya kwa mateso ya binadamu. Kupitia uzoefu huu, alijifunza maana ya kitambulisho kwake na ubinadamu wenye mateso, kuongoza njia ya kuijisalimisha maisha kwa upendo ili wote wawe na maisha mapya na bora.

Injili inaongea kuhusu mkutano ambao ulianza kwa ombi: “tunataka kumwona Yesu”. Hali halisi ilikuwa sherehe ya Pasaka. Wagiriki pamoja na watu wengine walikuja Yerusalemu kushiriki katika tukio kuu la utambulisho wa Wayahudi. Wanamfikia Yesu kupitia wawili kati ya wanafunzi wake ambao walikuwa na majina ya kigiriki, ni kwamba, Andrea na Filipo. Tamani ya Wagiriki kumwona Yesu inaendelea zaidi ya udadisi rahisi wa kutaka kuona mtu maarufu. Ombi lao ni kujua bora kuhusu utambulisho wa Yesu ili kuitumia maisha yao na yeye kwa yeye kama ilitokea na wanafunzi wa Yohana Mbatizaji wanaotaka kupaona mahali Yesu alipoishi na akawaambia, “njoni nanyi mtaona”. Ni mwaliko kufanya uzoefu. Hakuna njia nyingine kumjua Yesu. Katika injili siku ya leo Yesu anajionyesha kuongea kuhusu “Saa yake” kupitia mfano wa Chembe ya ngano. Saa hii inajumuisha mateso, kifo na ufufuko wake. Kama hii, mkutano na Yesu ya kweli ni kulishiriki fumbo la kujisalimisha kwake kwa upendo. Katika njia hii, mtu anaweza kuona maana ya kweli ya maisha na sababu ya kweli ya utafutaji kwa Mungu.  


Kumwona Yesu ni tamani yenye nguvu ya moyo wa binadamu, kwa sababu Yesu anadhihirisha Baba, yeye ni ishara hai ya Mungu. Yeye ni njia ambayo inawaongoza watu kwa Baba; yeye ni ukweli wa Mungu kuhusu binadamu na ukweli wa binadamu kwa Mungu; yeye ni uhai, ambao ni zawadi kuu ya Mungu, iliyotimizwa na Mwana wake. Maisha ya Yesu nzima ilikuwa ya utupu kabisa (Kenosis, neno la kigiriki), akichukua njia ya mtumishi, kwa sababu alikuja kutumikia si kutumikiwa. Kama hii, kila mtu anayetaka kumfuata lazima kufanya vivyo hivyo. Mafundisho ya Yesu mazima ni mwaliko kufikiri na kutenda tofauti kuhusu mawazo yaliyopo. Kulingana na Yesu ni lazima kuwa mtu wa mwisho ili kuwa mtu wa kwanza; kuitoa maisha ili kuipokea; kufa ili kuishi na kuwafanya wengine kuishi bora. Kama sisi ni watumishi kwa kazi hiyo ni kwa sababu tumepata imani ya Mwalimu Yesu anayetangaza, “ninawajua wale ambao nimewachagua”. Yesu anatujua kwa ndani na anatuita kumfuata, kuitoa maisha kama alivyotutolea. Hivyo, mtu ambaye anajisalimisha kwa Mungu ili kutumikia ndugu zake anajiunga na katika ushirikiano sawa ambao Mwana huanzisha na Baba. Maadhimisho ya Ekaristi yatusaidie katika ahadi yetu ya ubatizo, kutuhamasisha kutumikia katika jumuiya kwa furaha na ukarimu.   

Fr. Ndega
Mapitio: Rose Mong'are

Nenhum comentário: