Kutafakari toka Kutoka 22, 21-27;
1Thes 1, 5-10; Mathayo 22, 34-40
Kulingana
na Maandiko, Mungu ana uhusiano maalum na watu wa Israeli. Anaanzisha agano na
watu hao kuwapa miongozo kadhaa ili watende vyeme, kuhifadhi maisha yao. Ni
katika hali hiyo kwamba Amri ziliibuka/patikana. Kuishi katika Amri kumekuwa umuhimu
zaidi katika safari ya Watu wa Israeli kwa ambao Sheria ni Neno la Mungu na
Neno la Mungu ni Sheria. Wakati wao husema “Sheria ya Mungu ni kamilifu, faraja
kwa roho”, wanamaanisha kwa Neno la Mungu. Kuna uwiano wa kina kati ya Sheria
na Neno, kwa sababu amri za Sheria zinaonyesha huduma ya upendo wa Mungu anayeongea
kuonyesha njia za ukombozi na kisha zinadhihirisha pia utambulisho wa kweli wa
watu ambao wanatii, kukuza hisia za miliki ya Mungu wao. Utiivu kwa amri ni
chanzo cha baraka kinachoelekeza kwa uhai, wakati uasi kwa hizo unaelekeza kwa
kifu.
Katiku
Sheria kuu, Wayahudi wameweka sheria nyingi kwamba hatimaye zilibadilisha lengo
kutoka iliyokuwa muhimu zaidi. Amri kumi za awali zilikuwa mia sita kumi na
tatu. Watu maskini walichukuliwa wenye dhambi kwa sababu hawakuweza kukariri
amri hizi zote na kwa hiyo, hawakuziweka vitendoni. Hata hivyo, sehemu hii ya
idadi ya watu walijua na walikuza umuhimu zaidi wa Sheria. Hilo ni jibu la Yesu
anaposema: “upende Bwana Mungu wako na moyo wako wote, na akili yako yote, na
nguvu zako zote” (Dt 6: 4-5) “na jirani wako kama unavyojipenda mwenyewe” (Lev.
19: 18).
Kumpenda
Mungu ni amri ya kwanza ya zote, lakini Yesu aliiunganisha na upendo kwa
jirani, kuonyesha kwamba haiwezekani kumpenda Mundo bila kumpenda jirani. Yakobo
katika waraka wake anamfikiria kama mtu mwongo anayesema kwamba anampenda Mungu
na hampendi jirani. Kutoka amri ya kumpenda Mungu inabubujika kumpenda jirani
kama matokeo. Chanzo ni Mungu daima kwa sababu alikuwa aliyetupenda wa kwanza.
Ni kutokana na upendo kwamba Mungu anao kwetu – kwa njia ya ukarimu na bure –
ambayo inawezekana kuwapenda wengine na uhalisi. “hiyo ni changamoto kwa
tamaduni zote ikiwa ni pamoja na hizo
katika Afrika, ambapo uaminifu kwa familia na mila unakuzwa mara nyingi kama
amri ya kwanza.”
Yesu aliyefanika mwili, ni upendo wa huruma wa Mungu na
maisha yake yakasalimika kwa wote yanaonyesha kwamba kupitia upendo tu binadamu
anaweza fikia mafanikio yake binafsi. Bila shaka, kwamba kuwa ndani ya dini na
ushiriki misani ni ishara ya upendo kwa Mungu kama kipaumbele katika maisha
yetu. Hata hivyo, katika mwisho wa maisha yetu ombi letu halitakuwa “Je, ulikuwa
wa dini gani?” au “Je, mara ngapi ulienda misani?”, lakini swali kamili litakuwa,
“ulikuwaje upendo wako kwa wengine?” kiwango cha upendo wetu kwa Mungu kinaonyeshwa
katika njia kama tunavyowapenda wengine. Anapenda kweli mtu ambaye anatamani tu
wema kwa mtu mpendwa, hata kama hastahili. Hivi ndivyo Mungu anavyotupenda, kwa
ukarimu na bure. Uzoefu huu lazima utuongoze kufanya anavyofanya.
Muhimu
zaidi kwa Yesu ni kumpenda Mungu, kupenda pia jirani. ufundishaji wake wa ajabu
yako ulifanya amri hizo mbili hata kupatikana zaidi, akitoa ushauri kwamba inatosha
tupendana kama alivyotupenda. kama vile Mungu ametupenda katika Kristu, sisi
lazima tupende kutoka kwa Kristu. Yeyote anayependa katika njia hiyo amefahamu umuhimu
zaidi wa Sheria na maisha, kwa sababu yeyote anayefuata Yesu hafuati sheria au mafundisho,
lakini anafuata Mtu.
Kwa hiyo, kigezo tu Wakristu wanacho kushuhudia upendo wa
Mungu duniani ni kupenda wengine kama ndugu. Tunampenda Mungu wakati tunampa mahali pa kwanza katika maisha yetu, kutafuta
kwanza ufalme wake na haki yake, wakati sisi ni waminifu katika sala zetu kila
siku, tunaposhiriki kwa makini katika sherehe ya sakramenti.
Sisi huonyesha upendo kwa jirani wakati tunaweza kuhisi huruma mbele ya hali
halisi ya huzuni na mateso ya wengine na tunapatikana kuwasaidia katika
mahitaji yao. Katika maana hii, ilisemwa kuhusu Jimuiya za kwanza: “Oneni wanavyopendana”.
Hata hivyo, iliwezekana tu kwa sababu walibaki pamoja katika upendo wa Mtu aliyewaita.
Hitaji hilo lingalipo katika siku zetu na linaaminisha nguvu za uhai ya kazi
yetu kama Wakristu.
Fr. Ndega
Mapitio: Mwalimu Patrick
Nenhum comentário:
Postar um comentário