Tafakari kutoka Ezekieli 14: 11-12.15-17; 1Kor 15: 20-26.28; Mt 25: 31-46
Maandiko haya inaongea kwamba Mungu ni Mfalme-mchungaji
ambaye anawahifadhi na anajitambulisha na hao ambao
ni masikini. Upendo na huruma kwa wengine
ni kigezo ili kuingia ufalme wake.
Kwa maana hii, tukaribishe ujumbe wa Liturujia hii
kwa shukrani na uwazi,
kutafakari kuhusu fumbu la Ufalme wa Mungu
na utendaji wake kupitia
kazi ya Kristu.
Nabii Ezekieli
anashutumu kutowajibika ya viongozi
wa Watu wa Israeli ambayo ilisababisha
uhamisho, kipindi cha huzuni na mateso kwa
watu. Lakini katika ujumbe huu, nabii anatangaza
pia kwamba Mungu ni busara na makini sana kwa watu wake. Anachukua ubinafsi hali ya watu wake kama mchungaji
wa kweli, kuongoza wao kwa hali halisi mpya. Unabii huu hufanya mafanikio yake
katika Yesu Kristu, Mchungaji
Mwema. Kulingana na Mtakatifu
Paulo, Yesu anashinda nguvu zote
duniani, kupitia kifo chake na ufufuo
wake, kuokoa ubinadamu na kuanzisha
Ufalme wa Mungu Baba yake. Wanadamu
wote wanaoalikwa ni kwa ufalme
huu. Muungano na Kristu ni
usemi wa ushiriki huu na unaongoza kwa uzima wa milele. Hivyo,
kuwa miliki ya Kristu ni kuwa wa Ufalme
wa Mungu, dhamana ya uzima wa milele.
Andiko hili ya
Injili linajulikana kama “Hukumu ya mwisho” na wengi wetu hufikiri kwamba Yesu ni “hakimu” anayehukumu vitendo vya binadamu, kuwatuza wengi na kuwaadhibu wengine.
Lakini tulijifunza kupitia maneno yake
yenyewe kwamba “Mungu hakumtuma Mwana
ulimwenguni ili kuwa hakimu wake,
lakini kwa kuwa mkombozi wake” (Yohane 3, 17).
Hivyo, lengo lake si kuhukumu bali kuokoa. Hukumu
huanzishwa kwa vitendo vya watu. Kulingana na andiko
hili, Yesu ni Mfalme-mchungaji. Mfalme huyo
ana nia ya kukusanya watu wote karibu na yeye mwenyewe na huduma maalum kwa watu hao masikini. Anajitambulisha nao na anawaanzisha
kama rejea kuokoa
wengine. Anawahamasisha watu wengine
kufanya matendo mema kwao na
anawapa zawadi kwa hao ambao hukumbatia
sababu hiyo. Hivyo, huduma ya upendo tunayo kwa masikini ni kigezo
kuingia Ufalme.
Wainjilisti wanaonyesha
kwamba Yesu alikataa cheo cha
mfalme katika wakati wa utukufu, na akakubali katika wakati
wa ushinde. Upinzani wake kwa cheo hiki
ulikuwa kwa sababu mawazo ya kisiasa ya watu kuhusu suala hili. Lakini
yeye mwenyewe anatumia cheo
cha mfalme katika andiko hili ili
kutusaidia kuelewa maana haki ya Ufalme na lengo lake kama Mfalme. Ufalme
wake si kutoka ulimwengu huu na
hauwezi kuonekana (ni huko au ni hapa). Yesu anaufafanua
kamwe Ufalme wa Mungu, lakini alisema
kwamba huo ni tayari sasa kati
yetu na tunaweza kuhisi tukio lake. Katika
mafanikio yake ya kidunia, hali
halisi ya Ufalme wa Mungu si mbali sana toka hali halisi ya binadamu. inaishiwa kupitia thamani
nzuri za tamaduni zetu na unazishinda.
Kiini ya ujumbe wa Yesu
ni tangazo la Ufalme wa Mungu,
kwa sababu hatangazi mwenyewe lakini anatangaza Ufalme. Katika Yesu, Ufalme unakuwa
ukweli halisi. Mjadala wa uzinduzi kuhusu tukio hili maalum unafanyika kwa wakataliwa
na jamii, hao ambao ni maskini.
Katika nyuso zao, Yesu alitufundisha kutambua uso
wake wenyewe. Ufalme ni wao na wao ni
wamiliki wa Ufalme. Katika
matendo yake mema na watu hao, Yesu anaushahidi kwamba wakati mpya
umekwishaanza, kubadilisha hali nyingi
katika dunia, kama vile: wagonjwa wanapona, bubu
wanaongea, vipofu wanaona, maskini
wanahubiriwa Habari njema na watu wenye dhambi
wamepata msamaha wa Mungu . Upendo na huruma
wa Yesu kwao
ni mwanzo wa wakati huo mpya. Ni lazima kufikia
mafanikio yake katika Ufalme ufafanuzi wakati upendo
kwa Mungu na kwa jirani wataishiwa kwa ukamilifu wake.
Tunaalikwa kutambua
katika ishara za ukombozi za Kristu hatua ya wokovu wa Mungu na kufuata nyayo
zake kwa uaminifu, kutangaza habari
njema ya Ufalme. Kwetu, kutafuta Ufalme huo ni lazima kipaumbele, kwa sababu katika kutafuta hii
tunakuta maana ya maisha na kazi zetu.
Yesu ametukabidhi Ufalme wake na tumekabidhi maisha yetu kwake. Ni
kukabidhiana. Kumfuata Yesu ni kukubali ufalme; upinzani
dhidi ya Yesu ni upinzani kwa
utendaji wa Ufalme. Wakati sisi hupatikana kwa mipango ya Yesu, yeye hututumia kama wapatanishi wake ili kuendelea kutangaza kiinua
mgongo cha Ufalme wake, kuwakaribisha
watu wengine kujiunga na nguvu pamoja
naye katika uanafunzi wakarimu na halisi milele. Ingawa yeye huweza kufanya
kila kitu peke yake, alitaka yetu kwa sababu anajua kwamba tunamhitaji sana, kwa hivyo anasema,
"Bila mimi hamwezi kufanya chochote" (Yohane 15: 5).
Fr. Ndega
Mapitio: Rose Mong'are
Nenhum comentário:
Postar um comentário