Kutafakari kutoka Ez 47,1-2.8-9.12; 1Cor 3,9c-11.16-17; John
2, 13-22
Leo ni Sikukuu ya Kanisa. Hivyo,
ni sikukuu kwa sisi sote ambao tuliitwa kuwa wa Hekalu
hilo takatifu na hai la Mungu. Ni
mwaliko kutafakari kuhusu maana ya umoja
wa Kanisa na lengo lake katika dunia.
Kwa hivyo Maandiko ya Jumapili hii
ni kuhusu maana ya Hekalu katika maisha ya
Watu wa Mungu.
Katika maono ya nabii Ezekiel,
Hekalu ni mahali ambapo maji hai yanabubujika
kwa wingi, yakizaa maisha ambapo
hayo hupita. Maji hayo hai ni neema ya Mungu
inayofikia kila mtu, ikileta maisha na wokovu. Pendekezo
hapa ni maisha mapya ambapo kulikuwa kifo tu
na roho mpya ili kubadilisha
fikira na miundo ya kale. Utaratibu upya huu unajumuisha viumbe vyote vilivyowasilishwa kwa hatua
ya binadamu. Picha hii iliyotumiwa na Ezekiel ni
mwaliko kutafakari kuhusu zawadi za wokovu zilizokabidhiwa
Kanisa ili kufanya rahisi zaidi upatikanaji wa
binadamu kwa wokovu
uliotolewa kwa njia ya Yesu Kristu.
Katika injili, Yesu anaonyesha
huduma yake kwa nyumba ya Mungu na hasira yake kuhusu tabia ya kutoheshimu Hekalu.
Watu walikuwa wamebadilisha mahali pa sala kuwa sehemu ya biashara. Yesu
alitumia hali halisi hii ili kuwafundisha kuhusu utambulisho wake wa Hekalu la Mungu kwa ubora.
Katika Yesu Kristu mwanadamu anaweza kufanya mkutano wa kweli na Mungu. Elezo lake linafanya kutafakari bora
kuhusu lengo la Hekalu na tabia sahihi kwa uhusiano
na hilo. Ni mwaliko pia kwa wote kuwa mahekalu, kuabudu
Baba kwa Roho
na ukweli. Hao wanaokuwa wanafunzi wa Kristu hutengeneza naye Hekalu mpya
ambapo Mungu huishi.
Kanisa lipo kwa wokovu wa binadamu. Hili ni lengo lake.
Linamtangaza Yesu Kristu, wokovu wa Mungu kwa
wote. Ujumbe wa Kanisa ni mwaliko kwa kubadilika kwa Mungu, ni kwamba, kuishi
uhusiano wa ndani na Yeye, chanzo cha uhai. Kuishi mbali naye kuna maana ya kifo. Kanisa ni Hekalu
hai la Bwana ambalo huzaa maisha
ambapo yeye yupo. Kila jengo la Kanisa linavutia makini yetu hapana tu kwa uzuri wake, lakini juu ya yote, kwa sababu ni mahali pa sala na upendo wa kindugu panapomtangaza
wepo wa Mungu duniani. Kuna upuzi
kuelekeza sana makini juu ya kuta za
hekalu na kusahau maisha ya watu ambayo yanaonyesha nguvu za uhai wa Kanisa la
kweli ambalo ni Mwili wa Kristu. Kanisa
lingekuwa dhaifu sana kama wasiwasi wake ulikuwa
tu na hekalu la mawe
bila makini kwa hekalu
ambalo ni chanzo cha maisha na
mwanga kwa wote.
Kwa njia ya
ubatizo tuliitwa kwa kuzaliwa
upya. Kuzaliwa upya kiroho huko kumekuja
kwetu kupitia Kanisa. Kuzaliwa upya
huko kunatuongoza kwa uzima wa milele kwa
sababu hutubadilisha kwa hekalu
hai la Mungu. Katika maneno
mengine, Mungu kwa upendo mkuu na wema wake
ametufanya katika makao yake pekee.
Utambulisho wetu ni kuwa kanisa ambalo ni jamii ya imani na upendo, kwa njia ya ushirika na ushirikiano. Kama mawe hai tunaalikwa kuchangia kwa kuendeleza kujenga kanisa
kupitia ushuhuda wetu
wa maisha. utunzi kuhusu uzuri wa nje wa mwili ni nzuri, lakini
hauwezi kutuzuia kuchukua huduma
maalum ya hekalu hai la Mungu ndani yetu. Hiyo
ni kauli ya Mtakatifu Paulo katika waraka wake
kwa Wakorintho: “Ninyi ni hekalu
la Mungu na Roho wake anakaa ndani yenu”. Kwa kweli kama jumuiya ya Kikristu tunamotisha na Roho wa Mungu ili kuzaa matunda mazuri,
kuwa ishara ya upendo wa Mungu na
chombo cha wokovu wake. Imani iliyoishi katika jamii
kutufanya mashahidi wa ukweli na uhuru ili
watu wanaweza kuishi na shauku matumaini ya hali halisi mpya.
Fr. Ndega
Mapitio: Mwalimu Patrick
Mapitio: Mwalimu Patrick
Nenhum comentário:
Postar um comentário