sábado, 11 de agosto de 2018

TUNAMWENDEA KRISTO KWA SABABU TUNAVUTWA NA BABA



Kutafakari kuhusu Yoh 6, 44-51


       Ili tupate uelewa mzuri kuhusu andiko hili hatuwezi kusahau yale aliyosema Mtakatifu Geronimo: “Yule anayepuuza Maandiko Matakatifu anayepuuza nguvu na hekima ya Mungu. Kuyatojua Maandiko ni kumtojua Kristo.” Katika kifungu kingine anasema kwamba “Neno la Mungu ni mkate wa Kristo, nyama ya Kondoo, mwili wake na damu yake”. Hivyo, tunafahamu kwamba tunaweza kutumia andiko la leo kwa ajili ya Ekaristia lakini tena kwa ajili ya Neno la Mungu lililo mkate ulioshuka mbinguni. Tuko na uhusiano wa ndani kati ya Ekaristi na Neno: tunala na kushiba neno lilifanyika mwili (Yoh 1, 14).”

      Yesu anaongea na wenzake wa Galilaya katika sinagogi ya Kafarnao naye ndiye maana ya kashfa kama ilivyotokea katika Nazareth. Yeye ndiye Mungu wa kawaida anayehusika kwa hali ya kibinadamu hata kusababisha kashfa. “Wayahudi hawakiri mtu awe na uwezo hali ya kimungu (kushuka kutoka mbinguni) na asili ya kibinadamu ya Yesu ambayo wote walijulikana, haijumuishi asili ya kimungu yoyote. Labda, Yesu alikosa akikubali kuishi kama watu wa kawaida?

       Wakati yeye anasema: “mimi ndiye mkate ulioshuka kutoka mbinguni”, anaongelea hali yake kama Neno milele la Mungu ambalo lilifanyika mwili katika hali ya kibinadamu likiipandishia hali hii na kuizalisha hali mpya. “matumizi ya mkate ama chakula kama mifano yajulikana katika Maandiko. Manabii watumia kwa ajili ya Neno la Mungu (Am 8, 11; Is 55, 1-11). Maandiko ya Hekima yatumia kwa kuongelea Hekima ama akili (Meth 9, 1-6; Ben Sir 15, 3; 24, 18.21-22).” Yesu ndiye Hekima ya Mungu ambaye ufunuo wa biblia unaongea kama kuwa ni mtu (Yoh 1, 1s).

     Yeye anajifunua kwa wasikilizaji wake kama chakula kilichoshuka kutoka mbinguni si kwa binadamu tu bali kwa ajili ya uzima wa ulimwengu mzima. Tukumbuke maneno haya, yaani, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwana wake wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele (Jo 3, 16)”. Mwana anajitoa kama chakula kinachodumu hadi uzima wa milele kwa sababu ya mapenzi ya Baba aliye uhai na kusababisha uzima ndani ya kila mtu anayempokea Mwanawe. Maneno haya ni umuhimu katika mafundisho ya Yesu kama mwokozi na mkombozi wa dunia. Anatuokoa kwa kujitolea mwenyewe.

     Tafakari yetu ni pia kuhusu Ekaristi takatifu iliyo uwepo hai na kweli wa Yesu miongoni mwetu. Yeye anasema kwamba twamwendea yeye kwa sababu tunavutwa na Baba na tena kumwamini yeye ni kipimo ili tuwe na uzima wa milele ulio uzoefu wa kufufuka katika siku ya mwisho. Uzoefu huu ni ukamilifu wa ushirika wetu na Mungu, aliye chemchemi ya uhai na furaha milele. Fumbo la kazi ya Kristo linasisitiza kwamba yeye alikufa kwa sababu hakutaka kuwaacha wafuasi wake na kufufuka ili abaki pamoja nasi, kutulisha kwa mwili wake na  kutuonyesha njia ya uzima wa milele. Kwa maneno mengine anataka tuishi kutokana na mfano wake.

    Yesu anaongea kuhusu uzima bila mwisho na kwamba uko kwa watu wote. Huu ni maonyesho ya kujisalimisha kwake kwa hiari, kuendeleza uwepo wake miongoni mwa wanadamu na kufundisha njia ya utimizaji kabisa. Hiyo ni Ekaristi kama zawadi kubwa ya Mungu ambaye hataki kubaki mbali na binadamu. Ekaristi ni hazina ya kanisa, uwepo maalum ya mume wake na alama ya uzoefu wake wa kiroho kama mke wa mume aliye Kristu. Linaishi kwa sababu ya Kristu. Vivyo hivyo ni kwa wote ambao wanashiriki mkate mmoja na kikombe kimoja. Kupitia Ekaristi Yesu anatuingiza na kutuchukua kwake ili tuishi naye. Yeye anakaa ndani yetu nasi ndani yake. Anatuunganisha naye, kutuhusisha katika ushirika sawa kati yake na Baba. Bila shaka kwamba matokeo ni pia undugu wenye nguvu na mwafaka miongoni mwetu. Yesu anashughulika na hali ya wanadamu wasio na chakula na kutualika kushiriki katika hisia zake tunapopokea Ekaristi.

Fr Ndega



Nenhum comentário: