sábado, 3 de março de 2018

UHUSIANO MPYA KATI YA MUNGU NA WATU WAKE



Kutafakari kuhusu Kut 20: 1-17; 1Wak 1, 22-25; Yoh 2, 13-25

Maandiko Matakatifu yaongea kuhusu uhusiano maalum kati ya Mungu na watu wa Israeli. Yeye alianzisha agano na watu hawa akiwapa miongozo ili watembee salama na kufanya mapenzi ya Mungu. Katika hali halisi hii, amri kumi zilizaliwa. Kuishi Amri ilikuwa jambo muhimu katika safari ya Watu wa Israeli ambao wanafikiria Sheria kama Neno la Mungu na Neno la Mungu kama Sheria. Basi kuna uhusiano wa ndani kati ya Sheria na Neno la Mungu. Kupitia Sheria au Amri, Mungu anaonyesha utunzaji kwa watu wake na kuonyesha njia ya ukombozi.

Wakati watu wanafuata miongozo hii wanaweza kuona Baraka za Mungu, lakini wakati wanachagua ukosefu wa uaminifu matokeo ni kifo. Kidogo kidogo muhimu ya Sheria ilikuwa ikisahauliwa na kubadilishwa kuwa ni mawazo ya kibinadamu. Hali hii ilizaa aina ya dini ambayo haikuzaa matunda tena.  Ilipaswa kuchukua tena maana ya kweli ya Sheria kwa ajili ya kuanzisha tena uhusiano mpya na Mungu kupitia Agano mpya na milele. Iliwezekana kupitia Kristo, aliyejulishwa na Mtakatifu Paulo kama nguvu na hekima ya Mungu.

Katika injili tuko na tukio la kutakasa kwa hekalu. Katika wainjilisti wengine tukio hili lilijulishwa katika sehemu ya mwisho ya injili yao wakati alipoingia Yerusalemu ili kuteseka mateso yake. Kwa upande wa mwinjilisti Yohana ni tofauti, yaani anaweka tukio hili mwanzoni mwa injili yake. Kisha, Yesu alienda mpaka Yerusalemu na kuona huko hekaluni watu wakiuza ng’ombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi. Alihisi hasira fulani kwa sababu ya hali ile na mara akatengeneza mjeledi wa kamba na kuwafukuza wote nje ya hekalu. Katika mwanzo wa tukio hili hakuna mtu ambaye aliweza kufahamu tabia hii ya Bwana Yesu. Mara nyingi walikuwa na mazoea ya kumwona Yesu akitenda kwa huruma na upendo na unyenyekevu. Hawakutarajia kwamba aweze kutenda hivyo. Basi, tujaribu kufahamu maana ya tabia ya Yesu.

Watu walikuwa wamebadilisha mahali pa sala kuwa hali ya biashara. Alipowatoa wote hekaluni, Yesu alionyesha hamu yake kwa nyumba ya Mungu na hasira fulani kuhusu tabia ya kutoheshimu kwa Hekalu. Bila shaka mambo ambayo yalitendeka hekaluni yalitafsiri aina fulani ya dini iliyoko. Kwa  uwepo wa Yesu duniani aina hii ya dini imeisha na uhusiano wa kibiashara na Mungu imeshindwa. Uwepo wa Yesu unatangaza wakati mpya. Katika nafsi yake tunakuta Hekalu mpya, yaani mahali pazuri mno pa mkutano na Mungu. Katika Yesu mtu anaweza kukutana na Mungu kwa kweli. Mafundisho yake yaliwasaidia watu watafakari vizuri kuhusu lengo la Hekalu na tabia kamili kuhusu mahali huko. Msingi wa mafundisho yake ni kumwabudu Baba kwa Roho na ukweli. Hiyo ndiyo maana ya kuwa mwanafunzi wa Kristo, yaani kuwa hekalu pamoja naye.

Wale wanaokuwa wanafunzi wa Kristo wanaalikwa kuwa naye Hekalu jipya ambapo Mungu anaishi. Kwa njia ya ubatizo tumezaliwa upya kwa njia ya kiroho. Kwa njia hii tunabadilishwa kuwa mahekalu hai, yaani na makao yake Mungu. Kila mmoja wetu ndiye jiwe la ujenzi mkubwa unaoitwa Kanisa ambalo ni mwili wa Kristo na jumuiya ya imani na upendo. Kama mawe hai tunaalikwa kutenda pamoja kupitia ushuhuda wa maisha ili ujenzi huu kutimiza lengo lake. Utunzaji kwa urembo wa nje wa kimwili ni mzuri, lakini hauwezi kutuzuia ya kujali hekalu hai la Mungu ndipo ndani yetu. Hiyo ni kauli ya Mtakatifu Paulo katika waraka wake kwa Wakorintho: “Ninyi ni hekalu la Mungu na Roho wake anakaa ndani yenu”. Kweli kama jumuiya ya Kikristu tunaimarishwa na Roho wa Mungu ili tuweze kuzaa matunda mazuri, kwa kuwa vyombo vya wokovu wake. Imani tunayoishi katika jumuiya inatufanya mashahidi wa kweli. Ushuhuda wetu unatangaza ukaribu wa Mungu na hali mpya ambayo Yesu alileta katika nafsi yake mwenyewe.

Fr Ndega

Nenhum comentário: