sábado, 17 de março de 2018

"TUNATAKA KUMWONA YESU"



Kutafakari kutoka Yeremia 31:31-34; Waebrania 5:7-9; Yoh 12:20-33

Kutoka maandiko haya tunaanza kutafakari kuhusu fumbo la “Saa” ya Yesu, ambayo inajumuisha mateso, kifo na ufufuko wake. Kwa kupitia Saa hii yeye atamtukuza Baba na atamaliza kazi yake. Kazi ya Mwana Yesu ndio wokovu wa ulimwengu ambao ingawa ulikwisha tendeka kwa wote lakini kila wakati unaomba kukubali kwa hiari kutoka kila mtu. Upendo wa Mungu uliofunuliwa na Yesu ndilo Agano Jipya ambalo liliandikwa moyoni mwetu na kutupa utambulisho wa Watu wa Mungu. Tunataka kumuona Yesu kwa njia yake ya kujifunua mwenyewe na kujifunza kutoka kwake kuishi kama chembe ya ngano ambayo inakufa ili kutoa mazao mengi.   

Somo la kwanza linaongea kuhusu Agano jipya ambalo Mungu ataanzisha na Watu wake. Litakuwa tofauti sana na Agano la kwanza lililoandikwa katika mawe nao watu walikosa kwa uaminifu. Tabia kamili kwa agano hili jipya ni uhusiano wa ndani kati ya Mungu na watu wanaoalikwa kuishi kulingana na Neno lililoandikwa na Mungu moyoni mwao. Basi, Mungu anaongea na watu wake kutoka moyo kwa moyo ili wajione kutibiwa kwa upendo na huruma. Bila msamaha hakuna maridhiano, tena hakuna furaha. Uaminifu na hisia ya kuwa watu wa Mungu itakuwa utambulisho mpya wa watu hawa: “Nitakuwa Mungu wao nao watakuwa watu wangu”.

Kulingana na mwandishi wa Waraka wa Waebrania, kupitia utii kwa mapenzi ya Mungu, Yesu alianzisha Agano Jipya na kukubali kuteseka ili kutoa maana mpya kwa mateso ya binadamu. Uzoefu huu ulikuwa nafasi ya kujifunza zaidi maana ya utambulisho wake wa kibinadamu. Mfano wake wa kujisalimisha kwa upendo ni njia kuishi kama pendekezo kwa wote.

Injili inaongea kuhusu mkutano muhimu ambao ulianza kwa ombi: “tunataka kumwona Yesu”. mazingira ya tukio hili yalikuwa sherehe ya Pasaka ambayo Wagiriki na watu wengine walikuja Yerusalemu ili kushiriki pamoja na Wayahudi. Wagiriki walimkaribia Yesu kupitia Andrea na Filipi walio wanafunzi wake. Tamani ya Wagiriki ya kumwona Yesu ilikuwa zaidi ya udadisi wa kumwona mtu maarufu. Kitenzi “kuona” hapa kunamaanisha kujua kwa njia ya ndani kuhusu utambulisho wa Yesu. Basi, yeye alichukua nafasi ya kuwafundisha wanafunzi wake tena jinsi anavyotaka kutangazwa, yaani kama Masihi mtumishi ambaye alijisalimisha kwa upendo.

Tukio hili inatukumbusha ile la mwanzo wa injili ambalo wanafunzi wa Yohana Mbatizaji walitaka kumjua mwalimu Yesu naye aliwaalika watembelee mazingira yake, yaani “mjoni nanyi mtaona”. Ni mwaliko wa kufanya uzoefu. Hakuna njia nyingine ya kumjua Yesu. Msingi wa injili hii ni ‘ ‘Saa’ ya Yesu. Neno hili ndilo muhimu katika injili hii ya Yohana. Tunaweza kukuta vifungu vingi ambavyo vinaongea kuhusu jambo hili. Yesu alijaribu kuelea akiutumia mfano wa Chembe ya ngano ambayo inakufa ili kuzaa mazao mengi. Hivyo, muhimu ya tafakari yetu sio kifo bali maisha mengi. Saa yake Yesu inajumuisha mateso, kifo na kufufuka. Ndio upendo ulimwimarisha Yesu kutenda hivyo.  Hivyo, mkutano wa kweli na Yesu ni kushiriki katika fumbo la kujisalimisha kwake.  

Kumwona Yesu ni hamu ya moyo wa binadamu, kwa sababu Yeye ndiye wa kipekee anayeweza kumdhihirisha Baba. Maisha yake ya kibinadamu yalikuwa bila utukufu daima (Kenosis, neno la kigiriki), akichukua njia ya mtumishi, kwa sababu alikuja kutumikia sio kutumikiwa. Hivyo, kila mtu anayetaka kumfuata anapaswa kufanya vivyo hivyo. Watu ambao wanatukaribia kumtafuta Yesu, hawataki tuongelee Yesu fulani kulingana na maneno yetu, bali Yule aliyejisalimisha kabisa kwa ajili yetu akikubali msalaba kama ishara kubwa ya upendo. Hivyo, hakuna njia nyingine ya kuwa wanafunzi wake wa kweli ila tukubali kuwa wa mwisho ili kuwa wa kwanza; kuyatoa maisha ili kuyapokea baadaye; kufa ili kuishi milele. Tunaweza kushiriki katika ushirikiano ambao Mwana anaishi na Baba ikiwa tuko na uwezo wa kuyatoa maisha kama Yesu. Mashahidi wengi wa historia ya Kikristo walikuwa na uhakika huu. Watu wengi wanaendelea wakifa ili wengine wengi waweze kuishi sio kwa njia yoyote bali kwa heshima. Kwa upande wetu, hakuna njia nyingine ya kuwa waaminifu kama wanafunzi wa Yesu ila kuyatoa maisha kama yeye alivyo. Kwa hivyo, "tunataka kumwona Yesu".

Fr Ndega

Nenhum comentário: