domingo, 24 de dezembro de 2017

MWOKOZI WETU NDIYE MUNGU PAMOJA NASI


Kutafakari kuhusu Luka 2, 1-14

Tangazo la kuzaliwa kwake Yesu ndio ujumbe wa furaha kubwa kwa wote, kwa sababu Mwokozi amezaliwa kwa wote. Tufurahi kwa sababu Mungu anatupenda, yeye yupo kati yetu na kuleta wokovu kwetu. Mungu aliweza kufanya mambo yote peke yake lakini alipendelea kuuomba msaada wa Bikira Maria, wa Yusufu na wengine wengi. Katika mpango wake wa wokovu watu wanaalikwa kufania kitu kulingana na uwezo kibinafsi wa kila mtu. Katika tukio la kuzaliwa kwa Yesu, Mungu alionyesha njia yake mwenyewe ya kutenda, yaani, tukio rahisi na mahali padogo na watu wanyenyekevu. Hali hii inathibitisha msemo wa Afrika ambao husema, “watu wanyenyekevu, wakifanya vitu rahisi na katika mahali padogo wanaweza kubadilisha ulimwengu.” Mabadiliko makubwa ambayo jamii yetu inahitaji yapaswa kutokea ndani ya binadamu. Jamii mpya itatokea wakati kila mtu atambue haja ya kujibadilisha mwenyewe badala ya kujaribu kuwabadilisha wengine. Kulingana na Baba Mtakatifu Francisco, “Dunia itabadilika ikiwa tuanze kuyabadilisha matendo yetu kupitia tabia zetu na chaguzi zetu.”
Katika Yesu, Mungu amekuwa mmoja wetu, akichukua hali yetu ya kibinadamu na kulitoa pendekezo mpya la maisha. Kwa hivyo haitoshi kumkiri Yesu kama wokovu wa Mungu; ndiyo muhimu turuhusu kuongozwa na ujumbe wake wa amani na upendo. Kwa kuzaliwa kwake, Yesu aliwafanya binadamu wote kuwa ni familia moja na kujaza mioyo ya watu kwa furaha na matumaini. Kweli, Mungu anajifunua kama jirani, maskini na anayekataliwa, kutualika kutambua thamani ya ishara ndogo na miradi midogo. Katika ufalme, wake wadogo na waliokataliwa wanakuwa ni wakuu.
Wachungaji pia wanatufundisha sana. Hao walikuwa watu waangalifu ambao walichunga wanyama wao karibu na Bethlehemu wakati wa usiku. Walikuwa kweli waangalifu kwa sababu ndani yao hamu ya Mungu na uhakika wa ukaribu wake ulikuwa hai sana. Hivyo, hao walikuwa watu wa kwanza wa kuipokea habari ya kuzaliwa kwa Yesu kwa sababu mioyo yao ilikuwa macho. Mtu aliye na moyo makini anaweza kuamini katika habari njema na kutarajia hali nzuri katika kilaalfajiri mpya”. Mtu aliye na moyo makini ana ujasiri wa kuanza safari kwenye mkutano na Mungu katika mahali pasipotarajiwa, yaani katika hali ya mtoto mdogo na mahali maskini sana.
Mungu Mwenyezi alikubali kuwa ni mtoto mdogo, akiutegemea utunzaji na upendo wa binadamu. Akifanya hivyo, anatufundisha tuwe na unyenyekevu na kukubali udhaifu wetu wa kibinadamu ulio muhimu katika uhusiano wetu nawe. Imani inatuongoza kumtambua mtoto huyu mdogo wa Bethlehemu katika kila mtoto ambaye hukutana na sisi katika safari yetu ya kila siku. Kila mtoto anaomba upendo wetu. Tufikiri leo, kwa njia maalum, kuhusu baadhi ya watoto ambao hawana uzoefu wa upendo wa wazazi wao wala hawana mahali pa kuishi; kuhusu watoto ambao wanatumika kama askari, wanaobadilishwa katika vyombo vya vurugu, badala ya kuwa vyombo ya upatanisho na amani; tena kuhusu watoto walio waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia, na kuhusu watoto maskini waliolazimishwa kuziacha ndoto zao kwa sababu ya hali yao mbaya ya kiuchumi. Mwanga wa Bethlehemu uguse mioyo yetu ili tuwe na utunzaji na upendo kwa walio na mahitaji mengi.

Ingawa sisi huishi katika jamii ya ulaji ambayo inatuzuia kushughulika kwa thamani muhimu sana, tunapaswa kuwa macho. Krismasi si ulaji. Ni sikukuu ya ufunuo wa Fumbo la upendo wa Mungu unaoweza kubadilisha moyo wa kibinadamu. Upendo wa Mungu kwetu haitegemei astahili yetu bali wema na ukarimu wa Mungu mwenyewe. Uzoefu huu unatuimarisha tufanye vivyo hivyo ili kushinda hali ya vurugu na chuki katika hali yetu. Hivyo, Krismasi itakuwa sio kipindi kimoja kwa mwaka bali kila wakati. Itakuwa Krismasi daima ikiwa tujifunze kupenda kwa njia ya kweli na kuweka juhudi zaidi ili kujenga jamii ya undugu na haki kwa wema wa wote

Fr Ndega

Nenhum comentário: