sábado, 9 de dezembro de 2017

MTINDO KAMILI WA KUANDAA NJIA YA BWANA


Kutafakari kutoka Is 40, 1-5, 9-11; 2Pt 3, 8-14, Mk 1, 1-8

 

Maandiko haya yanatualika kuandaa njia ya Bwana kupitia safari ya kutubu, kwa kukubali mapendekezo ya Neno la Mungu na kutangaza habari njema kutoka uzoefu wa Neno hili. Wale ambao waliongea kwa jina la Mungu walikuwa watu waliobadilishwa na Neno hili kwa njia ya ndani na kwa hivyo, walikuwa mashahidi wa kweli. Mtu yeyote ambaye anaongea kwa jina la Bwana, anaweza kusaidia wengine watembee katika njia ya Bwana.
Nabii Isaya alitabiri kuhusu wakati mpya kwa watu waliokuwa wakiteseka uhamishoni mwa Babeli na kuutarajia ukombozi. Mungu hakuwasahau watu wake na kutaka waonje hali mpya. Hata hivyo ni lazima kuandaa njia ya Bwana, yaani, maisha yao wenyewe. Kama kosa la uaminifu kwa Mungu lilisababisha uhamisho, hakuna njia nyingine ya kuona maisha mapya ila uzoefu wa huruma ya Mungu kwa kupitia kutubu. Mungu anaonyesha enzi yake hasa anapoonea huruma. Hivyo, utukufu wake unadhihirishwa zaidi wakati tabia yetu yabadilika kwa sababu ya mkutano na huruma hii. Hii ndiyo habari nzuri ambayo yapaswa kutangazika. Katika somo la pili, maneno ya Petro ndiyo ushauri ili watu wasubiri ujio wa Bwana wakiwa macho na kujitolea kwa manufaa ya jumuiya. Kulingana na Petro, Mungu ni mvumilivu na mwenye huruma. Hivyo, yeye hataki kuwaadhibu watu, bali atarajia waweze kutubu na kuokolewe.
Miongoni mwa wainjilisti ndiye Marko peke yake ambaye anaingiza injili yake kwa kutumia maneno Habari njema wakati anapoongea kuhusu Yesu. Maneno haya habari njema yalijulikana wakati wa Yesu, lakini hayakutumia katika maana ya kidini; yalitumia ili kutangaza habari ya furaha, mfano, kuzaliwa kwa mfalme ama kutembelea kwa mfalme katika sehemu fulani ya ufalme wake. Tangazo la habari hii lilileta matarajio ya mabadiliko ya hali, lakini baadaye mambo yote yakaendelea kama kawaida. Nia ya Marko ndiyo kujibu swali kuhusu utambulisho wa Yesu, yaani, Yesu ni nani? Kweli katika mwanzo na mwisho wa injili hii tunakuta maneno ‘Mwana wa Mungu’ kumhusu Yesu na mambo yote ambayo Yesu anatenda katika injili hii yaonyesha kwamba Yesu anatoka kwa Mungu kweli. Basi, kulingana na Marko, habari inayoleta furaha ya kweli kwa dunia hii ndiye Yesu aliye Mwana wa Mungu.
 Habari njema ya Yesu inaanza kupitia kazi ya Yohana Mbatizaji, ndiye nabii mkuu, kulingana na Yesu mwenyewe. Yohana anajulishwa kama mfano kwa wote kwa sababu alitumia nguvu zake zote ili kuwaandaa watu wakaribishe Mwana wa Mungu, ndiye Yesu Kristo. Yohana aliishi katika upweke wa jangwa na kufunguliwa kabisa kwa msukumo wa Mungu. Katika mahali hapo alijifunza kutokana na Neno la Mungu, jinsi ya kushuhudia habari njema za wokovu. Ndilo jambo la ajabu tabia yake ya unyenyekevu hasa kuhusu mavazi na chakula. Ukuu wa Yohana ulionyeshwa katika uwezo wake wa kutambua ukuu wa Bwana, akijifikiria mwenyewe kama sauti tu ambaye huandaa njia ya yule atakayekuja. Katika ujumbe wake, Yohana alitangaza huruma ya Mungu akisema: “Mmrudie Bwana! Mungu atawasamehe dhambi zenu.” Pamoja na maneno haya, Yohana aliwabatiza watu kama ishara halisi ya kutubu na makaribisho ya huruma ya Mungu.

Sababu ya uaminifu wa ujumbe wa Yohana ilikuwa sio maneno yake tu, bali pia unyenyekevu wake na njia ya kweli ya kuishi. Hata bila maneno, maisha yake yalikuwa tangazo la kweli la hali mpya ambayo Yesu alikuja kuleta duniani. Maisha ya Yohane yatuambia kwamba tunaweza kufanya tofauti maishani mwa watu, lakini ahadi haiwezekani bila uzoefu wa jangwa, yaani, uzoefu wa ndani wa Mungu na wa Neno lake. Ndio kutoka jangwa kwamba pendekezo la mabadiliko linakuja kwetu. Tukiishi uzoefu wa mabadiliko tunaweza kuwa mashahidi wa habari njema kwa uaminifu kwa sababu ushuhuda wa maisha ndio ufanisi kuliko maneno. Uvumilivu na huruma ya Mungu ndiyo nafasi tunayohitaji ili tuweze kumrudia yeye. 

Fr Ndega

Nenhum comentário: