quarta-feira, 22 de abril de 2015

UWEPO HAI

Kutafakari Kutoka Matendo ya Mitume 3:13-15, 17-19a 1Yohana 2:1-5a; Luka 24:35-48

        Ikiwa Yesu hakuwa amefufuka imani ya Kikristu ingekuwa utupu, haina maana. Lakini Yesu alifufuka na hiyo ni maana ya uanafunzi na ushahidi wa mitume. Tangazo la tukio hili kuu lilifanywa na Mitume kwa shauku na furaha kubwa, wakiazimu njia mpya ya kuishi. Wakati Petro alianzisha hotuba yake kwa Wayahudi, alimsifu Mungu, ambaye kwa nguvu yake, alimfufua mtumishi wake Yesu kutoka kwa wafu. Petro aliwakumbusha pia kwamba ingawa watu hao walimkataa Yesu, hawakukataliwa na Yesu, ambaye alitarajia mabadiliko yao, akiwatolea uwezekano wa ushiriki katika uhai wake wenyewe. Wayahudi walifanya chaguo mbaya kwa sababu ujinga wao kuhusu utambulisho wa Yesu. Lakini, kupitia huruma ya Mungu katika Yesu, wana pia nafasi mpya ya kuishi. Mtakatifu Yohana anathibitisha, katika waraka wake, kwamba kupitia upatanishi wa Yesu huruma hii ya Mungu inafikika kwa wote. Utii kwa Neno la Mungu na kuishi amri yake ya upendo ni vigezo kumjua na kuipitia huruma yake.
Mwanzo wa injili ya siku ya leo ni mwendelezo wa uzoefu uliishi na wanafunzi wa Emau. Walikuwa wakisimulia toleo lao la tukio kwa wengine kwa shauku na furaha wakati ghafla Yesu mwenyewe akaonekana katikati yao, akithibitisha simulizi lao na akiwatolea amani kwa wote. Uzoefu  wa kushiriki pamoja mkate sasa unaenezeka kwa kushiriki kwa maisha na udugu. Katika wakati wa kwanza, hofu na ziada ya shaka iliwazuia kumtambua. Kosa la uhusiano wa ndani kuhusu njia mpya ya uwepo wa Bwana lilisababisha upinzani mioyoni mwao, likiwafanya kumfikiria roho. Yesu alikemea tabia zao na aliwaonyesha ishara za ushindi wake, ni kwamba, mikono na miguu. Alitenda kwa uvumilivu, akiheshimu mwendo polepole wa ufahamu wao na akafungua akili yao kupitia tafsiri haki ya Maandiko Matakatifu kuhusu yeye mwenyewe kama masiya aliyeteseka na aliyetukuzwa. Yesu si pepo; yeye ni uwepo hai, ambaye anakula na wapendwa ili kujipatia utambulisho wao wa wanafunzi na kuwahamasisha kwa kazi. Sasa wana sababu zenye nguvu kwa kuchukua tena njia ya uanafunzi na kuwa mashahidi wa kweli ili kutangaza mahitaji ya kutubu na maridhiano na Mungu na miongoni mwa watu.       
Kupitia uzoefu wa wanafunzi hao tunatambua kwamba furaha ya mkutano na Yesu lazima kutangazwa na unahamasisha uzoefu wa jumuiya, kuijalisha kwa maana. Kwa hali hii uzoefu wa jumuiya na uzoefu wa ufufuko ni uhusiano kwa sababu Bwana Mfufuka yupo katikati ya jumuiya. Bila usaidizi wa jumuiya tuna ugumu kutambua uwepo wa Bwana Mfufuka. Jumuiya hutupa uungaji mkono kwa ushahidi wa kweli na wenye fahari daima kuhusu mkutano na Bwana, kuweza uzoefu uliojaa umaana kwa wale ambao lazima kuwa mashahidi wake. Ni yeye ambaye anawaelimisha ufahamu wetu ili tuweze kuelewa Maandiko Matakatifu, kukuta katika Haya maana ya kweli ya uwepo wake miongoni mwetu. Alikubali uzoefu wa msalaba kwa mshikamano na waliosulibiwa wa wakati wote. Basi, hakuna mtu anaweza kudai kumfuata Kristu bila msalaba. Hakuna mtu anaweza kudai kuwa mwanafunzi wa kweli bila kuchukua ajili ambayo Mwalimu Yesu alichukua. Ufufuko wa Yesu ulifanya upya matumaini yote na ulithibitisha kwamba mateso, maovu na mauti hayatakwi na Mungu, ambaye anaweza kubadilisha bahati mbaya kwa neema, kufanya kuangaza uhai ambapo mauti tu yalipo.

Mungu wa uhai anatuita kuishi katika jumuiya na yeye yupo katikati yetu ili kuwa rejea ya maisha yetu na kutufanya vyombo vya amani yake. Kama wanafunzi wa kwanza, sisi pia tunakabiliwa na hali halisi ambazo zinatuletea wasiwasi na mashaka. Wakati tuko tayari kwa uzoefu wa mkutano binafsi na Bwana Mfufuka, kupitia Ekaristi na kushiriki kwa udugu, tunaimarishwa katika imani na sisi huisaidia imani ya jumuiya. Uzoefu unatuweza kushinda vikwazo njiani, kutubadilisha kwa mashahidi ya upendo ambao huyazaa maisha. Adhimisho la Ekaristi hili lituhamasishe kwa uzoefu wa mkutano na Bwana Mfufuka yupo miongoni mwetu. Ikiwa Uzoefu una nguvu, ushahidi utakuwa ufanisi.  

Fr Ndega
Mapitio: Rose Mong'are

Nenhum comentário: