domingo, 12 de abril de 2015

FURAHA YA MAISHA AMBAYO YANASHINDA MAUTI


Tunaadhimisha kufufuka kwake Yesu, maana ya imani na maisha yetu. Kupitia yeye maisha yanajipatia maana kabisa. Mwanga yake inawaelimisha giza ya maisha yetu na inafungua upeo wa macho ya maisha  bila mwisho. Na sikukuu ya ufufuko tunaalikwa kwa furaha ya kweli, ni kwamba furaha ya maisha ambayo yanashinda mauti, furaha ya upendo ambao unashinda huzuni. Yesu ni uwepo hai mwongoni mwa wabinadamu, kufufua matumaini yao. Ni nafasi nzuri kufanya upya ahadi yetu ya wanafunzi na kushinda hofu ya kuwa mashahidi washujaa.
Masomo ya Agano la Kale yanatuonyesha njia ya kushangaza na tefu, ambayo Mungu alitumia kwa kuongoza historia: Uumbaji, Agano, Ukombozi, Maisha mapya. Mungu ametaka daima furaha kubwa kwa kila moja wa viumbe vyake. Furaha hii inatokana na uhai ndani ya Utatu, ushirika wa upendo. Uzoefu kubatizwa ni uzoefu wa ufufuko, kwa sababu kupitia ubatizo tunaalikwa kwa kuzaliwa upya. Kuzaliwa huko kunamaanisha kufa na Yesu, kuzika hali zee ya wenye dhambi na kufufuka tena na Yesu kama watu ambao wamefanywa upya kabisa.  
Kulingana na Injili ya Marko, wanawake walikuwa na upendeleo kuwa mashahidi wa kwanza wa ufufuko wa Bwana. Waliamuka asubuhi sana, kwa sababu walihamasishwa kwa upendo ndani ya Yesu ambao unawaongoza kumtafuta. Wakati uzoefu wa ufufuko kwao kaburi tupu na tangazo la malaika, lakini ishara mbili zilitosha ili kuongoza tena lengo la uchunguzi wao. Yesu hakuwa yupo pale; alifufuka kutoka kwa wafu; anaishi. Habari njema hii ya furaha kubwa inahitaji lazima kutangazwa. Baada ya dhahiri ushinde, ambao ulikuwa kifo chake, aliruhusu uwezo wa kuona kwa ishara za ushindi wake ulikuwa wa kupatikana kwanza kwa wale ambao walikuwa waathirika wa ubaguzi katika jamii na walihisi watengwa. Kwa kweli kupitia chaguo hilo Yesu alikuwa akithibitisha pendekezo lake la muda mpya, mawazo mapya na uhusiano mpya. Ili kufanya kazi muhimu ya tangazo ya ufufuko, wanawake walikuwa na kuondokana na hofu na mawazo ya kuwa chini. Walikuwa hakika kwamba Mtu ambaye aliwachagua alikuwa akienda nao.  
   Kama wanawake na wanafunzi wa kwanza wengine, tunaalikwa kufanya uzoefu wa Bwana Mfufuka. Uzoefu huu siku hizi unahitaji imani zaidi kuliko ishara. Neno lake na ushahidi wa wale ambao hutumia maisha yao kutumikia jumuiya unatusaidia kushinda hofu ambayo anafufua wakati mwingine katika safari yetu. Hofu hutuzuia kuishi, imani yetu ya kweli na kuwa mashahidi wa kweli. Na uungaji mkono wa wengine na hatua ya Mungu wa uhai miongoni mwetu, tunaweza kushinda hofu yetu yote na kukubali kwa furaha na shauku kazi muhimu ya kutangaza habari njema ya ufufuko wa Yesu.     
Yeye yupo Yeye yupo miongoni mwetu ili kuwa ndani ya maisha yetu na kutufanya vyombo vya amani yake. Kupitia uzoefu wa wanawake, sisi pia tunaalikwa kufanya uzoefu wa kumtafuta Bwana Mfufuka. Tuna hakika kwamba siku hizi mkutano huu unatokea kupitia Ekaristi, udugu na ishara zingine nying katika familiia zetu. Kama hii tunaimarishwa katika imani yetu na tunaisaidia imani ya jumuiya. Uzoefu huu unatuwezesha kushinda vikwazo njiani, kutubadilisha kwa mashahidi ya upendo ambao unaizalisha maisha. Bwana Mfufuka anaishi miongoni mwetu! Tunahitaji kuelimisha tena hisia zetu ili kumtambua in hali halisi nyingi ambazo zinaishirikisha maisha yetu. Yeye atupe ujasiri ili kuwa mashahidi wake wa kweli.


 Fr. Ndega
Mapitio: Sara

Nenhum comentário: