Kutafakari kutoka Is 45: 1,4-6; 1 Thes 1: 1-5; Mt 22:
15-22
Maandiko haya yanatualika kutafakari kuhusu hisia zetu za miliki ya Mungu kama
wana wa watu wake na kutafakari pia kuhusu majukumu yetu na maendeleo ya Taifa
la Kenya kupitia malipo ya kodi halali.
Somo
la Kwanza ni tafsiri ya imani kuhusu ushindi wa Koreshi, mfalme wa Uajemi,
ambaye aliwakomboa Wayahudi kutoka mamlaka ya Babeli. Kulingana na Isaya,
ushindi wote wa Koreshi haukuwa uhalali wake, lakini ulikuwa tendo wa Mungu,
ambaye alimchagua Koreshi kama mjumbe wake ili kufanya Jina la Bwana kujulikana
kwa Mataifa yote, kuwaalika kwa imani katika Mungu mmoja tu. Kwa kweli Koreshi
alipata kushinda Falme zote za Mashariki, ikiwa ni pamoja na Babeli, akiruhusu
kwamba Wayahudi walirudi nyumbani na wakaishi utambulisho wao wa Watu wa Mungu
na uhuru. Basi, kama ilivyotukia na Koreshi, Mungu anaweza kutumia mtu yeyote
ili kufanya mipango yake.
Paulo
na wenzake wa uinjilishaji wanatambua Vipawa vya Mungu katika Jumuiya ya
Wathesalonike, hasa fadhila za imani, upendo na tumaini, zinazowatambua kama
wachaguliwa wa Mungu na mali yake. Katika maana hii, matendo yao yanafanywa
chini ya neema ya Mungu, kulingana na Injili waliyoichukua kwa shauku. Uzoefu
alioishi Paulo na Jumuiya hiyo na zengine ni kielelezo ili kufahamu bora uzoefu
wa Jumuiya siku hizi.
Wapinzani
wa Yesu wanamsifu kwa fadhila zake, lakini hawana nia kuwasilisha kwa hekima
yake. Kulingana na wao, Yesu ni mtu wa kweli, anayefunza njia ya Mungu kwa
mujibu na ukweli. Yesu ana maoni yake mwenyewe na kwa yeye mtu ni muhimu zaidi
kuliko hali yake. Ingawa waliongea ukweli kuhusu Yesu, katika mazungumzu yao,
inakosa imani ili kuukubali kama njia ya maisha yao. Yesu anatambua kwamba ni
mazungumzu mabaya na lengo la kumnasa. Kama Yesu aliwaambia “ndio” kwa swali
lao kuhusu malipo ya kodi, angechukuliwa mshirika wa utawala wa Warumi kwa
Wayahudi. Ikiwa jibu lake likawa “hapana kwa malipo ya kodi” angechukuliwa
mwasi. Basi, Yesu aliwaambia: “Mpeni Kaisari kilicho cha Kaisari na mpeni Mungu
kilicho cha Mungu”. Jibu lake linasisitiza ukuu na kipaumbele cha Mungu juu ya
wote na kila kitu.
Mahali pa kwanza katika maisha
yetu ni kwa Mungu. Yeye ndiye mwenye nguvu kwa kila mtu, ikiwa ni pamoja na
watawala. Sheria yake lazima iwe maarufu kwa sababu inaonyesha bora matarajio
ya binadamu. Hata kama tunakabiliwa na Serikali na sheria yake, hawawezi
kuchukua mahali Katika maisha yetu ambapo ni kwa Mungu na sheria ya binadamu
haiwezi kuweka upinzani kwa Sheria ya Mungu. Mungu tu anastahili kuabudiwa na
kutumikiwa. Hata hivyo, Yesu hakukataa umuhimu wa malipo ya kodi halali, kwa sababu upendo kwa Mungu
hautuzuii kushirikana na maendeleo ya nchi. Bali, kama Wakristu, kuchagua kwetu
ni kwa uhai na kwa kila kitu kinachoshirikana na lengo hile.
Kupitia sherehe ya Eukaristia
hii, tutengeneze upya ahadi yetu kama wana wa Mungu na miliki yake. Kupitia
msukumo wake, tuwe mashahidi wake wa nguvu na uzuri katika mitazamo ya
maendeleo ya haki na amani katika jamii.
Fr. Ndega
Mapitio: Mwalimu Patrick
Nenhum comentário:
Postar um comentário