Kutafakari
kutoka Luka 10, 25-37
Sehemu ya kwanza ya injili hii
inatukumbusha kuhusu andiko la mtu mmoja tajiri anayekuja kwa Yesu na swali
sawa: Nifanye nini ili kupokea uzima wa milele? Jibu la Yesu linafanya kumbukumbu ya amri ya Sheria, kuonyesha kuwa yeye anathamini
sana Mwelekeo huu kwa maisha. Yesu anapendekeza amri hizi kwa sababu haziende kinyume cha uhuru, lakini zinahusiana kwa hamu ya ndani ya binadamu katika kutafuta kwake kwa mafanikio ya binafsi. Kulingana na Yesu, amri si orodha ya sheria kukariri,
lakini ni uongozi kwa kuishi vizuri, kumpenda Mungu na kukua katika udugu kupitia
upendo halisi kwa jirani.
Swali: jirani yangu ni nani? linaonyesha kwamba kitu fulani si kizuri
sana katika ufahamu
wa amri. Labda mtu aliyeuliza swali kwa
Yesu alidhani kwamba ukumbusho wa Sheria ulikuwa wa kutosha kwa kumsifu Mungu. Hali hio inaweza tukia pia na sisi kwa
sababu, wakati mwingine, sisi hukaa na wasiwasi sana katika kutii sheria
na sisi husahau muhimu
zaidi katika uhusiano na watu wengine. Wakati tunauliza: jirani yetu ni nani?, kumbukumbu
ni daima sisi wenyewe
na uradhi wa mahitaji yetu. Lakini mfano ambao Yesu
anaongea kuhusu unaweka kumbukumbu nje yetu,
unabadili swali: unawezaje kuwa jirani kwa wengine?
Kuwa jirani si rahisi
sana kwa sababu tuna shughuli daima na kufanya vitu kwa haraka. Tulivyo na shughuli ndivyo tuna upunguvu
wa uwezo kujali mahitaji ya wengine. Ni lazima tubadilishe mawazo yetu na kukaribisha mfano wa Yesu ambaye ni Msamaria Mwema kwa ubora. Yeye anatufundisha kwamba uzima wa milele unawezekana tu kama upendo kwa Mungu unaishiwa mazoea ya upendo kwa wengine.
Kwa Yesu, upendo
ni halisi na kweli
wakati unaeleza kupitia ishara za upole na huruma. Kanuni ya kawaida kuishi
vizuri katika maisha ya shirika katika
kazi ni sisi wenyewe kutumika bora
kwa wema wa wengine, kusaidia katika mahitaji yao,
kwenda mbele ya mpango imara.
Yesu anajitambulisha na wale
ambao "wameanguka kando ya
njia". Je, tunaweza kutambua uwepo wake katika watu ambao kwa kawaida hukutana nao? Jinsi gani tunaitikia mahitaji ya wengine
wakati tuna haraka?
"Ee Bwana, fungua macho yetu ili kuona mahitaji ya ndugu
zetu. Tuhamasishe maneno na
vitendo katika huduma kwao". Amina.
Fr.
Ndega
Mapitio:
Mwalimu Patrick
Nenhum comentário:
Postar um comentário