Kutafakari kutoka Luka 11, 29-32
Katika kifungu hiki cha injili, Yesu anaonyesha kukosekana kwa uvumilivu
na wale ambao walitamani kwa ishara. Mahitaji kwa ishara
yalikuwa aina ya majaribu yaliyokataliwa na Yesu katika
jangwa na, kulingana na andiko la mwisho kuhusu majaribu, mshawishi angekuja
tena katika maisha ya Yesu katika wakati muafaka. Basi, hiyo ni moja ya nyakati kadhaa. Mahitaji kwa ishara yanaonyesha upinzani dhidi ya ujumbe wa Yesu, ni kwamba
Neno lake. Yesu alitumia nafasi hii ili kuwafundisha kuhusu kazi yake na utambulisho. Yeye
anarejesha historia ya Yona,
mjumbe wa Mungu, ili kusaidia watu kugundua
mtindo mpya kwa maisha yao. Watu
waliamini katika ujumbe wake
kwa ubadilishaji. Solomoni pia anatajwa na
Yesu kama kumbukumbu
kuelewa njia za Mungu. Hata hivyo, Yesu
anawashinda ndio hao
wawili kama ishara ya Mungu kwa ubora.
Historia ya wanadamu ina wingi wa ishara ambazo Mungu
amekuwa akiongoza watu kwa wokovu. Lakini
ishara yake kubwa ni Yesu, kumbukumbu ya Historia hii na timizo Maandiko.
Uwepo wake miongoni mwetu ni ishara ya upendo na
huruma ya Mungu, kuonyesha
mtindo mpya ya maisha kwa sababu yeye mwenyewe
ni Uhai. Anatangaza ukweli wa
Mungu kuhusu binadamu
kwa sababu Yeye mwenyewe ni Ukweli. Anaelekeza nyayo
zetu kwa Mungu kwa sababu Yeye mwenyewe ni Njia.
Kama wafuasi wa Yesu hatuhitaji ushahidi ili kumwamini kwa
sababu uhakika wa uwepo wake daima
maishani mwetu unatutosha. Kuhitaji ishara zaidi
badala ya Yesu, ni
kuweka Mungu kwa majaribu. Ishara ya Mungu
inaweza kuwa isiofaa kwa maisha yetu kama
hatuonyeshi ishara ya ubadilishaji
kama wenyeji wa Ninawi
mbele ya ujumbe wa Yona. Ubadilishaji ni
ishara ya ukomavu wa imani.
Bwana atujalie neema hii.
Fr. Ndega
Mapitio: Mwalimu Patrick
Nenhum comentário:
Postar um comentário