sábado, 30 de março de 2019

MUNGU WA YESU


Kutafakari kuhusu Lk 15, 1-3.11-32


Sura ya kumi na tano ya toleo la Luka ni maarufu miongoni mwa mifano ya Yesu. Inaitwa sura ya Mifano ya huruma. Tuna mifano mitatu (Kondoo aliyepotea: 4-7; Sarafu iliyopotea: 8-10; Mwana mpotevu: 11-32). Katika nafasi hii tunaalikwa kutafakari kuhusu mfano mmoja peke yake, yaani mwana mpotevu ama baba mwenye huruma. Mfano huu ndio maonyesho ya tabia ya huruma ya Mungu kwa ajili ya wenye dhambi kwa sababu ya upendo wake mkubwa.

Kwa kufahamu nia ya Yesu wakati aliposimulia mfano huu tunahitaji kutafakari kwanza kuhusu mazingira ambayo Yesu aliishi. Yeye ndiye sura ya huruma ya Mungu naye alifunua huruma hii siyo kwa maneno tu bali pia kwa matendo. Kwa hivyo, kulingana na andiko hili watozaushuru na wenye dhambi walimkaribia Yesu ili kumsikiliza. Wasingalifanya hili ikiwa wasingekuwa na uhakika wa kukaribishwa vizuri na Yesu. kwa upande mwingine, tuko na kikundi cha pili, kilichojumuisha Mafarisayo na Waandishi wa sheria ambao walichagua kimanung’uniko, kukosoa na kupinga ishara za Yesu kwa ajili ya kikundi cha kwanza.

Chote vikundi viwili ingawa vilikuwa na uzoefu tofauti ya Mungu na tabia tofauti kumhusu Yeye, watu hawa ni wanawe na hao ndio wapendwa naye. Hakuna hata kimoja kijuacho sura ya kweli ya Mungu kwa sababu watu wa kikundi kimoja fulani walijiona kama wenye haki na kuwalaumu watu wa kikundi kingine ambao walijikiri kama wenye dhambi, yaani bila nafasi ya kuondolewa dhambi yao. Katika mkutano na Yesu walivutiwa na huruma na, kwa hivyo, nafasi mpya kwa maisha yao. Hayo ndiyo mazingira ambayo Yesu alitumia ili kuumba hadithi hii ya Baba mwenye huruma. Tunataka kujifunza mengi kutoka kwa Baba huyo.
           
      Ingawa yako matukio mengi katika Agano la Kale ambayo yanaonyesha njia maalum ya Mungu ya kutenda, ni “katika Yesu Kristo kwamba huruma ya Mungu imepata kuwa hai na yenye kuonekana, na hata ilifikia kilele chake katika Yeye... Yesu ni uso wa huruma ya Baba. Kila kitu ndani yake kinaongelea huruma. Hakuna chochote kwake kinachopungukiwa na huruma (Baba Mt Francisco).”  

      Katika mfano wa mwana mpotevu, ingawa tuko na vitendo vya kijana mdogo na kijana mkubwa, macho yetu yamlenga baba wa vijana hawa wawili ndiye aliye mhusika mkuu wakati wote. Muhimu ya tukio hili ni uhusiano wake wa upendo kwa ajili ya vijana wake ambao wote ni wapotevu kwa njia tofauti. Kulingana na Yesu, Mungu ni kama baba mmoja aliye na watoto tofauti na kushiriki nao zawadi zake kwa njia sawa. Yeye anawapenda wote na kutaka wajione wakiwa katika familia, kushiriki katika furaha yake ya baba. Katika familia hii anautoa utunzaji na ulinzi ili wawe na maana nzuri ya kukaa katika ushirika naye daima. Wakati yeyote anapoamua kujitenga naye na kuenda mbali kutoka kwake sio kwa sababu anashindwa kupendwa, bali ni kwa sababu anajiona mwenye uhuru. Baba huyo anaheshimu uhuru wa watoto wake na kuwahakikishia makaribisho wakati wanapoamua kurudi nyumbani.

       Basi, mara nyingi uzoefu wetu ni kama vile hali hii. Tunajiona mbali na Mungu wakati sisi hutenda dhidi yake, yaani tunapomkosea. Yeye anajihisi ameachwa na kusalitiwa, lakini hashindwi kutupenda. Kama yule baba, Mungu anashughulika sana na maisha yetu kwa kutupatia ulinzi na utunzaji wake. Kwa hivyo tunahisi majuto na kuvutiwa ili kuishi tena uzoefu wa ushirika ambao tumepoteza. Ingawa mara nyingi hatuishi kama wanawe, kwa sababu ya dhambi zetu, Mungu anabaki mwaminifu daima kama Baba mwema. Huruma yake ina nguvu kuliko makosa yetu.

     Katika mfano huu yuko pia mwana mkubwa ambaye hajihisi mwana, kwa sababu anajiona kama mfanyakazi, wala hajihisi ndugu, kwa sababu anamkataa ndugu yake mdogo. Tabia ya huyo mwana mkubwa inaizuia furaha na sikukuu kwa kikamilifu. Kumrudia Mungu ni maana ya furaha kubwa kwake. Lakini furaha yake haiwezekani kuwa kabisa ikiwa hatushiriki katika hisia zake kuhusu wengine. Yeye anataka kwamba tutende kama yeye alivyo. Kwa hivyo Yesu alisema, “Muwe na huruma kama Baba yenu alivyo.” Upatanisho na wengine ni kipimo ili uhusiano wetu na Mungu uwe kweli. Hii ni njia ya kweli ya toba iliyo mwendo wa muda mrefu na huanza mioyoni mwetu. Turuhusu kuguswa na huruma ya Mungu ili tuweze kuwa vyombo vya huruma hii kwa wale wanaohitaji msamaha wetu.

Fr Ndega

Nenhum comentário: