Kutafakari kutoka Kumbukumbu
la Sheria 18: 15-20; 1Wak 7: 32-35; Marko 1: 21-28
Masomo haya ni mwaliko kwa sisi sote kukaribisha mafundisho
ya Neno la Mungu ambalo lina
uwezo wa kubadili maisha ya watu,
kuwapa uwezo ili kuwa wajumbe wa wakati mpya. Kulingana
na Somo la Kwanza, nabii ni mtu aliyeitwa kutoka
kati ya watu ili kuongea nao tu
ambayo Mungu anamwuliza kusema. Msukumu wa Mungu, pamoja na upatikanaji
wa nabii, ulifanya utofauti mkubwa
katika maisha ya watu wa Israeli,
ukiwaongoza kupitia maisha mapya. Mtakatifu Paulo anasifu mtu anayejituma
kwa huduma ya Bwana na anawamotisha
wengine wote wa jumuiya kuendelea
kumtumikia kwa kujisalimisha kabisa bila rizavu.
Yesu anaanza kazi yake kwa umma
kutangaza Ufalme wa Mungu na kuwaalika kwa kitubio. Kama hii, aliwaita wanafunzi wa kwanza, kulingana na kutafakari kwetu wiki
iliyopita. Yesu anawaalika wanafunzi
wake kukaa pamoja naye na anawafundisha
kupitia uzoefu wa maisha. Sehemu nyingi ya
miujiza ambayo yeye hufanya, yeye anafanya mbele ya wanafunzi wake. Tangu mwanzo, wanafunzi wake wamealikwa
kushiriki katika kazi yake na
kushiriki hisia zake kuhusu hali
halisi ya watu, hasa hao maskini.
Yesu hupenda kutembelea
na kufundisha katika masinagogi
kwa sababu katika mahali hapo kwa kawaida watu husanyika kusikiliza Neno la Mungu na kukubali mapenzi yake. Hali hii ilikuwa pia nafasi nzuri kuwafundisha wanafunzi wake, kuwasaidia watu kufungua
mioyo kwa mapitio ya Mungu.
Mamlaka yaliyopewa Yesu na Baba
mwenyewe yanaonyesha ubora wa mafundisho yake kabla ya njia ya mwandishi. Kidogo kidogo watu walikuwa wakielewa kwamba mtu huyo Yesu, ambaye
alizungumza kwa upendo na ukweli,
alikuwa mjumbe wa Mungu. Maneno yake yenye
uhai kabisa na yanaongoza kwa kitubio. Njia yake ya kuzungumza
ilizaa katika moyo
shauku kwa ajili ya Ufalme. Kama mjumbe wa Mungu, yeye
ni wa kipekee na mamlaka ya kufundisha watu. Wale ambao wana kazi ya kuongoza watu,
lazima kusikiliza sauti yake. Hata pepo wachafu wanatambua utambulisho na mamlaka ya Yesu, lakini hawashiriki ahadi
yake kwa ajili ya ubinadamu. Kwa hivyo, Yesu
hazungumzi nao; yeye tu anawamuru, kuwanyamazisha. Pepo wachafu hawa ni ishara ya nguvu za upinzani kwa mpango
wa Mungu, kudhoofisha watu na
kuwazuia kuonyesha uwezo wao kwa njia kamili. Kabla
ya nguvu hizi, Yesu anaweka mamlaka na anatenda
kama Mkombozi.
Uwepo wa Yesu kati ya binadamu unatawaza
wakati mpya, ni kwamba, wakati wa wokovu
wa Mungu. Wokovu uliowasilihswa
kupitia kinywa cha Yesu kinaongozwa na ishara halisi ya ukombozi.
Kulingana na matendo ya Yesu, nguvu ya Neno la
Mungu haitoki kwa tafsiri ya binadamu, lakini inatoka kwa msukumu wa
Mungu. Kwa hivyo mafundisho yake
yanachukuliwa mapya sana. Lakini haitoshi kutambua utambulisho wa Yesu
kama Masihi wa Mungu, kwa sababu
hata pepo wachafu wanafanya hivyo. Ni
muhimu kukubali pendekezo lake la
kitubio, kuruhusu uwezo wake kuondoa pingu ambayo inatuzuia
kufanya uhusiano mzuri na Mungu
na wengine. Upinzani dhidi ya
Yesu ni upinzani kwa utambuzi wa Ufalme wa Mungu. Kwa hali hii, tunatenda kama wapinzani wa Mungu, kutoweza kufuata kwa uaminifu nyayo
za Mwana wake ambaye, wakati anatangaza habari
njema ya Ufalme, anauliza kwa ushiriki
wa bure na jumla ya kila mtu. Kwa
upande wetu, kutafuta Ufalme
huu lazima uwe kipaumbele, kwa sababu juu
yake maana ya maisha na kazi zetu
huweka.
Ujumbe wa injili hii ni pendekezo
la uanafunzi upya. Ni mwaliko kwa sisi kupitia uwezo wetu wa kujisalimisha kwa mtu ambaye ametuita na
anataka kwamba tuwe wajumbe wake.
Yeye anatambua mwenyewe na wale waliomfuata yeye, Yesu anaendelea kutenda dhidi ya nguvu yoyote au mawazo ambayo yanaonea maisha ya watu. Kwa maneno mengine, kupitia matendo yetu, ishara za ukombozi
wa Kristo bado zinatokea katika maisha ya watu wengi. Kutoka kwake tunapokea mamlaka kuwa watu
halisi ili kusema
ukweli. Hakika kwamba Yesu anaambatana
nasi katika safari yetu, inatumotisha
kupigana dhidi ya maovu na dhambi zote
ambazo zinatuzuia kumtumikia Mungu
kwa ukarimu na bure. Neema yake itusaidie
kufanya kusudi hili.
Fr. Ndega
Mapitio: Mwalimu Patrick
Nenhum comentário:
Postar um comentário