Kutafakari kutoka Mwanzo 9:
8-15; 1Pt 3: 18-22; Mk 1: 12-15
Tumeanza
safari yetu ya toba inayoitwa Kwaresima. Kipindi hiki kinapendekeza safari ya ubadilifu,
kutuandaa kuadhimisha mafumbo makuu ya imani yetu, kufanya upya ahadi yetu na maisha
mapya kutokana na Kristo na ufufuo wake. Msimu wa Kwaresima ni mafungo makubwa
ya muda wa siku arobaini kwa Wakristo wengi, kutukumbusha kuhusu muda wa siku
arobaini ya Musa juu ya Mlima Sinai ili kuzipokea Amri na miaka arobaini ya
safari ya usafishaji wa watu wa Israeli katika jangwa na uzoefu wa Yesu katika
jangwa pia kabla ya kazi yake. Yesu alishinda majaribu yote kwa sababu akajiruhusu kuongozwa na Roho
Mtakatifu. Kila mtu ambaye anazifuata nyayo zake, na aliyefunguliwa kwa safari
ya ubadilifu, yeye husaidiwa na nguvu kutoka juu ili kufanya mapenzi ya Mungu
kwa mafanikio.
Masomo
ya Jumapili hii yanatuingiza katika safari ya upya wa ubatizo wetu, kutuonyesha
njia iliyopendekezwa na Mungu ili kufanya maisha mapya duniani. Kupitia Nuhu na
familia yake Mungu anafanya agano la kwanza na ubinadamu, kufanya upya uumbaji
wote. Pendekezo hapa ni uumbaji upya, ambao hutokea wakati mwanadamu hubadilisha
chaguzi zake, kufanya uhusiano mpya na Mungu na viumbe vyingine vyote vilivyo
hai. Agano ni ishara kwamba Mungu hataki kupoteza binadamu, kupendekeza daima
nafasi mpya ya utakaso na ubadilifu. Katika somo la pili, Mtakatifu Petro
anaongea kuhusu athari ya gharika kwa uumbaji wote kama ishara ya ubatizo ambao
humtakasa, kumpa binadamu maisha mapya katika Kristo.
Katika
sehemu ya kwanza ya injili, Yesu anaongozwa jangwani kwa nguvu ya Roho. Kama
hii alihamasishwa sana kuishi uzoefu huu kulenga katika maandalizi ya kazi iliyokabidhiwa
na Baba. Katika Biblia, Jangwa ni mahali pazuri daima kukutana
na Mungu na palikuwa ni mahali pale ambapo Watu wa Israeli walihisi upendo na ulinzi
ya Mungu mara kwa mara. Kwa Yesu uzoefu huo ulikuwa wa maana na Kupitia huo aliweza
kutambua bora mpango wa Mungu. Wakati huu pia alijaribiwa na Shetani na aliyashinda
majaribu yote kwa kuwa mtiifu kwa Baba yake. Alikubali hali hiyo ili kuonyesha
jinsi ya kushinda mtego wa mshawishi. Majaribu ya mali, nguvu na utukufu yaliyokabiliwa
na Yesu hayakumvuruga kutoka kufanya mapenzi ya Mungu.
Katika sehemu
ya pili ya injili tuna muhtasari wa mwanzo wa kazi ya Yesu na tangazo la Ufalme
wa Mungu na mwaliko kwa ubadilifu. Uwepo wa Yesu unaleta Ufalme wa Mungu, kuanzisha
wakati mpya, wakati wa wokovu. Hiyo ni habari njema ambayo ilitarajiwa kwa
wote. Ili kuamini habari njema iliyotangazwa na Yesu, ubadilifu ni muhimu. Moyo
ni kitovu cha maamuzi na ubadilifu unatokea moyoni, kwa hivyo imani ya kweli
katika Yesu inawezekana kama moyo unabadilishwa.
Katika uzoefu
wake jangwani, Yesu aliongozwa na Roho, akasaidiwa na Malaika na akawa makini
sana kuhusu mpango wa Mungu. Kwa hivyo hakuna kilichomvuruga kutoka muhimu
zaidi. Kama wafuasi wa Yesu, mara kwa mara sisi hushawishiwa kuacha kwa sababu
ni mpango wa mshawishi. Lakini mfano wa uaminifu wa Mwalimu Yesu ni mwaliko
kwetu tujiruhusu kuongozwa na Roho Mtakatifu, kusaidiwa na wengine na kuwa na
malengo ya wazi sana maishani mwetu ili kutambua vizuri katika kila kitu.
Majaribu zaidi ya kawaida katika jumuiya zetu ni kufikiri kwamba kuna watu wa
kutosha kutumikia au kutumia baadhi ya majukumo ili kutawala na kuwafedhehesha
wengine. Kwaresima hii itusaidie katika safari yetu ya ubadilifu, kutuhamasisha
kukaa kwa umakini katika muhimu zaidi - kama Yesu kuhusu mpango wa Mungu - ili
kushinda majaribu kufuata njia zingine.
Fr. Ndega
Mapitio: Mwalimu Patrick
Nenhum comentário:
Postar um comentário