Kutafakari kutoka Is 40, 1-5, 9-11; 2Pt 3, 8-14, Mk 1, 1-8
Mandiko haya yanatualika kuandaa njia kwa
Bwana kupitia kwa safari ya
ubadilifu, kutangaza na maisha
yetu habari njema za wokovu wa
Mungu. Kwa hivyo tunaalikwa
kufanya uzoefu kwa bidii wa Neno
la Mungu ili kuwa mashahidi wake
kama ilivyotokea na manabii, wajumbe waaminifu wa Mungu.
Nabii Isaya anazungumza kwa watu waliokuwa wakiteseka
uhamishoni wa Babeli, kutangaza wakati mpya, wakati wa ukombozi. Hali katika Babeli na
ukombozi baadaye ilichukuliwa
kutoka kupya. Lengo la ujumbe wa nabii ni kuwapa
faraja na matumaini kwa watu,
kuwahamasisha kuanza safari ya ubadilifu ili kuandaa
njia kwa hatua ya Bwana,
kukaribisha upendo wa huruma na kupitia
maisha mapya. Katika somo la pili, maneno ya Petro ni ushauri kwa watu kusubiri
kuja kwa Bwana kuwa macho, kutoa bora wenyewe kwa manufaa ya jumuiya. Kulingana na Petro, Mungu ni subira na huruma. Yeye hataki mtu
yeyote kuharibiwa, lakini
kusubiri kwa ubadilifu wa wote ili kuwaokoa.
Ujumbe wa nabii Isaya na maneno ya motisha ya Petro
yanaandaa mioyo ya watu kwa hatua ya Bwana. Hawaongei
kuhusu mawazo yao, lakini kile
ambacho Mungu amewaongoza kusema. Uaminifu kwa Neno la Mungu linaloishiwa katika njia ya mzizi akawapa uhakika kwamba wanasema ukweli.
Mtu yeyote ambaye anasema katika jina la
Bwana, anafikiria mwenyewe na uwezo wa kutafsiri matukio, kusaidia watu kutembea mbele
ya Bwana, kubaki waaminifu kwa mipango
yake. Kama ilivyotokea kwa Isaya
na Petro, ni mwaliko kwa
sisi kukaa makini ili kukubali, kuweka ndani na kushuhudia rufaa kutoka kwa Neno la Mungu.
Marko ni mwinjilisti tu ambaye anaingiza injili yake
kutumia maneno haya Habari njema wakati anaongea
kuhusu Yesu. Katika andiko hili, anatualika kutafakari
kuhusu Yohana Mbatizaji, nabii mkuu, kulingana na Yesu. Yohana anatolewa kama mfano kwa wote kwa sababu alitumia nguvu yake yote ili wokovu
wa Mungu unadhihirishwa kwa Yesu Kristu
lazima kukaribishwa na watu. Katika ujumbe wake, Yohana anatangaza huruma ya Mungu: “Badilisha kwa Bwana! Mungu atawasamehe dhambi zenu.” Hivyo, Yohana ni nabii wa Ubadilifu.
Badala ya maneno haya, Yohana anafanya pia
ishara halisi ya mwaliko kwa watu, kufufua matumaini
yao katika huruma ya Mungu. Yohana
aliishi katika upweke wa jangwa na alifunguliwa kabisa kwa msukumo wa Mungu. Katika
mahali hapo alijifunza kutoka kwa Neno
la Mungu, jinsi ya kushuhudia habari
njema za wokovu. Ukuu wa Yohana ulikuwa
kutambua ukuu wa Bwana,
kuzingatia mwenyewe kama sauti tu ambaye huandaa
njia ya aliyekuwa akuje.
Sababu ya uaminifu wa ujumbe wa Yohana
ulikuwa si maneno yake tu, lakini
unyenyekevu wake na roho ya sadaka,
usemi wa maisha inayoishiwa kwa nguvu.
Kwa hivyo watu walihisi
kuvutiwa na walikubali
pendekezo la ubadilifu. Ilibaki
kama changamoto kwa sisi sote
tunaoitwa kutangaza habari njema ya wokovu kupitia ya ushuhuda wa maisha zaidi kuliko kwa maneno. Ili ushuhuda
wetu lazima kweli kama huo wa Yohana, ni muhimu kwamba uzoefu
wa Neno la Mungu hukuwe uhai ndani yetu. Bidii zaidi ni uzoefu huu ufanisi
zaidi utakuwa ushuhuda. Kama hii
ubadilifu unatokea, kutuezesha kumwonyeshea Bwana makaribisho
ambayo Anastahili.
Fr. Ndega
Mapitio: Rose Mong'are
Nenhum comentário:
Postar um comentário