quarta-feira, 21 de janeiro de 2015

WITO KAMA UZOEFU WA UPENDO




Kutafakari kutoka Sam 3: 3-10; 1Wak 6: 13c-15a.17-20; Yoh 1,35-42

Liturujia ya Jumapili hii inathibitisha kwamba Mungu anaanzisha uhusiano wa upendo na kila mtu, kumwita kwa huduma ya watu wake. Mungu ndiye anayeanza kumwita mtu kwa jina lake mwenyewe, kuthamini historia yake na utambulisho wake. Ingawa Mungu anaweza kufanya kila kitu peke yake, alitaka kututumia kama washirika wake. Hali halisi hii ilihamasisha Mtakatifu Agostina kusema: “Mungu alituumba bila sisi, lakini akataka kutuokoa na ushiriki wetu”. 

Wito wa Samueli, unaosimuliwa katika somo la kwanza, ni mfano kwa wito wote. Mungu anakutana naye katika hali halisi yake na anamwita kwa jina lake. Bila shaka Samueli alihitaji mwendo wa utambuzi ili kufahamu tamani ya Mungu. Kuhani mkuu Eli alikuwa patanishi wa Mungu kusaidia Samueli kutambua sauti ya Mungu na kujibu kwa rufaa zake. Vivyo hivyo, tunahitaji kuwa uangalifu sana kutambua sauti ya Mungu kati ya sauti nyingi ambazo sisi husikia. Katika mwendo huu tumekuwa kusaidiwa na watu wengi na hali halisi nyingi. Kama Eli, tunaalikwa kupatikana kusaidia wengine kugundua mapenzi ya Mungu kwa wao. Kama Samueli, tunahitaji kuwa makini kwa mwito wa Bwana na kuwa ukarimu katika majibu yetu kwa mavutio yake. Tuongozwe na Neno la Mungu na tunaungwa mkono na usaidizi wa wengine, majibu yetu kwa Mungu lazima yawe daima ndiyo. 

Kulingana na Mtakatifu Paulo, wito wetu ni kuwa sehemu ya mwili wa kristu kama hekalu hai la Mungu. Kwa njia ya ubatizo Mungu ametufanya makao yake pekee. Hiyo ni kauli ya Mtakatifu Paulo katika waraka wake: “Ninyi ni hekalu la Mungu na Roho wake anakaa ndani yenu.” Basi, kama sehemu za mwili wa Kristu, utambulisho wetu ni kuwa kanisa kwa njia ya ushirika na ushirikiano. Ushuhuda wa maisha na heshima kwa mwili wetu inachangia kwa kuendeleza kujenga kwa Hekalu hili takatifu ambalo ni sisi sote. Hatuezi kubadili mwili wetu katika chanzo ya radhi na dhambi. Kila kitu ambacho sisi hufanya kuhusu mwili wetu lazima kiwe kwa utukufu wa Mungu. Ingawa utunzaji kuhusu uzuri wa nje wa mwili ni mzuri, hauwezi kutuzuia kuchukua huduma maalum ya hekalu hai la Mungu ndani yetu.
 
Injili inaongea kuhusu wito wa wafuasi wa kwanza wa Yesu na watu na hali zilizotumiwa na Mungu kama  mapatanishi kuwadhihirishia binadamu mafunbo yake. Ni mwendelezo wa andiko la ubatizo ambalo Baba anatoa ushuhuda kumhusu Mwana wake, alithibitisha ujumbe wake kama Mwokozi na kuwaalika wote kuyafuata maneno yake. Katika andiko la leo, Yohana anatambua Yesu ambaye anapita na anamwonyeshea kidole kama “Mwana-kondoo wa Mungu, aondoaye dhambi za dunia”. Ushuhuda wa Yohana unamotisha wengine kumfuata Yesu. Yohana ni mfano mzuri wa mpatanishi, anayekuza mkutano na anatoweka kwa unyenyekevu. Uzoefu wa “Njoni nanyi mtaona” ulioazimiwa na Yesu ulibadilisha maisha ya wanafunzi wa kwanza, kuwafanya mashahidi wapya wake ili kumotisha wengine katika uanafunzi. Wanafunzi wa kwanza walikuwa makini sana na upatanishi wa Mungu, basi wanajiruhusu kuongozwa, kuonyesha upatikanaji kumfuata Mwalimu Mkuu na kubaki naye, kufananisha hali yake ya maisha ili kuwa mashahidi.

Safari yetu ya wito ni historia ya upendo na inaweza kulinganishwa na wito wa Samweli na wanafunzi wa kwanza wa Yesu. Kila siku Mungu anamsha masikio yetu ili yasikie maneno yake na basi sisi wenyewe kugeuzwe nayo. Anaendelea kuzungumza nasi pia kupitia watu na hali ya jumuyia. Anatarajia kwamba tuweze kuwa makini kwa ishara hizi na kujibu mavutio yake kikamilifu. Kama Eli na Yohana Mbatizaji, tunaalikwa pia kuchangia katika kazi ya wito ili watu wengine, hasa vijana, waweze kugundua sauti ya Mungu ambayo inawaita katika maisha yao ya kila siku. tweze kuishi wito wetu kwa furaha na uaminifu, kuwamotisha wengine katika safari yao kama wafuasi wa Yesu.


Fr. Ndega
Mapitio: Mwalimu Patrick

Nenhum comentário: