Kutafakari kuhusu Mw 2: 18-24 Mk 10: 2-16
Yesu
alikuwa akiwafundisha watu kama ilivyokuwa desturi yake. Ghafla baadhi ya
Mafarisayo walimwendea wakimjaribu. Jambo lilikuwa kuhusu talaka likidhihirisha
mtazamo wao kuhusu ndoa na familia. Yesu alisahihisha mtazamo huo,
akiwakumbusha mpango wa kiasili wa Mungu kwa mwanamume na mwanamke ambao
tumesoma katika somo la kwanza.
Baadaye
alipoingia nyumbani aliendelea kuongea na wanafunzi wake kwa kina kuhusu uzinzi
akiuweka kwa uhusiano na talaka. Hatimaye, alionyesha tabia ya upendo kwa
watoto wadogo walio waathirika wa tabia mbaya ya wazima wazima katika ndoa na
familia. Yesu anajitambulisha na watoto anawakumbatia anawabariki anawalinda na
kuwaweka kama mfano na kipimo ili kumkaribisha na kuingia katika ufalme wake.
Hao wanastahili kuheshimiwa na kuthaminiwa ili waweze kukua kwa usalama na
furaha.
Baadhi
ya Mafarisayo wanatumia sheria ya Musa kumjaribu Yesu. Kulingana na mawazo yao,
Sheria hiyo inaruhusu talaka, lakini Yesu anaikataa hayo kwa sababu sio mpango
wa Mungu na tena hali ya mwanamke ilikuwa ngumu sana kwa sababu daima alionewa
na daima alitegemea huruma tu ya mwanamume. Kulingana na Kitabu cha Kumbukumbu
la Sheria, sura 24, mwanamume aliweza kumpatia mkewe talaka ikiwa hakupendezwa
naye “kwa sababu ameona kwake kitu kisichofaa”. Mwanamke alikuwa na nafasi
chache za kutoa talaka kwa mmewe, mfano mwanamume akiugua ukoma. Mbele ya hayo Yesu
aliwasaidia kufikiri vizuri kwa sababu Sheria zimewekwa kwa manufaa ya watu na
si watu kwa ajili ya sheria.
Kulingana
na mpango wa Mungu uliofunuliwa na Yesu, wote mwanamume na mwanamke wameumbwa
kwa sura na mfano wa Mungu naye ameweka ndani yao upendo unaowafanya
watamaniane na hatimaye kuwaacha wazazi wao, kuungana na kuwa mwili mmoja.
Jambo hili linaonyesha kuwa mme hana haki ya kuamua atakavyo kwa mkewe, mfano
kumwacha mke wake kwa muda wowote anaotaka.
Umoja
wao ni mtakatifu naye Mungu mwenyewe akiutaka na kuuweka. Mwendeleo ama
kupasuka kwa umoja huu haupatikani kwa hukumu ya kibinadamu. Inamaanisha kuwa
hawawezi kuachana au kutenganishwa. Lengo kuu la Yesu, ni kweka tena hali ya
ndoa isio na mwisho na hivyo kukarabati nafasi ya mwanamke kwa uhusiano na mmewe
uliyoharibiwa na sheria. Kulingana na Yesu Mwanamke ana haki kama mwanamume naye
anastahili kuheshimiwa kama sura na mfano wa Mungu. Nia ya Mungu ni kuwa mume
na mke waendelee kukua katika upendo na kupata uzima wa milele.
Tamani
ya kibinadamu ya kupenda na kupendwa ni maana ya uzoefu wa ndoa na wa familia.
Familia ni msingi wa uzoefu wa kibinadamu na yoyote ambayo ni dhidi ya kanuni
hii ni marufuku katika biblia. Kwa hiyo “Usizini” ni moja miongoni mwa Amri
Kumi. Kwa nini uzinzi hutishia familia? Uzinzi unaweza kuharibu familia kwa
sababu pamoja na uwezekano wa kusababisha ujauzito na kuzaliwa kwa mtoto bila
mpango kuna pia madhara ya kutisha kwa ndoa, kama hisia ya usaliti na upotevu
wa itibari. Kwa kifupi uzinzi unamaanisha maisha ya ulaghai.
Maana
ya Amri “Usizini” ni ulinzi wa familia. Kwa nini familia ni muhimu sana? Kwa
sababu pasipo familia uimara wa jamii hauwezekani; tena kwa sababu bila familia
mawasiliano ya thamani ya jamii kizazi kwa kizazi hayawezekani. Zaidi ya hayo
uhusiano kati ya wazazi na watoto unawafanya kuwajibika na kukomaa zaidi. Familia
inayaridhisha mahitaji ya hisia na fizikia/mwili, kuwapa watoto utoto salama na
imara. Yesu alijitambulisha na watoto na kuwajulisha kama mfano wa kukaribisha
mafundisho yake ili tuweze kuingia katika ufalme wake na kupata furaha kubwa. Kwa
upendo na wema mkubwa alikubali kuwa mmoja wetu na kuishi hali ya familia
akituletea furaha kubwa vile vile tunaalikwa kupendana sisi kwa sisi na kupatikana
kwa kutumikia wanaoishi pamoja nasi ili tuone furaha kubwa na kupata kushiriki
katika furaha yake kamili. Familia zetu iweze kukuta njia kamili ya kuishi
vizuri kwa kutambua haja ya kuishi kwa uaminifu. “Bila uaminifu hakuna furaha.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário