Mada
kuu ya tafakari hii ni Hekima. Asili yake ni Mungu naye ilijifanya kuonekana
katika nafsi ya Yesu Kristo, ambaye alijitambulisha kama "Mkate ulioshuka
kutoka mbinguni", yaani Hekima ya Mungu iliyofanyika mwili katika hali ya
kibinadamu. Kwa maana hii, mtu mwenye hekima kweli ni mtu tu ambaye anashikilia
kabisa mafundisho ya Yesu Kristo, kipimo cha furaha kamili.
Somo la
kitabu cha Hekima, kwa sambamba na Injili, inaleta ushuhuda wa Sulemani, ambaye
alichagua hekima badala ya nguvu na utajiri. Hekima haiwezi kulinganishwa na
kitu chochote kilichopo hapa duniani. Ni zawadi kutoka Juu na hupewa kwa mtu
yeyote anayeitafuta na kuipendelea kuliko vitu vingine. Tunapaswa kuiomba kwa
unyenyekevu na uvumilivu, tukijua kuwa ni nia ya Mungu mwenyewe kutuipatia ili
tuweze kufanya uchaguzi kulingana na mapenzi yake, kama vile Sulemani mwenyewe
alivyofanya.
Kifungu
kutoka kwa Waraka kwa Waebrania ni wimbo kwa Neno la Mungu. Hili ni hai na wenye
ufanisi na kwa sababu hii, ina uwezo wa kuingia ndani yetu kwa kina,
ikituwezesha kufanya kila kazi njema. Uwezo wa kupambanua unatoka kwa Neno kwa
sababu hili ni chanzo cha hekima. Tunapolikaribisha vizuri na kuruhusu tendo
lake maishani mwetu, hubadilisha moyo wetu wa jiwe pole pole, kuufanya uwe na hisia
na upatikanaji kwa mapendekezo ya kimungu.
Wakati
wa maisha ya Yesu ya umma, watu wengi walimjia, wakiruhusu kuguswa na
kubadilishwa na neno lake. Mara kadhaa, Yesu aliweza kuhisi furaha na kuridhika
kwa matokeo mazuri ya “kampeni” yake ya wito. Lakini kwa mtu huyo anayeonekana
katika Injili ya leo, hali ilikuwa tofauti kabisa, kwa sababu, ingawa alikuwa
na hamu ya uzima wa milele ndani yake, moyo wake ulikuwa umefungwa na kuhusishwa
na shughuli nyingi. Kwa kweli, mtu huyo alikuwa na bidii, alipatikana, alifuata
amri za zamani, lakini aliishi bila maana sana, kwa sababu maisha yake yalilenga
tu kutimiza sheria na kuwa na mali.
Yesu alimwona
kwa upendo, kama anavyofanya mtu ambaye anataka kukabidhi mtu mwingine kitu cha
maana sana kwa sababu anajua kuwa mtu mwingine huyo ana uwezo wa kuchukua ahadi.
Mwaliko wa kumfuata Yesu, basi, unatokana na mtazamo wa upendo ambao unaingia
ndani kwa kina, unamvutia mtu na kumtongoza. Mtazamo huu unafikiria muhimu uzoefu
wa imani, kupitia amri na pia unapanua upeo wa macho kupitia pendekezo jipya la
maisha, ambalo halitegemei kuheshimu sheria au ukali wake, bali kujinyima na
kushiriki mali. Kwa maneno mengine, Yesu anatualika tumfuate kwa busara.
Mabadiliko
ya kweli lazima pia yatekelezwe kwetu, kwani Neno ambalo kwa kawaida Yesu
anatuelekeza huleta pendekezo ambalo husababisha mapasuko kadhaa. Ikiwa
tunamfuata Yesu, tuyakatae mawazo ya ukusanyaj ama tubaki kwa mawazo hayo na kumkataa
Yesu. Mtu hawezi kuchagua Yesu na kuendelea vivyo hivyo, kwa mfano, kuendelea na
tabia sawasawa mbele ya mali kama mwanzo. Bila mabadiliko ya mawazo hakuna kumfuata
Yesu wa kweli.
Kwa
kawaida tuko na ngumu ya kuchagua vizuri kwa sababu tunafikiria sana juu ya
kile tunachopaswa kuacha ama kukataa. Mtu wa injili alifanya chaguo mbaya sana
maishani mwake kwa sababu hakutaka kukataa. "Sisi pia tusifanye makosa
yale yale kwa sababu wakati Bwana anatupa jukumu kubwa hivyo ni kwa sababu,
kwanza, alitufikia na muonekano umejaa upendo, akitupatia msaada kwa jibu
kulingana na matarajio yake". Na hii inatutosha.
Mbele
ya mazingira ambayo yajionyesha yamejaa mapendekezo ya kuvutia ni lazima hekima
nyingi na ujasiri wa kinabii kwa kuchukua ahadi muhimu kama ile ambayo Yesu
anatualika leo. Nayo haijahifadhiwa kwa wengine tu... Kila mtu ameitwa kuishi
njia ya maisha ya unyenyekevu na kujinyima, akiweka tumaini lake kwa Mungu
zaidi kuliko vitu alivyo navyo. Kujitolea kwa utumishi wa kindugu na kushiriki
mali alizo nazo kwa walio na shida kunaonyesha kwamba tunaelewa kuwa uzima wa
milele unaanza hapa duniani, na kutufanya tupate furaha iliyozidishwa katika
kila tendo mema kwa ajili ya wengine.
Tujiruhusu
kupendwa na Bwana na kukubali pendekezo lake ambalo linatuhakikishia uhuru wa
kweli, masharti ya kimsingi ya kupata uzima wa milele ambayo unaanza tunapoamua
kumwamini na kumfuata. Atupatie hekima yake ili tuweze kuwa na tabia kamili
mbele ya mali na kuchukua wito wetu kama wanafunzi kwa upatikanaji kabisa kwa
kumtumikia yeye kwa nafsi ya ndugu na dada zetu.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário