Mostrando postagens com marcador UFALME. Mostrar todas as postagens
Mostrando postagens com marcador UFALME. Mostrar todas as postagens

quarta-feira, 25 de novembro de 2015

UFALME WA YESU NI TOFAUTI KABISA


Kutafakari kuhusu Yoh 18, 33-37

            Tunasherehekea sikuku ya Bwana Wetu Yesu Kristu Mfalme. Yeye ni Mfalme wa mbingu na dunia; enzi na utawala wote ni wake. Liturjia hii inatualika kumfuata Mfalme huyo ambaye ni njia, ukweli na uzima. Kuutafuta kwanza ufalme wake ni maana ya kweli ya maisha yetu.

Mbele ya Pilato, Yesu hakukanusha juu ya ufalme wake,  bali anafafanua zaidi maana ya ufalme huo. Swali la Pilato kwa Yesu ya kwamba: “Wewe ni Mfalme wa Wayahudi?”, lilikuwa limewaza kuwa Yesu alikuwa mmoja wa wazalendo ambaye alitaka kuupindua utawala wa Roma na kuanzisha utawala mpya wa kisiasa kwa wayahudi. Wayahudi wengine walitumaini kuwa Masiha angewarudishia tena utawala wa Daudi. Wote, Pilato na Wayahudi, wana wazo ambalo sio kamili kuhusu ufalme wa mbinguni na kuhusu pia Yule aliyechaguliwa na Mungu adhihirishe ufalme huu. Yesu anakubali kuwa yeye ni mfalme, lakini siyo mfalme wa wayahudi tu. Yeye ni Mfalme wa wote na Ufalme wake ni tofauti. Kumbe ufalme wa Yesu si wa dunia hii lakini unawahusu wote waishio hapa duniani.

      Ufalme ni mapenzi ya Mungu ambayo Yesu aliishi na ufalme huu ni pia hali mpya aliyoanzisha ulimwenguni. Uwepo wake unaanzisha wakati mpya, yaani, wakati wa wokovu wa Mungu. Msingi wa ujumbe wa Yesu ni tangazo la wokovu wa Mungu ambalo ni sawa na tangazo la ufalme pia. Kwa kweli Yesu hajitangazi mwenyewe, bali anautangaza Ufalme. Katika Yesu mwenywe ufalme ulikuwa hali halisi ukisababisha mabadiliko ulimwenguni kwa wema wa wote hasa kwa walio na mahitaji mengi, yaani, wagonjwa wanapona, bubu wanaongea tena, vipofu wanapata kuona tena, maskini wanaipokea habari njema na wenye dhambi wanaondolewa dhambi zao. Kuna wengi ambao wanalitambua tendo la wokovu wa Mungu katika ishara za ukombozi za Yesu na wanajiruhusu kubadilishwa, lakini kuna wengine pia ambao wanajifunga wenyewe na hawawezi kutambua kile ambacho kinatokea kandokando yao. Upinzani dhidi ya Yesu ni upinzani dhidi ya mafanikio ya Ufalme wa Mungu. Katika maana hii ni ngumu sana kumfuata nyayo zake na kutangaza ufalme wake.

        Sio kwa Pilato tu, bali kwa wengine pia ilikuwa ngumu kufahamu kwamba Ufalme wa Yesu ni tofauti na wa dunia hii. Ufalme wake ni wa kuushuhudia ukweli na kuwaongoza watu katika njia ya kweli. Ufalme ambao Yesu anatangaza upo ndani yake na unaonyeshwa kupitia matendo yake miongoni mwa watu. Yesu hakufasili Ufalme lakini aliuonyesha upo ulimwenguni kupitia ishara nyingi. Hii si hali kwa kutazama bali kwa kuhisi na kutangaza. Hili ni fumbo la imani. Ingawa hatuna ufafanuzi kuhusu ufalme kutokana na injili, ibada ya Ekaristi ya siku hii inatujulisha baadhi ya thamani ambazo zina uhusiano wa ndani na ufalme ambao Yesu alikuja kutangaza, yaani, “Huu ni ufalme wa milele na ulimwengu wote, ufalme wa kweli na uzima, ufalme wa utakatifu na wa neema, ufalme wa haki, mapendo na amani.”


        Ni lazima kuwa makini sana kwa ishara za ufalme huu, kwa sababu, ingawa ufalme huu ni hali inayochanganyika na hali za binadamu, zipo ishara nyingi zinazoonekana kuwa wa Ufalme wa Mungu, lakini zinaweza kutudanganya. Yesu ni ishara ya ufalme kwa namna ya ajabu. Hatuhitaji nyingine. Msingi wa ufalme wa Yesu ni ushuhuda katika kweli unaoweza kubadili maisha ya watu, ikiwa tumkubali. Tunapomkubali Yesu na kumsikiliza na kisha kumruhusu awe kiongozi wa maisha yetu, tutakuwa tukiishi katika kweli. Kila aliye wa hiyo kweli humsikia sauti ya Yesu anayesema kuamba ndiye njia, ukweli na uzima. Ukweli huu utawapeni uhuru. Ufalme wa Yesu hupingana na uongo, uonevu na ukandamizaji na kila namna. Ufalme wa Yesu hautokani na nguvu au vita. Hivyo kila mmoja wetu ni budi aisikie sauti ya ukweli na kuamua kwa hiari yake kuifuata. Tuchukue pamoja na Mtakatifu Yohana Calabria ahadi ya kutafuta kwanza Ufalme wa Mungu kuiimarisha imani duniani katika Mungu Baba Mtoaji.

Fr Ndega
Mapitio: Sara

quinta-feira, 11 de junho de 2015

MUNGU ANAITOA NGUVU NA UHAI KWA VITU VYOTE


Kutafakari kutoka  Ezekieli 17: 22-24; 2Wakorinto 5: 6-10; Marko 4: 26-34

       Umuhimu wa liturujia hii ni uwepo kimya na ufanisi wa ufalme wa Mungu miongoni mwetu. Mungu anafanya kila kitu kwa wema wetu na anatarajia imani yetu kijumla katika kitendo chake. Somo la kwanza linaongea kuhusu hali ya utumwa wa Babeli katika mwaka wa 597 K.K. na linamzawadisha Ezekieli kama mmoja wa manabii aliyewaandama watu wa Israeli katika kipindi hiki kigumu. Watu hawakuwa na matarajio ya ukombozi, na Ezekieli aliwahamasisha kama mjumbe wa Mungu. Kulingana na nabii huyo, Mungu hakusahau watu; yeye yupo miongoni mwao na atawaokoa, akiwaletea maisha mapya na akiwafanya rejea kutangaza wema wake kwa mataifa yote. Katika mwendo huu wa ukombozi watu ni kama mmea mdogo utaokuwa mti mkubwa. Basi, Mungu atachukua watu wake waliodhulumiwa na walioaibishwa, atawainua kama chombo cha wokovu wake. Njia hii ya kutenda kwa Mungu inakumbukika katika wimbo wa Bikira Maria: “Bwana amewashusha wenye nguvu kutoka viti vyao vya enzi, na akawakweza wanyenyekevu”.

      Kulingana na Mtakatifu Paulo, sisi ni kama wageni, watu waliohamishwa ulimwenguni huu, mbali sana kutoka makao yetu penyewe. Sisi ni wa Mungu na hatuwezi kushikiliwa kwa ulimwengu huu, kwa sababu zawadi kuu ya imani tumepokea kutoka kwake inautoa mwelekeo kamili wa maisha yetu ili tufikie marudio salama katika Mungu mwenyewe. Zawadi ya imani inatuhamasisha kuchukua utambulisho wetu wa kikristu kwa uhusiano wa ndani na Kristu ambaye anatungojea ili kutuza kila mtu kulingana na chaguzi ambazo tumefanya katika dunia hii. Sisi sote tunaalikwa kwa maisha mapya yanayoweza kufikika kupitia neema ya wokovu wa Mungu katika Kristu na juhudi ya kufanya mema wakati tuko katika maisha haya.

        Katika injili Yesu anaongea kwa watu kutumia mifano ili kutueleza nguvu ya Ufame wa Mungu. Mfano wa kwanza ni kuhusu mbegu ambao unaota na unakua kwa nguvu wenyewe; ushirikiano wa binadamu ni kuutawanya tu, na kusubiri kwa mavuno ili kukusanya matunda. Wa pili ni kuhusu udogo wa kipimo cha mbegu ya haradali na ukuu wa matokeo yake. Kwa nini Yesu aliongea kwa watu akiitumia mifano? Chaguo la Yesu kwa njia hii ya lugha ni kwa sababu ya utambulisho wake na hali halisi ya watu wanyenyekevu na maana pia ni rahisi zaidi kwa ufahamu wao. Kama hii alifanya kufikika mafumbo makubwa ya Ufalme wa Mungu kwa wanyenyekevu. Hiyo ni njia iliochaguliwa na Mungu kutenda, akisababisha mchafuko kwa wenye uwezo na wenye nguvu, na akidhihirisha mafumbo yake kwa wanyenyekevu na maskini.

       Katika ujumbe wake, Yesu hakujitangaza; yeye aliutangaza Ufalme wa Mungu. Ufalme ni wa umuhimu katika ujumbe wake. Kulingana na Yesu, hali na nguvu ya Ufalme wa Mungu inategemea juhudi ya binadamu, bali kitendo cha neema ya Mungu inayotolewa bure. Kila mtu anaalikwa kufanya bora mwenyewe ili kushirikiana kwa ongezeko la Ufalme wa Mungu duniani, lakini aliyekabidhiwa kabisa katika kitendo cha Mungu. Kama hii alifanya Mt. Yohana Calabria, akitafuta kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake kupitia imani na kujisalimisha kabisa kwa riziki ya Mungu Baba. Huu ni umuhimu wa ujumbe wetu kama Poor Servants of Divine Providence.


       Watu wengi miongoni mwetu ni wakulima na mifano hii badala ya mafundisho kuhusu hali ya Ufalme wa Mungu, ni hamasa pia ili waendelee shughuli yao ya kila siku kwa uvumilivu na imani katika kitendo ya Mungu. Mifano hii anatualika kuangalia mwendo wa ongezeko la mashamba katika uwanja, hasa kuhusu mahindi na maharagwe. Sisi sote tunajua kwamba baada ya kazi ya kwanza ya kupanda tunategemea mvua na nguvu ndani ya mbegu. Hiki ni kitendo cha Mungu anayethamini juhudi ya binadamu kama ushiriki katika uumbaji na anatubariki kwa mavuno mengi. Tumshukuru Mungu kwa nguvu ambayo anatupa ili kufanya kazi kwa uaminifu na aendelee kutupatia Baraka zake kwa manufaa ya familia zetu. 

Fr Ndega
Mapitio: Sara