Mostrando postagens com marcador NENO. Mostrar todas as postagens
Mostrando postagens com marcador NENO. Mostrar todas as postagens

domingo, 21 de fevereiro de 2016

“HUYU NI MWANANGU MPENDWA, MSIKILIZENI”


Kutafakari kuhusu Lk 9, 28b-36

Tukio la kugeuka sura kwa Yesu kulitokea baada ya siku sita ya ufunuo kuhusu mateso, kufa na kufufuka kwake na mwaliko wake kwa wanafunzi wa kumfuata kulingana na njia yake mwenyewe, yaani “Kujikana mwenyewe, kuuchukua msalaba wake na kumfuata Yesu.” Habari ya kugeuka sura kwa Yesu tena inafuatwa na tangazo la pili kuhusu kifo na ufufuko wake. Kwa uzoefu huu Yesu aliwachukua wanafunzi watatu, Petro, Yakobo na Yohana. Kwa nini wafuasi hawa? Labda kwa sababu aliwapendelea kuliko wengine. Injili haiongei maana ya habari hii. Yesu aligeuka mbele ya wafuasi wake na ishara kuu zilikuwa nguo na mwili wake. Yesu aliwaonyesha kidogo utukufu wake na hali ya wakati ujao kuhusu mwili wa yeyote anayemfuata kwa uaminifu. Yesu anashiriki utukufu wake na wanafunzi wake kwa maana inampendeza kufanya hivyo ili wawe na furaha moja ya vile Mwalimu wao alivyo.

Kama illivyotokea kuhusu jangwa, Mlima pia ni mahali muhimu katika uhusiano wa Watu wa Israeli na Mungu; katika mwendo huu, Musa na Eliya wana ushiriki maalum. Katika Agano la Kale milima iliyojulikana sana ni Mlima Sinai na Horebu. Ilikuwa katika Mlima Sinai ambapo Mungu alikutana na Musa na kuwawekea Waisraeli mkataba/agano. Ilikuwa katika Mlima Horebu ambapo Eliya alijiandaa kwa muda mrefu akutane na Mungu. Katika Agano Jipya Yesu alitumia sana mahali huko mlima kama rejeo ya uhusiano wake na Baba na kama eneo kwa matukio muhimu katika kazi yake. Kulingana na utamaduni mmoja wa zamani, tukio la injili ya siku ya leo lilitokea juu ya milima Tabor.   

       Uwepo wa Musa na Eliya unaongea kuhusu rejea ya ufunuo katika Agano la Kale. Waliongea na Yesu wakionyesha kwamba hakuna mpasuko/mshipa kati ya mafundisho yao na mafundisho ya Yesu, bali uhusiano na mwendelezo. Lakini kulingana na sauti iliyosikika kutoka kwenye wingu, mwendelezo huu, ambao ni Yesu, lazima kuwa kipaumbele katika maisha ya wanafunzi kwa sababu ni Yesu peke yake kwa mamlaka aliyoyapokea kutoka kwa Baba ili kufundisha na kutafsiri kamili lile lililosemwa na mababu wa zamani.  Kusikiliza katika Biblia ni kitenzi chenye nguvu sana. Hii ni tabia ya myahudi mbele ya Neno la Mungu, akiweka vitendoni au kufanya mazoezi/vitendo kuhusu yale aliyosikia. Kusikiliza kuna uhusiano na kushika au kutenda. Baba anashuhudia kuhusu Mwana wake, anamweka kama rejeo cha maisha yetu: “Huyu ni Mwanangu mpendwa, msikilizeni”. Huu ni pia mwaliko ili tufananishe maisha yetu kulingana na Neno la Yesu. Neno la Yesu ni kipimo ili mtu awe pia mwana mpendwa wa Mungu kama Yeye. Tunashiriki katika kugeuka sura kwa Yesu kupitia kusikiliza makini kwa Neno lake.

     Kuhusu mambo hayo Mtakatifu Yohana Calabria alisema: sisi ni makini sana kwa maneno ya binadamu na kuhusu hiyo ni sawa. Lakini tunapaswa kuwa na uangalifu zaidi kwa Neno la Mungu ambalo ni – consecratory – huweka wakfu, ni kwamba, linalifanya lile linalosema.” Mtakatifu Yohane Calabria ilikuwa anasema hasa kuhusu injili ambayo ni sheria kwetu Poor Servants of Divine Providence. Katika sehemu nyingine ya maandiko yake alisema: “Ikiwa sisi huamini katika maneno ya kuapishwa kwa – consecration – katika misa, yaani “twaeni mle wote, twaeni mnywe wote”, tunapaswa kuamini pia wakati Yesu asema: “Msiwe na wasiwasi” au “Baba yeno wa mbinguni anajua kwamba mnahitaji vitu hivyo vyote” au “mtafuteni kwanza ufalme wa Mungu na matakwa yake, na hayo yote mtapewa kwa ziada.” katika maneno mengine, kutokana na Maneno ya Yesu tunaalikwa kuwa “Injili hai.” Hiki ni kipimo kwetu ili tuweze kumtambua uso uliogeukwa wa Yesu katika nyuso zenye mateso za ndugu wengi miongoni mwetu. Neema ya Mungu itusaidie kulisikiliza Neno lake kwa uangalifu na kutangaza habari njema ya siri ya Mwanae kama njia ya wokovu kwa ulimwengu wote.  

Fr Ndega

Mapitio: Sara  

terça-feira, 8 de dezembro de 2015

MATOKEO YA UZOEFU WA KWELI WA NENO LA MUNGU


Kutafakari kuhusu Bar 5, 1-9; Wafil 1: 3-6, 8-11; Lk 3, 1-6

      Liturujia ya jumapili hii inaendelea kutumwalika kumkaribisha Bwana anayekuja kutuletea wokovu. Tunapaswa kujiandaa vizuri ili tuweze kumpokee Masiya wakati wowote. Wakati wa Majilio unatusaidia kutambua kwamba kwa matayarisho kamili ni lazima mabadiliko ya moyo, kwa njia mpya kabisa.  Maneno ya nabii Baruku yalihamasisha watu utumwani Babeli yakitangaza ukombozi karibu. Baada ya mateso hayo yote wataweza kurudi nyumbani Yerusalemu kwa furaha kubwa kwa sababu Mungu aliwakumbuka na kuwaongoza katika mwangaza na utukufu wake. Huu ni mfano wa wokovu wetu katika Kristo. Paulo anatambua kwamba imani na ushirika wa Wafilipi ni uenezi wa injili waliyochukua kwa shauku na utayari. Kwa njia ya Kristo na injili yake wanaweza kuzaa mazao mazuri kwa utukufu na sifa ya Mungu.  

       Injili inaongelea Yohane Mbatizaji anayefikiwa na Neno la Mungu jangwani. Katika biblia jangwa ni mahali maalum kwa uzoefu wa Neno la Mungu. Katika mahali huko watu wengi walijibadilisha kuwa viongozi wenye nguvu kwa kuwaongoza Watu wa Mungu kulingana na mwongozo wake. Yohane Mbatizaji anafikiriwa kuwa nabii wa mwisho na mkuu wa manabii wote. Toleo la Luka linataja makuhani na viongozi wa kisiasa ili kuonyesha kwamba kupitia mjumbe wake, Mungu huingia katika maisha halisi ya watu kwa wakati fulani. Mungu haongei hewani bali hupitia katika matukio mazuri au mabaya  katika historia ya watu. Mungu alijifanya mmoja wetu na bado yuko nasi kwa namna mbali mbali. Kwa kiyo hakuna tukio lolote la historia lisilokuwa na maana. Kwa kuonyesha wito wa Yohane katika matukio ya wakati wake, Luka anaonyesha kwamba tukio kubwa liko karibu. Mungu anaingia katika historia kwa namna ya pekee na inabidi watu watayarishwe kumkaribisha Masiya aliyetarajiwa kwa muda mrefu.

Kuja kwake Yohane Mbatizaji kuna maana na kuufuata mpango wa Mungu ambaye ana wakati kamili kwa kila kitu. Neno lake linayabadilisha maisha ya Yohane katika chombo cha wokovu. Kama Yohane ni kiungo kati ya Agano la kale na Jipya, kazi yake inatangaza kwamba nyakati za Masiya ziko karibu kuanza. Yeye ni sauti tu ambayo inatayarisha njia za Bwana. Yohane aliwatayarisha watu kumpokea Masiya kwa ubatizo. Kupitia ishara hii alitangaza huruma ya Mungu iliyopatikana kwa kila mtu kwa sababu ni mpango wa Mungu kwamba wokovu wake ufikie wote. Basi ishara ya Yohane ilikuwa kielelezo cha kupita kutoka katika dhambi na mauti kwenda katika neema na maisha mapya ya Mungu. Kipengele muhimu katika tendo hili la Yohana ni kwamba aliwabatiza wale waliomhitaji Mungu na kutubu dhambi zao. Yohane na watu hao waliamini kwamba ni Mungu anayesamehe dhambi zao.

Ubatizo wa yohane ni tofauti na ubatizo wetu, lakini yote mbili ni nafasi ya kuishi maisha mapya. Kwa upande wetu maisha mapya ni zawadi ya Kristo na matokeo ya utume wake. Ubatizo wa kikristo, pamoja na maondoleo ya dhambi, unadhamini ushiriki katika uzima wa Mungu mwenyewe. Ubatizo ni wa kwanza katika sakramenti tatu za mwanzo ukifuatiwa na Kipaimara na Ekaristi. Ubatizo wetu ni alama ya nje ya kufa katika dhambi, na pia ni ishara ya ufufuko wa maisha mapya katika Kristo aliye mshindi dhidi ya dhambi na mauti. Yeye ni mwanga wa kweli ambao unamtia nuru kila mtu. Kupitia mwendo huu tumekuwa wana wa nuru ili tutembee katika nuru ya Mungu kila siku ya maisha yetu.


Kipindi cha Majilio kinatusaidia kujiandaa kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu. Wakati ulimwengu wa biashara unashauri watu wajiandae kwa Noeli kwa kununua vitu, kipindi cha Majilio kinatupendekezea matayarisho ya ndani kiroho, na hamu ya kutaka kutupatanishwa na Mungu na wenzetu. Kuna vikwazo vya kuondoa katika maisha yetu kwa msaada wa neema ya msamaha wa Mungu. Kwa hivyo tuchukue wakati mzuri huu kuadhimisha msamaha wa Mungu kwa sacramenti ya Upatanisho na kuishi kwa njia mpya uhusiano wetu na Mungu na wengine.


Fr Ndega
Mapitio: Sara