Mostrando postagens com marcador KUONA. Mostrar todas as postagens
Mostrando postagens com marcador KUONA. Mostrar todas as postagens

sábado, 27 de outubro de 2018

IMANI YETU INATUFANYA (INATUZUIA) KUONA NINI?


Kutafakari kutoka Yer 31,1-7; Wab 5,1-6; Mk 10, 46-52


     Kifungu cha Yeremia ni mwaliko wa furaha kwa sababu Bwana anapanga kutenda mambo ya ajabu katika maisha ya watu wake: hakika, kazi hii imekwisha anza. Yeye ndiye Baba amejaa upendo kwa ajili ya watu wake, hasa kwa ajili ya wadogo na wasio na nguvu miongoni mwetu. Yeye huvutia kwake kila anayeishi ili kufanya uzoefu wa wokovu wake kwa sababu “upole wake unafikia kila kiumbe.” Anatuambia leo: “Wewe ambaye husikiliza, wewe unayeteseka, wewe unayependa nawe unayesali, wewe ni mwanangu mpendwa, binti yangu mpendwa!” Mbele ya Mungu ambaye anatenda hivyo kwa ajili yetu, tabia yetu lazima kuwa ya amini kabisa, tukiacha nafasi kwa tendo la neema yake katika maisha yetu, yaani, kuruhusu Mungu awe Mungu ndani yetu.

       Kifungu cha waraka kwa Wayahudi kinaleta mfano wa kuhani ambaye amechaguliwa miongoni mwa watu na kufanya wakfu kwa manufaa yao. Yeye amevaa udhaifu na kwa hivyo anaweza kuhisi huruma kamili kwa ajili ya wanaokosa. Ukweli huu inamzungumzia Yesu Kristo, Kuhani wa kweli, ambaye “anakusanya katika nafsi yake udhaifu wa mtu na nguvu ya kufanya upya wa Aliye juu.” Yeye hakujitukuza nafsi yake kufanywa kuhani mkuu” bali ndiye Baba aliyemtukuza. Sisi pia tangu ubatizo wetu katika Kristo, tuko na heshima ya kikuhani iliyo huduma ya wokovu. Kwanza ya yote hii ni zawadi ya Mungu nasi mbele ya hali hii tunapaswa kujibu kwa uaminifu na furaha. Tunasaidiwa na neema yake na jumuiya ya imani ili tuweze kuishi wito wetu kama zawadi kwa ajili ya wengine.

        Kifungu cha injili anaongelea kuponywa kwa Bartimayo na, basi, ufunuo wa Yesu kama mwanga ambaye anatupa mtazamo mpya. Muujiza huu ulitokea wakati Yesu alikuwa anaondoka mji wa Yeriko, yaani, katika pembezoni. Yeriko ni mmoja miongoni mwa miji ya zamani ulimwenguni. Mji huu ni eneo la baadhi ya matukio makuu ya biblia; hata katika muda wa Musa iliongelewa kuhusu mji huu. Tukumbuke “kuzingirwa na kuchukuliwa kwa Yeriko” na Waisraeli katika wakati wa Yoshua (Yoshua 6, 1-27). Tukumbuke pia Zakayo; mabadiliko ya maisha yake yalitokea katika Yeriko. Mji huu ni karibu na mto Yordano na Yesu alipita mahali huko mara nyingi. Andiko la siku ya leo linaongea kuhusu mkutano wa Yesu na kipofu Bartimayo, aliyeketi kando ya barabara ya mji. Hakika alikwisha amesikia kuhusu Yesu na alitaka sana nafasi ya kukutana naye. Lakini hakujua kwamba Yesu pia alitaka kukutana naye ili kumwongozea njia mpya ya kuishi. Kisha, nafasi imefika! Shauku ya kipofu ilikuwa kubwa sana hata hakuna mtu aweze  kumnyamazisha.

        Kilio cha kipofu ni kilio cha kila binadamu ambaye anajua udhaifu wake mwenyewe na kuhusu mahitaji ya huruma ya Mungu. Kipofu ni ishara ya kivuo dhahiri cha ndugu zetu wengi walio waathirika wa udhalimu na kosa la usawa wa kijamii. Ni nafasi ya kutambua kwamba watu wengi wanaanguka au wameachwa barabarani ama katika mahusiano yetu. Wanapaza sauti kwa huruma na kwa nafasi kwa sababu wanaamini kwamba wale ambao wanajiona kuwa wafuasi wa Yesu wanaweza kusikiliza sauti yao na kuwatendea mema. Yesu alisikia si kilio cha kipofu tu, bali pia kilio cha wale ambao walimwambia kipofu “anyamaze”!, wakionyesha kutojali. Yesu analaumu kutojali kwa sababu kunaharibu undugu na kukana utambulisho wa mwanafunzi wa kweli.  

     Hakika jibu la Yesu linaonyesha mchanganyiko wa huruma na hasira, kwa sababu alikuwa akishughulika kwa upofu wa aina mbili tofauti, yaani, upofu wa Bartimayo na upofu wa umati wa watu ambao walikuwa wakimfuata Yesu bila ushirika na hisia zake. Je, ni nani ana upofu zaidi, yule aliye kipofu asili au wale ambao hawapati kuona walio na mahitaji kandokando yao? Hata hivyo kuna tumaini, kwa sababu miongoni mwa wale ambao walimwambia kipofu “nyamaze!” walikuwapo wengine ambao walimwambia “jipe moyo, anakuita! Yeye hajakusahau wala hawaachi wale ambao wanamwamini”. Sauti hizi ni za watu ambao wanachukua ujumbe wa kinabii na kupata kuwahamasisha waliokata tamaa. Ni ishara pia ya walio vyombo vya Mungu katika maisha ya yeyote anayetaka kugundua wito wake ili aweze kumjibu Mungu kulingana na matarajio yake.

     Yesu ambaye tunamfuata ni mwenye hisia sana. Ana macho na masikio yalio makini sana kwa hali halisi ya watu. Anatualika kuwa na hisia sawa naye. Mara nyingi sisi tu kama kipofu huyo, yaani, tunahitaji na kutarajia mkutano wa mabadiliko ya maisha ili kuona vizuri kile kinachotokea kandokando yetu na kumfuata Yesu ambaye analeta maana mpya kwa maisha yetu. Tena mara nyingi sisi ni kama wengine karibu na Yesu, lakini mbali sana na ndugu, waliofungwa kwa hali iliyo kandokando yetu na hata tunafikiri kwamba tuna mamlaka ya kuwaambia wengine: “mnyamaze”. Hapo tuko na kosa kubwa. Tunapaswa kuwa macho kwa baadhi ya uzoefu wa sala ambao unatufungua kwa Mungu lakini unatufunga kwa wengine. Ikiwa imani yetu haituongozi kukutana na wengine wala haitufanyi wenye huruma, mbele ya mateso na mahitaji yao, imani ni kipofu, ni udanganyifu na kuhitaji kupona. Mungu atupatie neema ya imani ya kweli na halisi.

Fr Ndega

sábado, 7 de abril de 2018

“HERI WALIOAMINI BILA KUONA”



Kutafakari kuhusu Matendo 5,12-16; Ufu 1,9-11a.12-13.17-19; Yoh 20,19-31


            Katika Jumapili hii Kanisa linawaalika waamini kutafakari juu ya jambo la huruma ya Mungu. Tunataka kujifunza kutoka kwa Kristo jinsi ya kuwa na huruma kwa wengine kama yeye alivyo kwa ajili ya Thomas aliye kutokuwepo katika jumuiya. Yesu mwenyewe, katika injili ya Mathayo anatuhakikishia: “Heri walio na huruma, maana watahurumiwa” (Mt 5:7). Kulingana na baba mtakatifu Francisco, “Yesu Kristo ni uso wa huruma ya Baba. Fumbo la imani ya Kikristo linaonekana kukuta awali yake katika neno hili (...) tunahitaji kutafakari fumbo la huruma. Hiyo ndiyo chemchemi ya furaha, utulivu na amani.”

Somo la kwanza linaongea kuhusu njia ya Wakristo wa kwanza ya kuishi kilicho kipimo cha utambulisho wa jumuiya za Kikristo za nyakati zote. Wakristo wa zamani walipata mafanikio katika safari yao kwa sababu ya vipimo vinne, yaani “mafundisho ya mitume, kuishi pamoja kindugu, kumega mkate na kusali.” Njia ya kuishi kama wamoja iliwavutia wengine wengi ambao walitambua katika matendo yao ya ajabu tendo la Bwana aliye Mfufuka. Hivyo,  kwa ushuhuda wao watu wengi walikutana na huruma ya Mungu. Katika somo la pili, Paulo anamtukuza Mungu kwa sababu ya huruma yake kwa ajili ya watu wake tulio sisi sote. Kwa ufufuko wa Kristo tulifanywa upya na kuitwa kwa tumaini hai na kuishi imani yetu kwa furaha na kwa ahadi mpaka tupate lengo la imani yetu, yaani wokovu.

Baada ya ukatili kwa Bwana wao, wanafunzi wa Yesu waliishi katika mazingira ya hofu. Hawakutaka kuwa na mwisho sawa wa mwalimu wao, lakini waliendelea wanakutana hata kwa siri. Mambo mengi ambayo walijifunza kutoka kwa Yesu yalikuwa maana ya utambulisho wao. Basi, ingawa walikuwa na hofu hawakuwa wasio na tumaini kwa sababu yule aliyewaita kumfuata aliwataka kama mashahidi wake. Akijua kwamba walihitaji msaada, Yesu aliwajia akiingia bila kufungua milango maana hakuna kitu ambacho kiweze kuweka mipaka kwa mwili wa Yesu Mfufuka. Hali hii mpya ya mwili wake ni tangazo la hali ijayo ya miili ya wafuasi wake walio waaminifu kwake. Yesu aliingia na kusimama katikati yao kwa sababu anataka kuwa rejeo maishani mwao. Yeye alikuja kuwasaidia kushinda hofu na mashaka mengi katika safari yanayowazuia kumshuhudia kwa kweli.

Matokeo ya kwanza ya uwepo wa Bwana Mfufuka kwa wanafunzi ni furaha, yakithibitisha kwamba kuwa mwanafunzi wa Yesu ni kuwa mwenye furaha. Furaha inaifungua milango ya moyo kwa kuzipokea zawadi zingine. Bwana Yesu anaipa jumuiya ya wanafunzi amani kama utambulisho na Bwana wao aliye pia “Nabii asiye na ukatili”. Ikiwa Bwana Mfufuka yu katikati ya uzoefu wa jumuiya, wana wa jumuiya hii wanakuwa vyombo vya amani. Pumzi ya Roho Mtakatifu ni ishara ya maisha mapya kwa ubinadamu uliofanyika upya kabisa kwa msalaba na ufufuko wa Kristo. Watu wapya wamekusanika kwa jina la Yesu na kwa msaada wa Roho Mtakatifu wanaitwa kuishi kwa ushirika na upatanisho na kuzisaidia zawadi hizi kwa wengine.

Thomas hakuwepo katika mkutano wakati Bwana Mfufuka alijionyesha akitoa zawadi zake. Hakika Thomas alipendelea uzoefu tofauti, yaani uzoefu wa “nje ya jumuiya.” Kipengele cha kwanza kuhusu Thomas ni kuhusu kutokuwepo kwa jumuiya. Mtu huyo ni mfano wa wale ambao wana ugumu wa kushiriki pamoja katika jumuiya. Kutokuwepo huko ni hatari kwa uzoefu wao wa imani wa kibinafsi na kunaweza kuweka vikwazo kwa imani ya wengine. Kwa upande mwingine, tunaweza kusema kwamba mfano wa Thomas unafanya jumuiya kushuhudia imani yake kwa kweli na kuaminika.  Haitoshi kusema “tumemwona Bwana!”. Bali ni lazima kumtambua na kumtangaza bila hofu kama “Bwana wangu na Mungu wangu!”. Kwa sababu ya Thomas, Yesu anatangaza maneno haya ya ajabu, yaani “Heri walioamini bila kuona.”

Kwa mitume Yesu anatupa zawadi ya imani na kumwomba tuishi imani hii pamoja na wengine, kwa kupendana na kusaidiana kama matokeo ya maisha mapya kutokana na ufufuko wa Bwana wao. Mtu ana ugumu wa kuamini ikiwa anaamini peke yake. Imani ya mtu ni matokeo ya uzoefu wa jumuiya ya Kanisa, kwa sababu imani ya Kanisa inaitangulia, inaizaa na kuiimarisha imani ya mtu huyo. Bila ushiriki kwa hamu katika Jumuiya ya Kanisa, tuko na ugumu wa kutambua ishara za uwepo wa Bwana Mfufuka miongoni mwetu na imani yetu inakuwa haba na tena ndiyo hatari kwa uzoefu wa wengine.

Andiko hili linatusaidia kutambua umuhimu wa kushiriki pamoja katika jumuiya. Bwana Mfufuka alitaka kujifunua kwetu kupitia msaada wa wengine. Tunapaswa kuwa macho kwa mwelekeo wa ubinafsi katika jamii ambao umeshawishi mahusiano yetu na kuuvuruga undugu wetu. Kwa njia ya ubinafsi maovu mengi yanatujia. Ni lazima kumchukua Yesu kama kipimo cha uzoefu wetu wa jumuiya nayo jumuiya inapaswa kuwa na nafasi muhimu katika maisha yetu ili tuweze kushinda hofu na kutokuwa na imani ili ushuhuda wetu uwe ufanisi katika hali iliyo kandokando yetu.

Fr Ndega