Kutafakari kuhusu Matendo 5,12-16; Ufu 1,9-11a.12-13.17-19; Yoh 20,19-31
Katika Jumapili hii Kanisa linawaalika
waamini kutafakari juu ya jambo la huruma ya Mungu. Tunataka kujifunza kutoka kwa
Kristo jinsi ya kuwa na huruma kwa wengine kama yeye alivyo kwa ajili ya Thomas
aliye kutokuwepo katika jumuiya. Yesu mwenyewe, katika injili ya Mathayo
anatuhakikishia: “Heri walio na huruma, maana watahurumiwa” (Mt 5:7). Kulingana
na baba mtakatifu Francisco, “Yesu Kristo ni uso wa huruma ya Baba. Fumbo la
imani ya Kikristo linaonekana kukuta awali yake katika neno hili (...) tunahitaji
kutafakari fumbo la huruma. Hiyo ndiyo chemchemi ya furaha, utulivu na amani.”
Somo la kwanza linaongea
kuhusu njia ya Wakristo wa kwanza ya kuishi kilicho kipimo cha utambulisho wa
jumuiya za Kikristo za nyakati zote. Wakristo wa zamani walipata mafanikio
katika safari yao kwa sababu ya vipimo vinne, yaani “mafundisho ya mitume,
kuishi pamoja kindugu, kumega mkate na kusali.” Njia ya kuishi kama wamoja iliwavutia
wengine wengi ambao walitambua katika matendo yao ya ajabu tendo la Bwana aliye
Mfufuka. Hivyo, kwa ushuhuda wao watu
wengi walikutana na huruma ya Mungu. Katika somo la pili, Paulo anamtukuza
Mungu kwa sababu ya huruma yake kwa ajili ya watu wake tulio sisi sote. Kwa
ufufuko wa Kristo tulifanywa upya na kuitwa kwa tumaini hai na kuishi imani
yetu kwa furaha na kwa ahadi mpaka tupate lengo la imani yetu, yaani wokovu.
Baada ya ukatili
kwa Bwana wao, wanafunzi wa Yesu waliishi katika mazingira ya hofu. Hawakutaka
kuwa na mwisho sawa wa mwalimu wao, lakini waliendelea wanakutana hata kwa
siri. Mambo mengi ambayo walijifunza kutoka kwa Yesu yalikuwa maana ya utambulisho
wao. Basi, ingawa walikuwa na hofu hawakuwa wasio na tumaini kwa sababu yule
aliyewaita kumfuata aliwataka kama mashahidi wake. Akijua kwamba walihitaji
msaada, Yesu aliwajia akiingia bila kufungua milango maana hakuna kitu ambacho
kiweze kuweka mipaka kwa mwili wa Yesu Mfufuka. Hali hii mpya ya mwili wake ni
tangazo la hali ijayo ya miili ya wafuasi wake walio waaminifu kwake. Yesu
aliingia na kusimama katikati yao kwa sababu anataka kuwa rejeo maishani mwao.
Yeye alikuja kuwasaidia kushinda hofu na mashaka mengi katika safari yanayowazuia
kumshuhudia kwa kweli.
Matokeo ya kwanza ya
uwepo wa Bwana Mfufuka kwa wanafunzi ni furaha, yakithibitisha kwamba kuwa mwanafunzi
wa Yesu ni kuwa mwenye furaha. Furaha inaifungua milango ya moyo kwa kuzipokea
zawadi zingine. Bwana Yesu anaipa jumuiya ya wanafunzi amani kama utambulisho
na Bwana wao aliye pia “Nabii asiye na ukatili”. Ikiwa Bwana Mfufuka yu
katikati ya uzoefu wa jumuiya, wana wa jumuiya hii wanakuwa vyombo vya amani. Pumzi
ya Roho Mtakatifu ni ishara ya maisha mapya kwa ubinadamu uliofanyika upya
kabisa kwa msalaba na ufufuko wa Kristo. Watu wapya wamekusanika kwa jina la
Yesu na kwa msaada wa Roho Mtakatifu wanaitwa kuishi kwa ushirika na upatanisho
na kuzisaidia zawadi hizi kwa wengine.
Thomas hakuwepo
katika mkutano wakati Bwana Mfufuka alijionyesha akitoa zawadi zake. Hakika
Thomas alipendelea uzoefu tofauti, yaani uzoefu wa “nje ya jumuiya.” Kipengele
cha kwanza kuhusu Thomas ni kuhusu kutokuwepo kwa jumuiya. Mtu huyo ni mfano wa
wale ambao wana ugumu wa kushiriki pamoja katika jumuiya. Kutokuwepo huko ni
hatari kwa uzoefu wao wa imani wa kibinafsi na kunaweza kuweka vikwazo kwa
imani ya wengine. Kwa upande mwingine, tunaweza kusema kwamba mfano wa Thomas
unafanya jumuiya kushuhudia imani yake kwa kweli na kuaminika. Haitoshi kusema “tumemwona Bwana!”. Bali ni
lazima kumtambua na kumtangaza bila hofu kama “Bwana wangu na Mungu wangu!”.
Kwa sababu ya Thomas, Yesu anatangaza maneno haya ya ajabu, yaani “Heri
walioamini bila kuona.”
Kwa mitume Yesu anatupa
zawadi ya imani na kumwomba tuishi imani hii pamoja na wengine, kwa kupendana
na kusaidiana kama matokeo ya maisha mapya kutokana na ufufuko wa Bwana wao. Mtu
ana ugumu wa kuamini ikiwa anaamini peke yake. Imani ya mtu ni matokeo ya
uzoefu wa jumuiya ya Kanisa, kwa sababu imani ya Kanisa inaitangulia, inaizaa
na kuiimarisha imani ya mtu huyo. Bila ushiriki kwa hamu katika Jumuiya ya
Kanisa, tuko na ugumu wa kutambua ishara za uwepo wa Bwana Mfufuka miongoni
mwetu na imani yetu inakuwa haba na tena ndiyo hatari kwa uzoefu wa wengine.
Andiko hili linatusaidia
kutambua umuhimu wa kushiriki pamoja katika jumuiya. Bwana Mfufuka alitaka
kujifunua kwetu kupitia msaada wa wengine. Tunapaswa kuwa macho kwa mwelekeo wa
ubinafsi katika jamii ambao umeshawishi mahusiano yetu na kuuvuruga undugu wetu.
Kwa njia ya ubinafsi maovu mengi yanatujia. Ni lazima kumchukua Yesu kama
kipimo cha uzoefu wetu wa jumuiya nayo jumuiya inapaswa kuwa na nafasi muhimu katika
maisha yetu ili tuweze kushinda hofu na kutokuwa na imani ili ushuhuda wetu uwe
ufanisi katika hali iliyo kandokando yetu.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário