Mostrando postagens com marcador UBABA. Mostrar todas as postagens
Mostrando postagens com marcador UBABA. Mostrar todas as postagens

sexta-feira, 24 de junho de 2016

MUNGU ANATUPATIA YALE TUNAYOHITAJI


Kutafakari kuhusu Mt 6, 24-34

Kifungu hiki cha injili ni andiko la msingi wa kiroho ya Mt. Yohane Calabria. Huyu ni mwanzilishi wa Shirika letu, yaani, Poor Servants of Divine Providence. Alianza kuwajali watoto maskini na yatima kwa sababu alitambua kwamba tendo hili lilikuwa mapenzi ya Mungu. Nambari ya watoto iliongezeka daima na vyakula havikutosha kwa wote. Lakini Mungu aliyekuwa makini sana kwa hali hii, akapatia daima yale ambayo Yohane Calabria na watoto waliyahitaji kwa kuishi. Hali hili ilidhihirisha maneno ya injili ambayo tunatafakari.
Kwa upande wa Mungu, yeye anajua kwamba tunahitaji mambo hayo yote. Kwa upande wa binadamu ni lazima kuwa na imani na kujisalimisha mikononi mwa Mungu ambaye ni Baba na Mtoaji. Mtakatifu Yohane Calabria alikuwa na uhakika kuhusu hali hii kwa sababu “aliishi injili na kwa injili”. Kupitia Injili aliugundua ubaba wa Mungu kwa njia halisi sana. Ugunduzi huu mkubwa ulisimuliwa na Askofu aliyeitwa Chiot kutoka Jimbo la Verona - Uitalia ambaye alitembelewa na Mt Calabria kwa kumjulisha kuhusu tukio muhimu. Huu ni msukumo katika safari yetu kama watoto wa Mungu.
“Usiku mmoja, padre Calabria aliandika na kuituma barua kwa baba askofu Chiot akisema, “ningojee kesho saa nne asubuhi maana nahitaji kuongea nawe. Wakati padre Calabria alipofika nyumbani mwa Askofu Chiot, baba huyo alimwuliza swali: Je, bahati mbaya gani ilitokea? Barua yako ilinisumbusha. Padre Calabria akamwambia, “hapana bahati mbaya; hili ni jambo la ajabu.” - “La ajabu!”, aliuliza baba Chiot. Naye padre Calabria aliendelea kwa kusema, “Alisoma injili nzima!” Baba askofu alisema, “Hili si jambo la ajabu!” Je, inawezekana kuwepo padre ambaye hajasoma injili nzima?” Padre Calabria alisema, “Tafadhali, niruhusu kueleza. Mimi pia nimekwisha soma na kuihubiri injili, lakini juzi baada ya kuishi kwa ugumu mchana kutwa na bila kupata utulivu kwa kulala usingizi, nilichukua inijili na kuisoma nzima pamoja na kitabu cha Matendo ya Mitume. Nilipata kusoma kila kitu kwa usiku mmoja peke yake. Jambo hili lilisababisha uzoefu wa ajabu maishani mwangu. Kweli injili ni jambo kubwa! Nimestaajabia. Hebu, sikiliza! “Msiwe na wasiwasi kuhusu maisha yenu: mtakula nini au mtakunywa nini, au kuhusu miili yenu, mtavaa nini. Waangalieni ndege wa angani, wao hawapandi wala hawavuni au kuweka ghalani, lakini Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Fikirini maua ya shambani yameavyo. Hayafanyi kazi wala hayafumi. Lakini nawaambia, hata mfalme Solomoni katika fahari yake yote hakuvikwa kama mojawapo ya hayo maua.”
Padre Calabria ailikuwa amesisitiza yaliyomhakikishia maana ya kweli ya kuishi na kutangaza, yaani Mungu ni Baba nasi tu watoto wake. Alichukua kama ahadi na mpango wa maisha kwake na kwa shirika lake zima maneno ya mstari wa 23, yaani, “Mtafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake na hayo yote mtapewa kwa ziada.”
Je, Maneno haya yana maana gani katika safari yetu siku ya leo? Kulingana na Yesu hatuwezi kuwatumikia mabwana wawili, yaani Mungu na mali. Mali inaweza kuvuruga uangalifu wetu kwenye njia ya Mungu ya kutenda na kuwajali watoto wake. Yesu hakanushi kwamba sisi tunahitaji mambo mengi. Lakini anajua kwamba kosa la utambuzi linatuongoza kuishi kwa wasiwasi na kusumbukika kuweka uangalifu katika yale yasiyo muhimu sana.
Kulingana na mafundisho tumepokea kutoka kwa Yesu Mungu ni Baba kabla ya kuwa Muumba. Yeye si kama baba yeyote bali yu Baba Mwema ambaye anashughulika sana na hali ya wana wake. Yeye analinda na kutunza bila kulala. Yeye anajua mahitaji ya wana kabla ya wamwombe kitu. Kwa utunzaji wa upendo Mungu anashiriki zawadi zake na wana wake, kutarajia kwamba tufanye vivyo hivyo kwa ajili ya wengine ili undugu kati yetu uwe maonyesho ya ubaba wake. Matatizo yote yapaswa kufikiriwa na kusomeka kwa maelewano na ubaba wa Mungu.” Mungu hamsahau hata mmoja wa wana wake.

Tunaalikwa kumwelekea kwa imani na kuwa na uhakika kwamba tumepokea sana. Mungu hatupatii daima yale tunayomwomba, bali anatupatia daima tunayohitaji. Ikiwa hatupokei yale tunayomwomba yeye ni kwa sababu hatuombi ipasavyo. Tufanye upya imani yetu katika riziki yake kuwa na tabia kamili katika ushusiano wetu naye.  

Fr Josuel Ndega
Mapitio na marekebisho: Sarah

quarta-feira, 7 de outubro de 2015

MUNGU BABA YETU KATIKA BIBLIA NA KATIKA MAWAZO WA Mt. YOHANE CALABRIA

katika siku hii ya maadhimisho ya sikukuu ya Mtakatifu Yohana Calabria nataka kupendekeza kutafakari kuhusu UBABA WA MUNGU. Tunamshukuru Mungu Baba ambaye ametupa Yohane kama nyota mbinguni na nuru karibu nasi. 
YOHANA WA MASKINI (M: Jorge Trevisol – Translation to Kiswahili: Fr Ndega)
- Imba viumbe vyote! Hii ni siku kwa wote/ Mungu alitupa Yohana, nyota mbinguni, nuru karibu nasi/ imba viumbe na watu!/ imbeni kwa furaha kubwa!/ uhai unapendeza Mungu/ ana upendo wa Baba kwa maskini wake/ Ref: /: Imba Yohana wa maskini, kwamba dunia itakusikiliza/ Mungu aliyefanya mvua, jua, bahari na ni Baba yetu pia.:/ 2. Ninahisi upo karibu/ naimba na unaimba nami/ unasema kwa nyuso za wengi kwa uhai dhaifu ndani yangu unakutafuta/ ufukuze hofu yetu/ kila wakati una nguvu/ Kuishi sasa kwa muda ni kuhisi kwamba wewe ni yote milele/ 3. kwa sababu uliishi hayo/ kwa sababu ulituambia/ vivyo hivyo tutaishi/ pamoja na wewe/ kamwe bila na wewe/
MPANGO WANGU WA KUTAFAKARI
Utangulizi
1 Ubaba wa Mungu katika Biblia
            1.1 neno Baba kwa uhusiano na Mungu katika Agano la Kale
            1.2 neno Baba katika Injili
            1.3 maneno Mungu Baba ni yenyewe ya Waraka wa Mitume
            1.4 Yesu anamdhihirisha Mungu kama Baba
            1.5 “Sala Baba yetu ni awali ya Injili” (Mt. Yohane Calabria)  
2 Uzoefu wa Ubaba wa Mungu kwa Mtakatifu Yohana Calabria na Familia yake ya Kiroho
Hitimisho

Utangulizi
Msomo wa kutafakari kwetu ni kuhusu Mungu Baba au ubaba wa Mungu. Bila shaka kwamba baada ya tutafute maana ya maneno haya katika Biblia, rejeo kwa kutafakari kwetu itakuwa maandiko, mawazo na mtazamo wa Mtakatifu Yohana Calabria. Msomo huu kuhusu ubaba wa Mungu ni jambo la msingi la kiroho ya Calabria. Ni vizuri sana kujua kwamba Yohana Calabria aliwekwa mtakatifu katika mwaka wa Mungu Baba ambao ulikuwa sehemu ya mwisho katika maandalizi kwa sherehe ya yubilei ya Miaka elfu mbili ya kuzaliwa kwake Bwana Yesu Kristu.
Mwanaume huyo mkuu anayeitwa Yohana Calabria alizaliwa terehe nane mwezi wa kumi mwaka wa elfu moja mia nane sabini na tatu. Alikuwa maskini sana kwa mtazamo wa kibinadamu na tajiri sana kwa upande wa Mungu. Kulingana na uzoefu wake tunajifunza kwamba hatuweze kuongea kuhusu Mungu ikiwa hatupitii hayo. Na huu ulikuwa uzoefu wake, yani, Mungu ni Baba na Mtoaji. Ingawa hali mbili inatokea pamoja katika Mungu, tutatafakari kuhusu ubaba peke yake.

1 Ubaba wa Mungu katika Biblia

1.1 neno Baba kwa uhusiano na Mungu katika Agano la Kale
Maneno Baba yetu si maneno ya Yesu tu, kwa sababu kabla yeye yalitumika katika maandiko ya manabii ya Agano la Kale. Bila shaka Yesu hakuyatumia maneno haya tu, bali alianzisha uhusiano mpya na Mungu, akileta maana mpya kabisa kwa maneno Baba yetu. Neno Baba kwa uhusiano na Mungu, tunaweza kukuta katika: Isaya 9:6 (Baba milele); Is 63:16 (wewe ni Baba yetu - mara mbili); Is 64:8 (wewe ni Baba yetu); Yeremia 3:4.19 (Baba yangu – mara mbili); Malaki 2:10 (Tuna Baba mmoja)

1.2 neno Baba katika Injili
Kuhusu injili hali ni tofauti sana kwa sababu neno hili lilikuwapo midomoni mwa Yesu daima, yaani, Baba, Baba yangu, Baba yenu, Baba yake, Baba Yako, Baba yao, Baba yetu,etc. Katika Mathayo - mara 42; Marko – mara 5; Luka - mara 16; Yohane – mara 114. Tunaweza kusema kwamba Yohane ni “Injili ya Baba” kwa sababu inaongea sana kuhusu uhusiano wa Yesu na Baba yake. Tena tunatambua kwamba katika toleo hili peke yake tunaweza kufanya maneno kama Baba mtakatifu, Baba mwenye haki, Baba yangu na yenu pamoja, etc. Katika matoleo ya Mathayo, Marko na Luka tunakuta uzoefu wa ubaba kwa uhusiano na huruma na kujua, kwa nfano, Baba atawasamehe, Baba yenu anajua,etc.  Lakini sala ya Bwana inayojulikana kama Baba yetu, tunaweza kukuta katika Mathayo na Luka peke yao.

1.3 maneno Mungu Baba ni yenyewe ya Waraka wa Mitume
Maneno mawili pamoja, yaani, Mungu Baba, tunakuta katika Agano Jipya peke yake na hasa katika Waraka: Wagalatia 1,1; Waefeso 6,23; Wafilipi 2,11; Wakolosai 3,17; 1Wathesalonike 1,1; 2Wathesalonike 1,2; 1Timotheo 1,4; 2Timotheo 1,4; Tito 1,4; 1Petro 1,2; 2Petro 1,17; 2Yohane 1,3; Yuda 1,1. Mara nyingi maneno haya Mungu Baba yanatumika kuonyesha shukrani au utambulisho kuhusu zawadi za Mungu katika jumuyia. Yanaonyesha pia matakwa ya mtume mwandishi kuhusu safari ya imani ya jumuiya fulani.

1.4 Yesu anamdhihirisha Mungu kama Baba
Yesu anapoongea na Mungu na kuhusu Mungu, anatumia neno Baba. Hali hii inatafisiri uzoefu wa ndani, ushirika wa upendo na uhai kati ya Mwana na Baba yake. Maisha yake na uzoefu wake na Baba ni mwaliko kwa wasikilizaji washiriki katika ushirika sawa, wakiishi kwa uzoefu wa ndani na Mungu. Yesu anatuletea ufunuo wa uso kweli wa Mungu: wa kwanza - Mungu aliye na wasiwasi kwa utunzaji wa upendo kwa kila kitu, “hata nywele moja ya kichwa chetu” (Lk 21,18); wa pili - Mungu Baba, ambaye ana watoto tofauti na anashiriki zawadi zake na wote kwa njia sawa. Anawapenda wote na anataka kwamba watu wote wajihisi kuishi katika familia, washiriki furaha yake kama Baba. Katika familia hii anautoa utunzaji na ulinzi ambao ni maonyesho ya upendo wake wa Baba. Tuko katika ushirika wa ndani naye ikiwa tunashiriki hisia zake kuhusu wengine. Kwa hivyo Yesu alitufundisha kusali, akishiriki nasi njia yake yenyewe ya kusali. Alitujulisha kujua huyo ambaye ni Baba yake na Baba yetu pia.

1.5 “Sala Baba yetu ni awali ya Injili” (Mt. Yohane Calabria)

Mantra: Baba sikia wanao, sikia sauti zao, sikia dunia nzima...
Yesu anapowafundisha wanafunzi wake kusali, aliwakumbusha kuhusu mahitaji ya tabia ya mwana anayemwomba Baba kwa imani. Kama yeye alivyoishi, tabia kamili ya wanafunzi lazima kuwa kujisalimisha mikononi mwa Huyo anayejua mahitaji ya wana kabla ya wamwulize kitu. Sala ya kweli ni kitendo cha kujisalimisha. Sehemu ya kwanza ya sala ambayo Yesu anawafundisha wanafunzi wake ni utambulisho wa ubaba wa Mungu, ambaye ni mwema na mtoaji. Katika sala hii, kila kitu ambacho kinaja baada ya Baba kinategemea kwa neno hili/mwelekeo/hali. Ni lazima kufanya mapenzi ya Mungu ili Ufalme wake utokee duniani kama mbinguni. Mapenzi ya Baba huyu lazima kuwa chakula cha watoto wake kama kilichotokea na uzoefu wa Yesu miongoni mwa wanadamu.  
Kwa Baba huyu sisi lazima kuhutubia kwa imani, wenye uhakika kwamba tumepokea sana. Tunaomba kwa mkate, msamaha na upatanisho. Kulingana na Maandiko matakatifu, “kutokana na wema wake tumepokea neema juu ya neema”. Sala hii inathibitisha utunzaji wa upendo wa Mungu anayeshiriki zawadi zake na wana wake, akitarajia kwamba tufanye vivyo hivyo na wengine ili udugu uwe maonyesho ya kweli ya ubaba wake na chombo cha huruma yake. Maombi Baba yetu yanatufundisha kufikiri kuhusu mahitaji ya wengine na si kwa mahitaji ya kibinafsi tu. Kupitia sala hii tunaomba muhimu zaidi, yaani, “mkate wa kila siku” kwa sababu sisi lazima kupinga dhidi ya aina yote ya ukusanyaji na ubadhirifu ambao unaharibu udugu, kufanya maskini na wenye njaa wateseke. Kuhusu mambo haya Baba Mtakatifu Francisco asema: “Ulaji umetuongoza kutumia chepesi pamoja na ubadhirifu wa chakula cha kila siku... sisi lazima kukumbuka kwamba chakula ambacho sisi hutupa takatakani ni kama ikiwa tulikuwa tumeiba kutoka meza ya walio maskini na wenye njaa.”
Kwa Mt. Yohana Calabria, “sala Baba Yetu ni awali ya Injili. Matatizo lazima kufikiriwa na kusomwa kwa uhusiano na maelewano kwa ubaba wa Mungu.” Ikiwa tunasema “Baba Yetu” ni kwa sababu tunasadiki kwamba sisi ni ndugu wa wengine wengi. Mungu hawabagui watu na hamsahau yeyote wa wana wake. Hapendezwi na sala ambayo haifikirii ndugu wengine. Mungu si daima anatupa vitu ambavyo tunamwomba, bali anatupa daima vitu tunavyohitaji kwa sababu anajua kila kitu. Ikiwa mara nyingi hatupokei vitu ambavyo tunamwomba ni kwa sababu hatuombi ipasavyo. Labda kutokuwa na tabia na nia kamili iliyodaiwa na Yesu wakati aliwafundisha wafuasi wake kusali. Tunaalikwa kuishi kwa udugu kutokana na ubaba wa Mungu na kuwa na mioyo ya wana, kwa sababu mtu asiyeishi kama mwana hajifunzi kuwa ndugu.

2 Uzoefu wa Ubaba wa Mungu kwa Mt. Yohana Calabria na kwa Familia yake ya Kiroho
Mantra: Baba yetu sisi ni wanawe, Baba yetu sisi ni ndugu...
Mt. Yohane Calabria alikuwa mwenye unyeti daima kwa ishara za utunzaji wa Mungu ulimwenguni. Lakini usiku mmoja wakati yeye hakupata kulala usingizi, alichukua injili na aliufanya ugunduzi mkubwa. Aligundua jinsi ya kuishi kwa uhalisi ubaba wa Mungu. Kifungu ambacho kiliichukua uangalifu wake zaidi kilikuwa Mt 6,24-34. Kutokana na kifungu hiki alichukua ahadi kwake na kwa familia yake ya kiroho, yaani, “Mtafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake; na hayo yote mtapewa kwa ziada.” Kulingana naye kwa kushuhudia duniani kwamba Mungu ni Baba, Mama, Kila Kitu, tunahitaji kwanza kufanya sisi wenyewe uzoefu wa ubaba wa Mungu na kulima hisia ya miliki ya Baba huyu. Kama hivyo alimwambia mama fulani: “Sisi ni wa Mungu, Mungu ni Baba, Mama Kila kitu chetu. Upende Bwana na atakuwa heri (mwenye furaha)” (24-1-1930).
Kwa yeye, “Mungu ni Baba na Baba mwema. Hakuna mama ambaye anawapenda sana watoto wake kama Mungu anawapenda watu wote na kila mmoja wetu”. Calabria anaongea pia kuhusu Mungu kama Riziki, kwa sababu kulingana naye, haiwezekani kutenga Ubaba wa Mungu na Riziki yake. Kwa hivyo, asema, “Riziki ni Mama mpole ambaye hupatia kila kitu kwa wema wetu, hata kwa wema wetu mkubwa. Tunapaswa kuhisi tumebebwa kwa mikono yake ya mama”. Yohana Calabria aliamini katika ukweli huo na aliyapanga maisha na kazi zake zote kulingana na hali hii. Katika mwanzo mwa kazi yake, alipoonekana mtoto wa kwanza, Yohana alifahamu kwamba Mungu akatarajia kutoka kwake imani maalum ambayo huonyeshwa kupitia matendo mema kwa masikini wapendelewa na Mungu. Baada ya mtoto wa kwanza, wengine wengi walikuja nyumbani. Nyumba hiyo iliitwa “Nyumba ya wavulana wema”. Kama hii, ishara ya mapenzi ya Mungu ilikuwa wazi sana kwa Yohana Calabria.
Kupitia uzoefu ambao Mt. Calabria aliishi kuhusu ubaba wa Mungu, akawa mshahidi na mhubiri wa ubaba huu. Kama hivyo asema, “Injili anatuongelea, kwa mfano, Mungu ni Baba, anatujali zaidi kuliko ndege wa angani na maua ya mashamba hata atatujalia kile ambacho tunahitaji kwa chakula na kwa mavazi, lakini tunapaswa kuutafuta kwanza Ufalme wake na haki yake. Basi, je, imani yetu katika ubaba wa Mungu ni nzuri? Je, tena ni nzuri imani yetu katika Riziki yake takatifu na wema?” 
Imani kweli na asili inafikiria Mungu si kama Muumba na Bwana tu, bali kwanza kama Baba”. Mungu ni Baba, hutujali na wote ambao tunawapenda; macho yake ni makini sana kwa kila kitu; hakuwezi tokea chochote kisichotarajiwa kama mshangao (bila maana); kila kitu kinapangwa na kuongozwa na hekima, nguvu na wema wake pasipo mwisho. Juu ya yote tunaweza kusema kwamba ni kwa wema wake.

Hitimisho
Uzoefu wa ubaba wa Mungu ulimhamasisha Yohane Calabria kuanza Kazi kubwa. Katika mwanzo, padre Yohane alisaidiwa na mama yake. Lakini, baada ya wakati mchache, walikuja Mabruda, Mapadre, Masister, makundi mengi ya watu wasio watawa. Pamoja na padre Yohana, sisi ni Familia ya Kiroho ya Calabria inayoitwa “Poor Servants of Divine Providence” na kazi yetu ni kutafuta Ufalme wa Mungu. Hali hii inatokea katika ahadi ya kuifufua imani duniani kwa Mungu Baba wa wanadamu wote, kupitia kujisalimisha kabisa kwa Riziki yake. Kiroho yetu ni Injili. Kulingana na Mtakatifu Yohana Calabria, tunahitaji kurudi kwa Injili daima ili maisha yetu yabadilike na hali kandokando yetu pia.
Maandiko ya Mt. Yohana Calabria yanadhihirisha jinsi alivyokuwa na ubinadamu mno, akifahamu ugumu wa wengine, lakini kwa wakati sawa, alijua kuonyesha njia kamili kwa ufumbuzi wa matatizo yao. Kutokana na uzoefu wa Mt. Calabria tunajifunza kwamba Mungu ni Baba mwema na mtoaji bila mwisho, na sisi sote ni ndugu katika Kristo. Tunaalikwa kuishi kama ndugu kutokana na ubaba wa Mungu na kuwatendea mema wengine vivyo hivyo tungependa wao watutendee. Kulingana naye, “Tunapaswa kuwa na kujihisi watumishi, bali kwa utumishi wa Mwenyeji fulani ambaye ni pia, na kwanza kabisa, Baba. Basi utumishi wetu ni wa wana, utumishi wa huria na upendo... kama alivyotumika Bwana wetu Yesu Kristo, mtumishi wa Baba kwa namna ya ajabu, ambaye wakati wa maisha yake ya kibinadamu alifanya tu kutimiza amri zako: “Ninafanya kama Baba alivyoniamuru kufanya.”

Tumsifu na tumshukuru Mungu Baba kwa kielelezo cha imani ambacho ni Yohane Calabria na mtume wake duniani kupitia Familia yake ya Kiroho. 

Fr Ndega
Mapitio: Sara