Mostrando postagens com marcador MASKINI. Mostrar todas as postagens
Mostrando postagens com marcador MASKINI. Mostrar todas as postagens

terça-feira, 27 de setembro de 2016

HALI YA MASKINI INATUHUSU SISI


Kutafakari kuhusu Lk 16, 19-31

     Mungu anashutumu kutofautiana na unafiki katika safari ya watu wake na anapendekeza njia tofauti. Kulingana na somo la kwanza, utumwa katika safari ya Waisraeli ulikuwa matokeo ya kosa la uhusiano mwema na Mungu na la ahadi ya kuujenga undugu. Ibada yao ilibadilika kuwa jambo bila maana, yaani haikuonyesha tena ukarimu wa moyo wala haikusababisha mabadiliko katika uhusiano miongoni mwa watu na katika jamii. Walio na nguvu waliishi kwa kutofautiana mbele ya hali ya wengine na matendo ya nje hayakuihusu tabia ya ndani. Wakitenda hivi walivutia hali mbaya kwa maisha yao. Lakini tunajua kwamba Mungu hakuwaacha watu hawa, akitenda kwa uaminifu hasa kuhusu hali ya maskini na wasio na nguvu kwa maana maisha yao yanathamini sana kwa Bwana. Somo la pili linaonyesha ushuhuda wa Mtakatifu Paulo kuhusu Timotheo. Kulingana na ushuhuda huu haiwezekani kuwa mtu wa Mungu kwa kulitumia jina tu. Utambulisho wa mtu wa Mungu wa kweli unaonyeshwa kupitia kufuata haki, utawa, imani, upendo, uvumilivu na upole.   

       Kama tujuavyo, mifano ni sehemu ya ajabu ya ufundishaji wa Yesu. Kupitia mfano yeye anaweka rahisi na kupatikana kwa wote siri za Ufalme wa Mungu. Katika andiko hili, Yesu anasimulia mfano wa mtu tajiri na Lazaro maskini anawaonya wasikilizaji wake kuhusu hali ijayo iliyo matokeo ya chaguzi za watu katika wakati huu. Mtu tajiri ni ishara ya walio na mazoea ya kuitumainia mali bila kuguswa na hisia kuhusu kile kinachotokea kandokando yao. Hao walichagua kwa nafsi yao njia ambayo itawaongozea mauti. Lazaro ni ishara ya walio maskini ambao wameachwa bila ulinzi na utunzaji; wanapiga kelele ili wapate nafasi ya kuishi kwa heshima. Tena Lazaro ni pendekezo la kuishi tofauti, kuyalenga maisha katika thamani za kweli. Huyo ni ishara ya uvumilivu, ya mapigano na mwaliko wa kumtumainia Mungu ambaye katika riziki yake hawaachi wale ambao wanamwamini.

       Kupitia mfano huu Yesu anatukumbusha kuhusu hali ya kikatili ambayo ipo katika jamii yetu, yaani kutokuwa na usawa kati ya watu. Katika mafundisho yake, Kanisa limeshutumu hali hii mara nyingi kwa kusema, “Hali mbaya ya jeuri imezaa matajiri walio na utajiri zaidi daima juu ya maskini walio maskini zaidi daima.” Hali hii ni tofauti kabisa na matarajio ya Mungu ambaye, kulingana na wema wake, ananyesha mvua kwa wenye haki na wasio na haki, tena kwa walio wema na kwa wabaya ili vitu vyote alivyoumba kwa wote vipatikane kwa wote. Mfano mzuri tunapata katika Wimbo wa Bikira Maria ambao unaishuhudia njia ya ajabu ya Mungu ya kutenda, yaani yeye huwashusha wakuu na kuwapandisha wadogo ili waweze kuishi pamoja kama ndugu na kwa usawa wa haki na wa heshima. Mungu anajitambulisha na hali ngumu ya wasio na nguvu na ya maskini. Udhalimu wote unaofanyika kwao unamgusa Mungu ndiye kuwepo katika upande yao. Katika wakati ujao, baada ya hali ya dunia, hali itakuwa tofauti, yaani waliopokea mambo mema katika maisha yao bila ahadi na hisia kuhusu hali ya wengine wataumizwa na wale waliopata mabaya kama Lazaro alivyo, watafarijiwa. Yeyote ambaye anatumia mali yake ili awadharau wengine anatupa maisha yake takatakani kwa sababu maisha hayamaanishi mali mengi bali uwezo wa kutenda mema. Kuhusu mambo haya Mt. Yohana Calabria alikuwa na haya ya kusema: “Maskini wako ili matajiri waokoke/waokolewe”. 

     Hali ya maskini ina uhusiano na sisi sote, kwa sababu “dhambi ya jamii ni matokeo ya kiasi cha dhambi za kibinafsi”. Basi, ni lazima toba/mabadiliko sio kwa ajili ya dhambi za kibinafsi tu, bali pia kuchukua jukumu kuhusu dhambi ya kijamii. Mwendo huu unaweza kwanza kupitia tabia ya kuacha njia ya ukusanyaji ambayo kwa kawaida inatuongoza kuwa na kutofautiana kuhusu hali ya wengine. Tunaalikwa kuchukua njia ya unyenyekevu inayokihusu kitu kidogo na kutufanya kuguswa na hisia kuhusu wale wasio na kitu. Mungu anatuokoa maana ya upendo wake, lakini anathamini sana juhudi zetu kama alivyosema Baba Mt. Benedito wa kumi na sita: “kwa kweli, wokovu ni zawadi iliyo neema ya Mungu, lakini ili uwe ufanisi katika maisha yangu unadai ridhaa yangu, ambayo inaonyeshwa kupitia matendo, yaani kupitia utayari wa kuishi kama Yesu alivyo kwa kuufuata mfano wake.” 

Fr Ndega

quarta-feira, 24 de fevereiro de 2016

HALI YA MASKINI INA UHUSIANO NASI


Kutafakari kuhusu Lk 16, 19-31

     Kama tujuavyo, mifano ni sehemu ya ajabu ya ufundishaji wa Yesu. Kupitia mfano yeye anaweka rahisi na kupatikana kwa wote siri za Ufalme wa Mungu. Siku ya leo Yesu anasimulia mfano wa mtu tajiri na Lazaro maskini anawaonya wasikilizaji wake kuhusu hali ijayo na kama matokeo ya chaguzi za watu katika wakati huu. Mtu tajiri ni ishara ya walio na mazoea ya kuitumainia mali bila unyeti kuhusu kile kinachotokea kandokando yao. Wao walichagua kwa nafsi yao njia ambayo itawaongozea mauti. Lazaro ni ishara ya walio maskini ambao wameachwa bila ulinzi na utunzaji; wanapiga kelele ili wapate nafasi ya kuishi kwa heshima. Kwa wakati sawa, Lazaro pia ni pendekezo la kuishi tofauti, kuyalenga maisha katika thamani za kweli. Huyo ni ishara ya uvumilivu, ya mapigano na mwaliko wa kumtumainia Mungu ambaye katika riziki yake hawaachi wale ambao wanamwamini.
      Kupitia mfano huu Yesu anatukumbusha hali katili ipo katika jamii yetu, yaani kukosekana kwa usawa kati ya watu. Katika Amerika Latina, kanisa lilikuwa limekwisha shutumu baadhi ya miaka iliyopita kwamba “Hali mbaya ya jeuri imezaa matajiri waliokuwa na utajiri zaidi daima juu ya maskini waliokuwa maskini zaidi daima.” Hali hii ni tofauti kabisa na matarajio ya Mungu ambaye, kulingana na wema wake, ananyesha mvua kwa wenye haki na wasio na haki, tena kwa walio wema na mabaya ili vitu vyote alivyoumba kwa wote vipatikane kwa wote.. wimbo wa Bikira Maria unashuhudia hali hii kwa njia ya ajabu na furaha kubwa kwa sababu ya njia ya Mungu ya kutenda, yaani yeye huwashusha wakuu na kuwapandisha wadogo ili waweze kuishi pamoja kama ndugu na kwa usawa wa haki na heshima.  
     Mungu anajitambulisha na hali ngumu ya wasio na nguvu na ya maskini. Udhalimu wote unaofanyika kwao unamfikia Mungu ndiye yumo ndani yao. Katika wakati ujao, baada ya hali ya dunia, hali itakuwa tofauti, yaani waliopokea mambo mema katika maisha yao bila ahadi na unyeti kuhusu hali ya wengine wataumizwa na wale waliopata mabaya kama Lazaro alivyo, watafarijiwa. Yeyote ambaye anatumia mali yake awadharau wengine anatupa maisha yake takatakani kwa sababu maisha hayamaanishi mali mengi bali uwezo wa kutenda mema. Kuhusu mambo haya Mt Yohana Calabria asema: “Maskini wako ili matajiri waokoke/waokolewe”. 

     Kipindi cha Kwaresima kinatukumbusha kwamba hali ya maskini ina uhusiano nasi, kwa sababu dhambi ya jamii ni matokeo ya kiasi cha dhambi kibinafsi. Basi, ni lazima toba sio kwa dhambi za kibinafsi tu, bali kuchukua jukumu kuhusu dhambi ya jamii pia. Mwendo huu unaweza kwanza kupitia kuacha njia ya ukuzaji na ukusanyaji ambayo kwa kawaida inatuongoza kwa kutofautiana ili tuchukue njia ya unyenyekevu ya maisha ambayo inakihusu kitu kidogo na kutufanya wenye unyeti kuwahusu wale wasio na kitu. Mungu anatuokoa kwa sababu ya upendo wake, lakini anathamini sana juhudi zetu kama alisema Baba Mt Benedito wa kumi na sita: “kwa kweli, wokovu ni zawadi iliyo neema ya Mungu, lakini ili uwe ufanisi katika maisha yangu unakudai kukubalika kwangu kuonyeshwa kupitia matendo, yaani kupitia utayari wa kuishi kama Yesu alivyo na kutembea baada yake.”

Fr Ndega
Mapitio: Sara 

domingo, 24 de janeiro de 2016

MJUMBE WA HABARI NJEMA KWA MASKINI NA WALIOKATALIWA NA JAMII


Kutafakari kuhusu Lk 1, 1-4: 4,14-21

        Liturujia ya jumapili hii inaongea kuhusu umuhimu wa Neno la Mungu ambalo lazima kusikika kwa heshima na kutangazwa kwa shauku. Neno hili ni alama ya upendo na utunzaji wa Mungu kwa watu ambao ni mali yake. Katika somo la kwanza, Ezra aliitangaza Torati ambayo ni Neno la Mungu kwa Waisraeli. Watu walisikiliza kwa uangalifu na kujibu kwa utayari. Neno la Bwana ni faraja na kutia moyo. Hili Neno ni maana ya furaha ambaye inakuja kutoka kwa Bwana na kuitoa nguvu kwa watu wote. Kupitia Neno la Mungu watu wanakumbuka mambo makuu ambayo yaliwapa maana ya utambulisho kama Watu wa Mungu. Ni mwaliko wa kumsifu Mungu kwa sababu ya uaminifu wake na kufanya upya ahadi yao ya waruhusu kuongozwa na Mungu ambaye anaongea kuzionyesha njia za uzima na ukombozi. Kama Watu wa Agano la Kale waliokusanyika kama mtu moja kwa sababu ya Neno la Mungu, vivyo hivyo ni uzoefu wetu kama washiriki wa mwili wa Kristo, yaani ingawa sisi ni wengi, tulibatizwa kuwa mwili mmoja. Karama mbalimbali ambazo tumepokea ni kwa ajili ya manufaa ya mwili mmoja huu.
Sehemu ya kwanza ya injili inaongea kwamba habari njema ya Kristo iliwazaa mashahidi wengi. Imani yetu ni matokeo ya uzoefu, yaani uzoefu ambao tumepokea kutoka kwa waliotutangulia na uzoefu wa kutafuta binafisi. Maisha ya wale waliotutangulia yanaendelea kushuhudia kwamba bila uzoefu imani yetu katika Kristo ni haba. Mwinjilisti Luka analitoa andiko lake kwa heshima ya mtu fulani aliyeitwa Theofilo, kwa sababu katika karne ya kwanza yalikuwa mazoea kufanya hivyo. “Theofilo alikuwa mtu wa maana aliyesifika katika jamii ya Wapagani, aliye kuwa Mkristo kutokana na mahubiri ya mitume.” Maana ya neno Theofilo ni “mpendwa wa Mungu”. Kama haya ni matokeo ya uzoefu wetu wa Neno la Mungu, yaani tunakuwa wapendwa. Sehemu ya pili ni kuhusu uzoefu wa Yesu mjini mwake Nazareti, mahali alipolelewa. Alienda huko akiongozwa na Roho Mtakatifu na kutangaza kwa shauku Neno la Mungu kama mpango wake kwa watu waliotarajia ufunuo wa Masiya kwa hamu sana.
Yesu alichagua wakati wa liturujia kwa kutangaza kipaumbele cha kazi yake. Anajihisi aliyetiwa mafuta na kutumwa na Roho ili atangaze habari njema kwa maskini na ukombozi kwa wanaoonewa; yeye anaweza kuyafufua matumaini yao na kuwarudishia furaha ya maisha yao. Hali hizi ni maana ya utambulisho wa Yesu na sehemu ya mpango wa upendo na wokovu wa Baba yake. Kipaumbele cha Yesu ni kipaumbele cha Mungu. Basi, tunaweza kuwaza furaha kubwa imo ndani ya Yesu kwa sababu ya njia hii ya Mungu ya kutenda. Mungu anapenda kila mtu na kutaka kuwafikia wote kwa upendo wake. Lakini kuna baadhi ya watu ambao wanahitaji utunzaji maalum, kwa sababu wanakataliwa na jamii. Mungu anatudai kuwa macho kwa hali hii. 
Katika Yesu wakati wa neema na wokovu unaanza. Yesu ni mkombozi ambaye alikuja kuwaweka huru wanadamu wote waliopoteza uhuru wao kwa sababu ya dhambi. Ukombozi ambao Yesu anatangaza ni zaidi kuliko hali ya roho iliyosababishwa na dhambi. Anataka kuifikia jamii kabisa, kwa sababu hali hii ina mawazo kinyume na mpango wa Mungu uliodhihirishwa na Yesu. Kama inavyotokea katika kifungu kingine (k.m. Mathayo) hii ni sehemu ya tangazo la Ufalme wa Mungu ambalo linalihusu pendekezo la mabadiliko. Sisi sote pamoja na jamii nzima tunapaswa kufikiri vizuri kuhusu mwelekeo ambao tumechagua kwa maisha yetu. Yesu anataka kuujenga ubinadamu na jamii mpya. Anaweza kufanya hivi peke yake, lakini anapendelea kutuhusisha ili tuwe na unyeti kama yeye alivyo na tuweze kuchukua vipaumbele vya utume wake. Nguvu ya neno la Yesu ilitokana na upako wa Roho Mtakatifu. Roho mmoja aliyemwongoza Yesu katika kazi yake anataka kutuongoza pia ili tuwe na uhusiano mpya na walio maskini na waliokataliwa kati yetu. Ufunuo wa Yesu ni hamasa ili tufanye tofauti maishani mwa watu wengi. Neema yake itusaidie tuwe vyombo vya wema na utunzaji maalum kwa walio na mahitaji mengi.
Fr Ndega

Mapitio: Sara