Kutafakari
kuhusu Lk 16, 19-31
Mungu anashutumu kutofautiana na unafiki katika safari ya watu wake na
anapendekeza njia tofauti. Kulingana na somo la kwanza, utumwa katika safari ya
Waisraeli ulikuwa matokeo ya kosa la uhusiano mwema na Mungu na la ahadi ya
kuujenga undugu. Ibada yao ilibadilika kuwa jambo bila maana, yaani
haikuonyesha tena ukarimu wa moyo wala haikusababisha mabadiliko katika
uhusiano miongoni mwa watu na katika jamii. Walio na nguvu waliishi kwa kutofautiana
mbele ya hali ya wengine na matendo ya nje hayakuihusu tabia ya ndani. Wakitenda
hivi walivutia hali mbaya kwa maisha yao. Lakini tunajua kwamba Mungu
hakuwaacha watu hawa, akitenda kwa uaminifu hasa kuhusu hali ya maskini na
wasio na nguvu kwa maana maisha yao yanathamini sana kwa Bwana. Somo la pili linaonyesha
ushuhuda wa Mtakatifu Paulo kuhusu Timotheo. Kulingana na ushuhuda huu haiwezekani
kuwa mtu wa Mungu kwa kulitumia jina tu. Utambulisho wa mtu wa Mungu wa kweli unaonyeshwa
kupitia kufuata haki, utawa, imani, upendo, uvumilivu na upole.
Kama tujuavyo, mifano ni sehemu ya ajabu ya ufundishaji wa Yesu. Kupitia
mfano yeye anaweka rahisi na kupatikana kwa wote siri za Ufalme wa Mungu. Katika
andiko hili, Yesu anasimulia mfano wa mtu tajiri na Lazaro maskini anawaonya
wasikilizaji wake kuhusu hali ijayo iliyo matokeo ya chaguzi za watu katika
wakati huu. Mtu tajiri ni ishara ya walio na mazoea ya kuitumainia mali bila kuguswa
na hisia kuhusu kile kinachotokea kandokando yao. Hao walichagua kwa nafsi yao
njia ambayo itawaongozea mauti. Lazaro ni ishara ya walio maskini ambao wameachwa
bila ulinzi na utunzaji; wanapiga kelele ili wapate nafasi ya kuishi kwa
heshima. Tena Lazaro ni pendekezo la kuishi tofauti, kuyalenga maisha katika
thamani za kweli. Huyo ni ishara ya uvumilivu, ya mapigano na mwaliko wa
kumtumainia Mungu ambaye katika riziki yake hawaachi wale ambao wanamwamini.
Kupitia mfano huu
Yesu anatukumbusha kuhusu hali ya kikatili ambayo ipo katika jamii yetu, yaani
kutokuwa na usawa kati ya watu. Katika mafundisho yake, Kanisa limeshutumu hali
hii mara nyingi kwa kusema, “Hali mbaya ya jeuri imezaa matajiri walio na
utajiri zaidi daima juu ya maskini walio maskini zaidi daima.” Hali hii ni
tofauti kabisa na matarajio ya Mungu ambaye, kulingana na wema wake, ananyesha
mvua kwa wenye haki na wasio na haki, tena kwa walio wema na kwa wabaya ili
vitu vyote alivyoumba kwa wote vipatikane kwa wote. Mfano mzuri tunapata katika
Wimbo wa Bikira Maria ambao unaishuhudia njia ya ajabu ya Mungu ya kutenda,
yaani yeye huwashusha wakuu na kuwapandisha wadogo ili waweze kuishi pamoja
kama ndugu na kwa usawa wa haki na wa heshima. Mungu
anajitambulisha na hali ngumu ya wasio na nguvu na ya maskini. Udhalimu wote
unaofanyika kwao unamgusa Mungu ndiye kuwepo katika upande yao. Katika wakati
ujao, baada ya hali ya dunia, hali itakuwa tofauti, yaani waliopokea mambo mema
katika maisha yao bila ahadi na hisia kuhusu hali ya wengine wataumizwa na wale
waliopata mabaya kama Lazaro alivyo, watafarijiwa. Yeyote ambaye anatumia mali
yake ili awadharau wengine anatupa maisha yake takatakani kwa sababu maisha
hayamaanishi mali mengi bali uwezo wa kutenda mema. Kuhusu mambo haya Mt.
Yohana Calabria alikuwa na haya ya kusema: “Maskini wako ili matajiri
waokoke/waokolewe”.
Hali ya maskini ina uhusiano na sisi sote, kwa sababu “dhambi ya jamii
ni matokeo ya kiasi cha dhambi za kibinafsi”. Basi, ni lazima toba/mabadiliko
sio kwa ajili ya dhambi za kibinafsi tu, bali pia kuchukua jukumu kuhusu dhambi
ya kijamii. Mwendo huu unaweza kwanza kupitia tabia ya kuacha njia ya
ukusanyaji ambayo kwa kawaida inatuongoza kuwa na kutofautiana kuhusu hali ya
wengine. Tunaalikwa kuchukua njia ya unyenyekevu inayokihusu kitu kidogo na kutufanya
kuguswa na hisia kuhusu wale wasio na kitu. Mungu anatuokoa maana ya upendo
wake, lakini anathamini sana juhudi zetu kama alivyosema Baba Mt. Benedito wa
kumi na sita: “kwa kweli, wokovu ni zawadi iliyo neema ya Mungu, lakini ili uwe
ufanisi katika maisha yangu unadai ridhaa yangu, ambayo inaonyeshwa kupitia
matendo, yaani kupitia utayari wa kuishi kama Yesu alivyo kwa kuufuata mfano
wake.”
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário