Kutafakari kuhusu Lk 15, 1-32
Sura ya kumi na tano ya toleo la Luka ni maarufu miongoni mwa mifano ya
Yesu. Hii inaitwa sura ya Mifano ya huruma. Tuko na mifano mitatu (Kondoo
aliyepotea: 4-7; Sarafu iliyopotea: 8-10; Mwana mpotevu: 11-32). Mifano hii inaonyesha
tabia ya huruma ya Mungu kuhusu wenye dhambi na furaha ya kukutana tena na yule
ambaye alipotea. Kwa kufahamu nia ya Yesu alipoisimulia mifano hii tunahitaji
kutafakari kwanza kuhusu mazingira ambayo Yesu aliishi.
Katika muktadha huo, baadhi ya watu walijiona waliostahili wokovu wa Mungu kwa sababu
ya uaminifu wao kwa Sheria. Walichukua mamlaka ya kuwatenganisha watu, wakiwapanga
kama wema au wabaya. Mamlaka haya hayatoki kwa Mungu kwa sababu kipimo ni
ubaguzi. Walisahau kwamba mbele ya Mungu watu wote ni sawa. katika njia yake ya
kupenda Mungu hambagui yeyote. Kwa upande wake watoza ushuru na wenye dhambi ni
watoto wake kama vile ndio Mafarisayo na Waandishi. Ikiwa hao wanaweza kuzaa undugu,
tena wataweza kuishi katika ushirika na Mungu, anayekaribisha kila mtu ili awaokoe
wote.
Ingawa
yako matukio mengi katika Agano la Kale, ambayo yanaonyesha njia maalum ya
Mungu ya kutenda, ni “katika Yesu Kristo kwamba huruma ya Mungu imepata kuwa
hai na yenye kuonekana, na hata ilifikia kilele chake katika Yeye... Yesu ni
uso wa huruma ya Baba. Kila kitu ndani
yake kinaongelea huruma. Hakuna chochote kwake kinachopungukiwa na huruma (Baba
Mt Francisco).” Kama
alama ya huruma ya Mungu, Yesu ana chaguo wazi sana, yaani, “Mtu huyu huwakaribisha
wenye dhambi, tena hula nao”. Maneno haya yalisemwa na wale waliompinga Yesu. Kwa
kweli, Yesu alikuwa na njia maalum ya kuongelea huruma ya Mungu, yaani katika Yesu
jambo la huruma lilionyeshwa “kwa
neno lake, matendo yake na kwa nafsi yake yote.” Yeye alitumia
ishara nyingi za makaribisho, akithibitisha lengo la ujumbe wake na ukweli wa
mafundisho yake. Kwa kweli, watozaushuru wengi, makahaba na wengine waliokataliwa
na jamii, walijiona kukaribishwa na Yesu na tena kubadilishwa kwa sababu ya
mkutano na huruma ya Mungu.
Katika mfano wa mwana mpotevu,
ingawa tuko na tukio la kijana mdogo na hisia za kijana mkubwa, macho yetu yamlenga
baba wa vijana hawa wawili ndiye aliye mhusika mkuu wakati wote. Uhusiano wake
wa mapendo kwa vijana wake, ambao wote ni wapotevu kwa njia tofauti ndio
umuhimu wa tukio hili. Kulingana na Yesu, baba huyo ni kama Mungu ambaye ana
watoto tofauti na kushiriki nao zawadi zake kwa njia sawa. Yeye anawapenda wote
na kutaka watu wote wajione wakiwa katika familia, kushiriki kwa furaha yake
kama Baba. Katika familia hii anautoa utunzaji na ulinzi ili wawe na maana
nzuri ili kubaki naye daima. Wakati yeyote anapoamua kutenda kinyume naye na
kubaki mbali sana naye, sio kwa maana mtu huyo hajihisi kupendwa, bali ni kwa
sababu anajiona mwenye uhuru. Kama huu ni uzoefu wa upendo wa Baba: huu ni wa
hiari na kuuzaa uhuru. Sisi pia tunahisi mbali sana na Mungu wakati sisi
hutenda kinyume naye, yaani, tunapomkosea. Yeye anajihisi ameachwa na kusalitiwa,
lakini haachi kutupenda. Kama yule baba, Mungu anashughulika sana na maisha
yetu. Anakuja kututafuta ili kutupa sisi ulinzi na utunzaji wake. Kwa hivyo
tunahisi majuto na kivutio cha kuishi tena uzoefu wa ushirika tumeopoteza. Ingawa
mara nyingi tunakataa utambulisho wetu wa wana, kwa dhambi zetu, Mungu haukatai
utambulisho wake wa Baba kamwe.
Katika mfano huu yuko pia mwana
mkubwa ambaye hajihisi mwana, kwa sababu anajiona kuwa ni mfanyakazi, wala hajihisi
ndugu, kwa sababu anamkataa ndugu yake mdogo. Tabia ya huyo mwana mkubwa inaizuia
furaha kamili ya Baba na ukamilifu wa sikukuu. Kumrudia Mungu ni maana ya
furaha kubwa kwake. Lakini furaha yake haiwezekani kuwa kabisa ikiwa
hatushiriki katika hisia zake kuhusu wengine. Hataki kwamba tuwe na wivu kuhusu
njia yake ya kupenda; anataka kwamba tutende kama yeye alivyo. Kwa hivyo Yesu
alisema, “Muwe na huruma kama Baba yenu alivyo.” Upatanisho na wengine ni
kipimo ili uhusiano wetu na Mungu uwe kweli. Hii ni njia ya kweli ya toba iliyo mwendo wa muda mrefu na huanza mioyoni mwetu. Kupitia Ekaristi hii, turuhusu kuguswa na huruma ya Mungu ili tuweze kuwa vyombo
vya huruma hii kwa wale wanaohitaji msamaha wetu.
Fr Ndega
Mapitio na marekebisho: Serah
Nenhum comentário:
Postar um comentário