Kutafakari kuhusu Lk 14: 25-33
Umati wa watu waliandamana na Yesu, lakini sio
wote waliokubaliana naye. Alipoitambua hali ya kutokuwa na ahadi na makubaliano,
aligeuka, akiwakazia macho na kuzungumza nao. Maneno yake yalikuwa nafasi ya
kutafakari kwa kweli maana ya safari yao. Ingawa Yesu alikuwa maarufu, kwa
sababu ya mambo mema kwa ajili ya watu, utume ambao Yesu alichukua kutimiza
mapenzi ya Mungu hauleti umaarufu. Watu walichanganyikiwa kuhusu Yesu kwa sababu
hawakumjua bado na kumfuata kwa njia yoyote. Kama Yesu hakuwa na nia ya
kumdanganya yeyote, aliongea nao kwa uwazi sana kuhusu maana ya kumfuata na
matokeo ya uamuzi huu. Kusema hivyo kulikuwa tabia yake ya kawaida kama
alivyofanya kwa ajili ya wale kumi na wawili, yaani aliwajulisha masharti ili wawe
wanafunzi wake wa kweli. Kutoka kwao, Yesu hakutarajia werevu ama upumbavu,
bali kupatikana na hatia. Hawawezi kumfuata Yesu kwa sababu walipokea habari tu
ya kuwa ni vizuri kufanya hivyo. Yesu anatarajia zaidi, mabadiliko ya ndani.
Andiko hili ni mwaliko wa kuchukua ahadi ya
kumfuata Kristo kwa kupanga mambo ya kesho, yaani kuwa na uwezo wa kuona mbele
ili kutenda vizuri ama Kuwa na utoaji ili kuepuka kufaragua. Ni vizuri kuota
ndoto lakini ndoto hii inapaswa kuihusu hali halisi mtu anayoishi, vinginevyo
itakuwa udanganyifu tu. Yesu anataka kuepuka kwamba safari ya wafuasi wake iwe
pasipo maana ama udanganyifu. Ni lazima utambuzi, hekima, kupanga na uamuzi. Mungu
mwenyewe anatupa mfano wa kuwa na mipango ya muda mrefu ili tupate mafanikio
katika safari yetu kama wafuasi wa Yesu. Yeye Mungu alipanga kumtuma mkombozi
ndiyo maana miaka ilihesabiwa kwa kurudi nyuma maneno kabla ya Kristo (K.K)
kuzaliwa yakitumika. “... wakati maalum ulipotimia, Mungu alimtuma Mwanawe
aliyezaliwa na mwanamke... ili apate kuwakomboa waliokuwa chini ya sheria.”
(Wagalatia 4: 4-5). “Hata baadhi ya wakulima hutegemea mvua inyeshe hata kama
hawajaandaa shamba mahali pa kupanda mbegu kama za mahindi au maharagwe.”
Kupanga mambo ya kesho ni muhimu.
Yesu alisema, “Basi, kadhalika kila mmoja wenu
asiyeacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.” Kama ilivyotekea
katika vifungu vingine, Yesu aliwapendekezea watu mpango wa maisha nao mpango
huu unajumuisha kujinyima, kwa sababu yeyote anayekutana na Yesu kwa kweli
amekwisha pata hazina ya kweli kwa maisha yake wala hawezi kubaki alivyo, yaani
mambo mengine hayana maana tena. Kwa maneno mengine, Yesu anataka kuwa
kipaumbele maishani mwa wanaoamua kumfuata. Hakuna jambo lingine ambalo liweze
kuitoa maana ya kweli kwa maisha yao ila Yesu mwenyewe. Wanafunzi wa Yesu wa
kweli walimtegemea Mungu katika mambo yote kama Yesu alivyo. Yeye alishiriki na
wanafunzi wake ufalme wa mbinguni na kuwajulisha njia ya msalaba ili waweze
kufanya mapenzi ya Baba yake. Kupitia njia hii, tunatambua kwamba Kumfuata Yesu
hakuuleti upendeleo au hadhi, bali mateso na kujisalimisha kwa ajili ya ufalme
wa Mungu. Basi, yeyote ambaye anataka kuishi shwari na bila ahadi hawezi
kumfuata Yesu. Tena yeyote ambaye anatamani kumfuata Kristo bila msalaba
hatamfuata Yeye kwa kweli kamwe.
Kupitia njia ya
unyenyekevu na utupu Yesu alipata utukufu. Kupitia njia hii utambulisho wa
wanafunzi na mwalimu Yesu unatokea. Kwa upande wa Kristo msalaba ulikuwa sehemu
muhimu katika mwendo wa kufanya mapenzi ya Mungu na kudhihirisha mpango wa
upendo wake. Kwa upande wetu kama wanafunzi, kuchukua msalaba ni ishara ya
utayari wetu kwa kuruhusu kuongozwa na Mungu na kuyakaribisha mapenzi yake kwa
maisha yetu. Kwa kufikia lengo hili tunapaswa kujikana nafsi yetu, yaani kujisahau
sisi wenyewe ili wengine waweze kukumbukwe. Tunapaswa kujikana ili Mungu aweze
kujifunua kwa nguvu yote ya upendo wake. Kujiondoka kutoka katikati/mahali
muhimu ili wengine waweze kuwa na nafasi zaidi. Kwa maneno mengine, tunapaswa kuwafikiria
wengine kuwa wamuhimu zaidi kuliko sisi wenyewe. Kama haiwezekani kumfuata
Kristo bila msalaba, mfano wake wa uaminifu kwa mpango wa Mungu utuimarishe ili
tuchukue msalaba wetu wa kila siku, kumfuata kwa uaminifu na kufanya mapenzi ya
Mungu.
Fr Ndega
Mapitio na marekebisho: Serah
Nenhum comentário:
Postar um comentário