Mostrando postagens com marcador UPENDO. Mostrar todas as postagens
Mostrando postagens com marcador UPENDO. Mostrar todas as postagens

domingo, 21 de maio de 2017

UPENDO WA KWELI UNAONYESHWA KWA ISHARA HALISI


Kutafakari kutoka Mdo 8,5-8.14--17; 1Pt 3,15-18; Yoh 14, 15-21


        Maandiko haya yanaanza kuongea kuhusu kazi ya Roho Mtakatifu aliye upendo wa Baba na Mwana naye anatolewa ili aandamane na kazi ya jumuiya ya wanafunzi wa Yesu ili wapate kujua kamili kuhusu ufunuo wake. 
         
        Kulingana na somo la kwanza baada ya mateso dhidi ya Kanisa katika Yerusalemu, watumishi wengi walikimbilia maeneo mengine ili kuinjilisha. Shemasi Filipi alifanya kazi katika Samaria na kupata mafanikio, yaani Wasamaria walikaribisha neno la Mungu kwa furaha kubwa. Ishara za ajabu alizotenda Filipi zilithibitisha ukweli wa maneno yake. Pedro na Yohana walifunga safari kutoka Yerusalemu kwenye Samaria ili kukutana na Filipi kama ishara ya ushirika wa Kanisa zima, linaloongozwa na Roho Mtakatifu, limejaa matunda mengi kwa wokovu wa watu.

         Uinjilisti hauna mipaka na kulenga kuondoa ukuta wa utengo ambao hugawanya watu. Kazi hii inaimarishwa na Roho Mtakatifu aliyetolewa sio kwa uzoefu umefungwa wa kikundi kimoja tu bali ni zawadi kwa wote. Kupitia yeye waliomfuata Yesu wako tayari daima “kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yao”. Lakini hii ndiyo kazi ya kufanywa kwa upole na heshima ili mapenzi ya Mungu yakafanyike. Wamisionari ni vyombo tu. Kweli ndiye Mungu mwenyewe anayefanya kazi kwa Roho wake akisababisha mabadiliko na furaha kubwa maishani mwa watu.  

       Katika injili tunaendelea na hotuba ya mwisho ya Yesu. Yeye aliongea na wanafunzi wake moyo kwa moyo, akionyesha hisia zake za ndani kwa ajili yao. Hotuba hii inadhihirisha uhusiano wa ndani kati ya Yesu na Baba na pendekezo la Yesu kwa wanafunzi wake ili waweze kuwa ufanisi katika utume wao.  

         Aliposema, “mkinipenda, mtazishika amri zangu,” aliwaomba ahadi kwa ajili yake kwa njia halisi kwa sababu upendo ni halisi, yaani wakati mtu anaposema kwamba anapenda mwingine anapaswa kuonyesha ishara halisi ambazo zinathibitisha upendo huu. Ishara halisi Yesu anazotarajia kutoka kwa wanafunzi wake ni kupendana na kutumikiana kama Yesu alivyofanya. “Huu ni upendo ambao unamfanya mtu kuyatoa maisha yake kwa ajili ya wengine.”

         Yesu hatawaacha wanafunzi wake kama walio yatima bali ataendelea miongoni mwao kwa njia tofauti. “Hatakuwa nao kimwili, lakini wataweza kuuhisi uwepo wake kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu ataendeleza yale yote aliyowafundisha na kuwaongoza hadi kuelewa kikamilifu maana ya mafundisho ya Yesu katika wakati zao wenyewe. Sio watu wote walio tayari kupokea zawadi hii, bali ni wale mitume ambao waliandaliwa kuipokea katika maisha yao kwa njia ya Yesu. Mwombezi huyo ni “Roho wa Kweli” atakayetoa ushuhuda kwa Yesu na kuwaongoza mitume wake katika kweli yote.” Yeye ni pia Roho wa Umoja atakayehakikisha umoja wao hasa wakati wa mateso. Msemo fulani wa Kiafrika unasema: “umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu”.


        Ahadi ya Yesu ya kurudi kwa ajili yao inamaanisha kuendelea kuwepo, lakini kwa njia ya ndani, yaani kupitia upendo. Ndio upendo kati ya Yesu na wanafunzi wake ambao utawafanya watu wasadiki. Ndio kwa upendo ambao Mungu anatupa kwa Roho wake kwamba tunaweza kuendeleza kazi ya Yesu. Tunaishi katika ulimwengu ambao upendo umepoteza maana yake ya kiasili, yaani mtu anasema, ninapenda ikiwa naweza kuchukua nafasi juu ya mwingine” ama “napenda mpaka wakati fulani” ama “nawapenda baadhi ya watu tu, lakini sipendi wengine”. 

      Yesu anatuzungumzia sisi kuhusu upendo tofauti; ndio upendo wa kweli. Ukweli wa upendo huu unaonyeswa na uwezo wa kujitolea na kutumikia bila kufanya ubaguzi wa watu. Mtu anayependa kweli anataka tu manufaa ya mtu anayempenda. Ndio kwa upendo huu ambao Yesu anatualika siku ya leo. Huu sio upendo ambao unaniongoza kufanya lile ambalo linanipendeza tu bali unaniwezesha mimi kujisalimisha kwa ajili ya wengine. Ndio upendo ambao unatufanya kuacha ubinafsi wetu na kuenda kukutana na wengine katika mahitaji yao. Huu ni upendo ambao unafanya kazi yetu iwe ufanisi daima naye Roho Mtakatifu tu anayeweza kuuimarisha upendo huu mioyoni mwetu. Kwa hivyo, uje Roho Mtakatifu!   

Fr Ndega

sexta-feira, 24 de junho de 2016

ALISAMEHEWA KWA SABABU ALIPENDA SANA

Kutafakari kuhusu Lk 7:36-8,3



     Tukio hili la mwanamke mwenye dhambi lilitokea humo nyumbani kwake Simoni Mfarisayo, aliyemwalika Yesu kula chakula. Yesu Alipokuwa mezani akila pamoja na wageni wengine mwanamke huyo anayefahamika kama mwenye dhambi akatokea na kuanza kumkaribia Yesu akimwonyesha ishara za upendo na shukrani kwa sababu aliuona msamaha na upendo wa Mungu katika hali yake ya dhambi. Ingawa Simoni alichukwa ahadi ya mwaliko, ni Yesu mwenyewe aliyetaka kukutana na Simoni na kumwongozea njia mpya ya kuishi. Kwa kweli Simoni alihitaji njia mpya, mtazamo mpya na kadhalika. Alimwalika Yesu lakini hakujua jinsi ya kumkaribisha vizuri. Yeye alisahau ishara za msingi kama zilivyokuwa desturi miongoni mwa Wayahudi, yaani, hakumpa Yesu maji kwa miguu yake; hakumbusu Yesu akionyesha kwamba alipendezwa na kutembelea kwake; hakumpaka kichwa chake Yesu mafuta.

      Katika injili ya Luka, Yesu anapenda kushiriki pamoja na watu katika chakula. Kwa kushiriki milo na watu wa aina na ngazi zote katika jamii, Yesu alionyesha kuwa yeye alikuwa wa watu wote, matajiri na maskini pamoja. Tukumbuke wakati alipokula chakula nyumbani kwake Mathayo pamoja na wenye dhambi wengi; tukumbuke pia wakati alipojikaribisha mwenyewe kwa karamu nyumbani mwa tajiri Zakayo. Kutembelea kwake Yesu kunasababisha mabadiliko maishani mwa watu kuwaongoza kufikiri na kutenda tofauti. Katika injili ya leo, ingawa alikuwa Simoni ambaye alimwalika Yesu nyumbani kwake, ni mwanamke fulani ambaye alimkaribisha vizuri. Mwanamke huyo ingawa hana jina, yaani heshima, hata hivyo ana ishara ambazo Yesu alitarajia kukuta kutoka kwa Simoni aliyejiona amejaa heshima. Mtazamo wa upungufu wa Simoni uliona kwanza udhaifu na makosa ya mwanamke. Lakini Yesu alimwalika Simoni kuona vizuri, akisema, “unamwona mwanamke huyo?” Huu ni mwaliko wa kuanza tena na kuona tofauti, kama Yesu mwenyewe alivyo. Yesu anajua dhambi nyingi za mwanamke huyo, hata hivyo anatambua kwanza ishara nyingi za upendo ambazo zinashinda udhaifu wake. Kwa upande wa Yesu upendo unashinda dhambi naye mtu anathamini zaidi kuliko makosa yake.  

         Katika mazingira yale, Simoni ni mmoja miongoni mwa waliojiona kuwa wenye haki na kwa hivyo, walijiona pia kwa mamlaka ya kuwachagua baadhi ya watu na kuwakataa wengine. Yesu anaukubali mwaliko wa Simoni, lakini haukubali mwelekeo wake wa kumhukumu mwanamke aliye miguuni mwake. Yesu anataka kwamba Simoni atambue kuwa mgawanyiko kati ya watu wazuri na wabaya haukubaliki mbele ya Mungu. Katika njia ya Mungu ya kutenda ubaguzi hauko. Pendo na huruma yake yapatikana kwa wote. Kwa hivyo Yesu alimsamehe mwanamke huyo na kupendekeza toba kwa wengine. Hili ni sharti ili huruma ya Mungu iwe ufanisi maishani mwao. Kama hivi Yesu alitangaza ufalme wa Mungu na wale ambao walimfuata waliruhusu kuguswa na huruma ya Mungu. Ni jambo la ajabu kwamba injili hii inaanza kwa mwanamke bila jina na kuhitimisha kwa majina kadhaa ya wanawake, yaani, Mariamu, Yohana, Susana na wengine wengi waliopokea tena heshima yao kwa sababu ya mkutano na Yesu na huruma ya Mungu.


      Kama ilivyotokea kwa mwanamke huyo, sisi pia tunaalikwa kujiona kukaribishwa na kubadilishwa kwa sababu ya mkutano na huruma ya Mungu hasa kupitia uzoefu wa sakramenti ya kitubio na upatanisho. Uzoefu huu tena unatusaidia kuushinda mwelekeo wetu wa kibinadamu wa kuwahukumu wengine na kuuona makosa yao kuliko tabia zao nzuri. Wakati tunapowahukumu tunajiona wenye haki, yaani tunajiona bora kuliko wengine. Je, ni nani aliye mwenye haki mbele ya Mungu? Tunaalikwa kuweka juhudi zaidi ili tuweze kuwaona wengine kwa mtazamo wa Yesu. Kama ilivyotokea katika tukio la mwanamke, Yesu anaona upendo wetu kwa kanisa, kwa jumuiya, kwa familia juu ya yote. Nao upendo wetu unaonyeshwa kupitia uzoefu wetu wa kusamehe, wa kuwakaribisha wengine vizuri na kuwatendea mema. Kusamehe ni asili ya Mungu (Kut 34:6). Hatuununui msamaha wa Mungu kwa mapendo yetu bali tunaupokea kwa hiari. Ekaristi hii takatifu itusaidie kupenda na kusamehe kama Mungu alivyo. 

Fr Josuel Ndega
Mapitio na marekebisho: Sarah

segunda-feira, 11 de abril de 2016

ANATUONYESHA NJIA BORA YA KUTENDA, KUTUTUMIKIA NA KUTUALIKA KUMFUATA


Kutafakari kuhusu Mdo 5,27-32.40-41; Ufu 5, 11-14; Yoh 21, 1-19

         Huu ni mwaliko wa kukutana na Bwana Mfufuka na kumtambua kama upendo ambao unaitoa maana kwa maisha. Ishara anazoonyesha Bwana huyo ni alama ya kwamba yeye anaijua hali yetu na kunampendeza kushiriki katika shughuli zetu za kila siku. Yeye anatuonyesha njia bora ya kutenda, kututumikia na kutualika kumfuata kwa upendo ambao ulionyeshwa kupitia utumishi wa ndugu. Somo la kwanza linatuambia kwamba ni lazima kupatikana na hatia kwa kumtii Mungu kuliko wanadamu, kulingana na ushuhuda wa Petro na wafuasi wengine. Ni Roho Mtakatifu ambaye aliwaimarisha wafuasi wa kwanza wakubali kuaibishwa na kuteseka kwa ajili ya jina la Yesu. Tumepokea Roho huyo kwa kumtii Mungu na kuyatangaza mambo makuu yake bila hofu, kupitia maisha yetu. Kulingana na somo la pili, Yesu yu Mwanaa-Kondoo aliyechinjwa na kuishi milele. Yeye anastahili sifa na heshima ya pekee kwa sababu kujitolea kwake kwa ajili yetu kulitufanya kushiriki katika utukufu wake na heri ya milele.

     Katika injili Yesu anatokea tena kwa wanafunzi wake. Baadhi ya walimu wa Kanisa wanasema kwamba sura hii ya ishirini na moja iliongezeka baada ya hitimisho la injili, kwa sababu, baada ya kupokea kutembelea kwa Kristo, wanafunzi kumi na mmoja waliimarishwa sana ili waendelee safari yao kama mashahidi wa Bwana mfufuka. Lakini, kulingana na andiko la siku ya leo, nambari ya wanafunzi ni saba. Ingawa namba saba katika Biblia inamaanisha ukamilifu, hali hiyo ya kikundi cha wanafunzi wa Yesu haikuwa kamili. Kikundi chao kimevunjika na kukosa lengo. Hakuna kitu kingine cha kufanya ila kuvua samaki bila mpango kama walivyofanya kabla ya kukutana na Kristo. Inaonekana kwamba kupita kwa Yesu katika maisha yao hakusababisha mabadiliko yoyote. Walitenda wakati wa usiku bila kupata kitu.  Kwa kweli walitenda bila Kristo na matokeo ni kukatisha tamaa. Asubuhi inawaletea zawadi kubwa, yaani, uwepo wa bwana Mfufuka. Bwana huyo aliwasalimia kama rafiki aliyejulikana sana, lakini wanafunzi hawamtambui kwa sababu ya kuchoka kwa kazi bila mafanikio. Tena aliwaalika kuibadili njia ya kuvua samaki, yaani, kuubadilisha mwelekeo wa maisha yao. Baada ya kuona tendo la ajabu, mwanafunzi aliyependwa anatambua kwamba hakuna mwinigine aweze kupendekeza jambo kama hili ila Bwana Yesu.

     Wanafunzi walitambua kwamba ni lazima kuwa macho kuhusu ishara za uwepo wa Bwana wao na kusikiliza tena yale anayosema kama mwongozo kwa mafanikio katika kazi yao. Mfano wa mwanafunzi aliyependwa na Yesu unatuhakikishia kwamba uzoefu wa upendo unafanya kuona mbele. Wakati wengine walimwona mtu mgeni tu ambaye aliwapendekezea mabadiliko ya upande wa mashua, yule aliyependwa aliona mbele na kutambua uwepo wa Bwana. Ni uzoefu wa upendo ambao unasaidia kuona tofauti na vizuri. Kujiona kupendwa ni kufanya uzoefu wa uwepo wa mtu, yaani uwepo ambao hauwaachi waliopendwa. Upendo ndio unajua, unakuja, unajali na kutumikia. Upendo ni mwaliko wa kubadilisha mawazo, tabia, mwelekeo, njia, kila kitu. Hii ndiyo maana ya kuvua samaki tofauti. Utayari wa kuvua samaki ulionyeshwa na Petro ambaye ni wa kwanza wa kujifunga vazi na kujitupa baharini, yaani alijifunga pendekezo la Kristo na kuchukua kazi kwa shauku na ujasiri kukabili upinzani wa kibinafsi na changamoto nyingi za uinjilishaji.


      “Je, unanipenda?” Petro alikiri mara tatu upendo wake kwa Yesu licha udhaifu wake. Kama ilivyotekea na Petro, hivyo Yesu anatuuliza swali sawa na kutarajia upendo wa kweli kutoka kwetu. Kwa upande wa Yesu ni muhimu utayari wetu kwa utumishi wake kwa uaminifu mpaka upeo. Upendo ndio maana ya utume wetu. Upendo tu unatusaidia kuona mbele na kumtambua Bwana katika hali isiyotarajiwa. Ikiwa huu ni haba hautatuongoza kwa kujitolea kabisa kama mwalimu wetu Yesu alivyo. Yeye amefufuka ili atuonyeshe kwamba kujisalimisha kwa upendo ni njia ambayo inamtukuza Mungu na kuendeleza kazi ya mwanawe. Kujitolea kwa upendo wa kweli kunaitoa maana kwa kazi yetu na vitu tu ambavyo vinafanyika kwa upendo vinadumu milele.    

Fr Ndega
Mapitio na marekebisho: Sarah

quarta-feira, 13 de maio de 2015

KUPENDA KAMA MUNGU ANAVYOPENDA


Mdo. 10: 25-26, 34-35, 44-48; 1Yoh. 4: 7-10; Yo 15: 9-17

     Mungu hawabagui watu kwa maana anapenda na katika upendo hakuna ubaguzi. Mungu anawakaribisha wale wanaomwabudu na wanaishi kwa udugu. Kuabudu na udugu ni uhusiano na wale ambao wanamwabudu kwa njia hii, wanaabudu kwa Roho na ukweli. Roho Mtakatifu aliwashukia wale ambao wakalisikiliza Neno la Mungu kupitia kinywa chake Petro, akidhibitisha kwamba Mungu anawatendea wote kwa usawa. Mbele ya Mungu hakuna mtu wa heshima zaidi kuliko mwingine. Mungu hakuzi upendeleo na hakubali umaarufu, bali anatarajia ahadi kwa njia yake ya kufikiri na kutenda. Maana kwa njia hii ni upendo wake wa uhuru kwa wote.      
      Mtakatifu Yohana katika waraka wake anawaalika watu kupendana kwa sababu upendo kutoka kwa Mungu na wale wanaopenda wanamjua Mungu. Basi, kupenda ni kujua. Kujua katika Biblia si uzoefu wa akili, lakini ni uzoefu wa ndani. Mungu anajua kwa sababu anapenda. Kumjua Mungu ni kumpenda, kufanya naye uzoefu wa ndani. Mungu ni upendo na aliwapenda sana wanadamu kwamba alimtuma Mwanawe pekee kama maonyesho makuu ya upendo huu ili kuwafundisha watu jinsi ya kupenda kwa kweli. Kutokana uzoefu huu tulipata maisha kwa maana upendo tu unayazaa maisha na wale ambao wanakubali kuhusishwa katika uhusiano wa upendo kati ya Baba na Mwana, wanaishi maisha mapya.
      “Mwana alitupenda kama Baba anavyompenda”. Andiko hili la injili ni sehemu ya ujumbe wa maagano ya Yesu. Yaliyomo ya ujumbe huu ni urithi wake Mwalimu, aliokuwa na kama muhimu zaidi ili kuacha kwa wale ambao lazima waendeleze kazi yake. Umuhimu wa mafundisho ya Yesu ni kupenda. Upendo una chanzo chake katika Mungu kwa sababu Mungu ni upendo na anampenda Mwana. Uwepo wa Mwana miongoni mwa wanadamu uliufanya upendo huu kujulikana. Upendo ni ndani ya Mungu; ni maana ya ushirikiano wake. Wanadamu ni matokeo ya ushirikiano huu na wanaalikwa kujihusisha katika ushirikiano huu sawa, kukaa katika upendo wa Kristu. Kigezo ili kukaa katika upendo wake ni kuishi mafundisho yake, ni kwamba, kupendana kama alivyotupenda na akajitoa kwetu. Yesu halazimishwi kutupenda. Upendo wake ni maonyesho ya furaha yake yote: furaha ya ushirikiano wake na Baba, furaha ya kuwa miongoni mwa wanadamu, furaha ya kuwachagua wanadamu kama washirika katika kazi yake, furaha ya kuutoa uhai kwao. Kuushiriki upendo wake nasi, Yesu anayajaa maisha yetu kwa furaha kubwa kwa sababu kwa yeye upendo na furaha inatembea pamoja. Kama hii, mtu tu anayependa kwa kweli ni wenye furaha ya kweli.  
      Upendo ni maana ya wokovu wa ulimwengu, kwa sababu ilikuwa kwa upendo kwamba Mwana wa Mungu aliutoa uhai wake. Kulingana na Yesu thamani ya urafiki wa kweli hupimwa kwa uwezo wa kuyasalimisha maisha kwa upendo. Yesu ni rafiki yetu kwa sababu alifanya hivyo vizuri sana. Alituchagua na alituteua kuenda na kuyazaa matunda, na matunda yanayodumu. Tutakuwa marafiki zake ikiwa tuna ujasiri wa kupenda kama yeye alivyopenda. Anajitambua na wale wanaotumwa katika jina lake. Utambulisho huu ni matokeo ya upendo wake ndani yetu kwa sababu ni sahihi/tabia ya upendo kuumba utambulisho na hisia ya miliki. Ikiwa tunakaa pamoja naye tutakuwa watu wa ushirika na tutaweza kusaidia ushirika katika jumuiya zetu. Huu ni ushahidi wetu  wa kwanza: Mwone kama wanavyopendana”! Ilikuwa maoni kuhusu Wakristu wa Kwanza. Upendo wao ulionyeshwa kupitia ridhaa wao kwa wao, kushiriki pamoja, uvumilivu katika maombi pamoja na unyenyekevu wa moyo. Je, maisha yako ni maonyesho ya yale wewe huamini? Itawezekanaje jumuiya zetu kuonyesha hali halisi hii ya Jumuiya za Kwanza?
      Badala ya kuuzaa ushirikiano katika jumuiya, upendo hutufungua kwa watu wengine nje, wanaohitaji kukaribishwa pia. Wale wanaopenda kweli hawabagui watu na ni makini kwa hali halisi maalum, kujifunza kutoka kwa Mungu, anayewapenda wote, lakini anapendelea maskini na wale hawana nguvu. Kama hii pia mama, anawapenda watoto wake wote, lakini ana utunzaji maalum kwa mtoto mgonjwa. Basi, tufikiri kuhusu upendo wetu kwa wale wanaohitaji zaidi katika jumuiya.    

Fr Ndega
Mapitio: Sara

sexta-feira, 7 de novembro de 2014

UMUHIMU ZAIDI WA MAISHA



Kutafakari toka Kutoka 22, 21-27; 1Thes 1, 5-10; Mathayo 22, 34-40

       Kulingana na Maandiko, Mungu ana uhusiano maalum na watu wa Israeli. Anaanzisha agano na watu hao kuwapa miongozo kadhaa ili watende vyeme, kuhifadhi maisha yao. Ni katika hali hiyo kwamba Amri ziliibuka/patikana. Kuishi katika Amri kumekuwa umuhimu zaidi katika safari ya Watu wa Israeli kwa ambao Sheria ni Neno la Mungu na Neno la Mungu ni Sheria. Wakati wao husema “Sheria ya Mungu ni kamilifu, faraja kwa roho”, wanamaanisha kwa Neno la Mungu. Kuna uwiano wa kina kati ya Sheria na Neno, kwa sababu amri za Sheria zinaonyesha huduma ya upendo wa Mungu anayeongea kuonyesha njia za ukombozi na kisha zinadhihirisha pia utambulisho wa kweli wa watu ambao wanatii, kukuza hisia za miliki ya Mungu wao. Utiivu kwa amri ni chanzo cha baraka kinachoelekeza kwa uhai, wakati uasi kwa hizo unaelekeza kwa kifu. 
       
     Katiku Sheria kuu, Wayahudi wameweka sheria nyingi kwamba hatimaye zilibadilisha lengo kutoka iliyokuwa muhimu zaidi. Amri kumi za awali zilikuwa mia sita kumi na tatu. Watu maskini walichukuliwa wenye dhambi kwa sababu hawakuweza kukariri amri hizi zote na kwa hiyo, hawakuziweka vitendoni. Hata hivyo, sehemu hii ya idadi ya watu walijua na walikuza umuhimu zaidi wa Sheria. Hilo ni jibu la Yesu anaposema: “upende Bwana Mungu wako na moyo wako wote, na akili yako yote, na nguvu zako zote” (Dt 6: 4-5) “na jirani wako kama unavyojipenda mwenyewe” (Lev. 19: 18).     
         Kumpenda Mungu ni amri ya kwanza ya zote, lakini Yesu aliiunganisha na upendo kwa jirani, kuonyesha kwamba haiwezekani kumpenda Mundo bila kumpenda jirani. Yakobo katika waraka wake anamfikiria kama mtu mwongo anayesema kwamba anampenda Mungu na hampendi jirani. Kutoka amri ya kumpenda Mungu inabubujika kumpenda jirani kama matokeo. Chanzo ni Mungu daima kwa sababu alikuwa aliyetupenda wa kwanza. Ni kutokana na upendo kwamba Mungu anao kwetu – kwa njia ya ukarimu na bure – ambayo inawezekana kuwapenda wengine na uhalisi. “hiyo ni changamoto kwa tamaduni zote ikiwa ni pamoja na  hizo katika Afrika, ambapo uaminifu kwa familia na mila unakuzwa mara nyingi kama amri ya kwanza.”       
      Yesu aliyefanika mwili, ni upendo wa huruma wa Mungu na maisha yake yakasalimika kwa wote yanaonyesha kwamba kupitia upendo tu binadamu anaweza fikia mafanikio yake binafsi. Bila shaka, kwamba kuwa ndani ya dini na ushiriki misani ni ishara ya upendo kwa Mungu kama kipaumbele katika maisha yetu. Hata hivyo, katika mwisho wa maisha yetu ombi letu halitakuwa “Je, ulikuwa wa dini gani?” au “Je, mara ngapi ulienda misani?”, lakini swali kamili litakuwa, “ulikuwaje upendo wako kwa wengine?” kiwango cha upendo wetu kwa Mungu kinaonyeshwa katika njia kama tunavyowapenda wengine. Anapenda kweli mtu ambaye anatamani tu wema kwa mtu mpendwa, hata kama hastahili. Hivi ndivyo Mungu anavyotupenda, kwa ukarimu na bure. Uzoefu huu lazima utuongoze kufanya anavyofanya. 
      Muhimu zaidi kwa Yesu ni kumpenda Mungu, kupenda pia jirani. ufundishaji wake wa ajabu yako ulifanya amri hizo mbili hata kupatikana zaidi, akitoa ushauri kwamba inatosha tupendana kama alivyotupenda. kama vile Mungu ametupenda katika Kristu, sisi lazima tupende kutoka kwa Kristu. Yeyote anayependa katika njia hiyo amefahamu umuhimu zaidi wa Sheria na maisha, kwa sababu yeyote anayefuata Yesu hafuati sheria au mafundisho, lakini anafuata Mtu.
    Kwa hiyo, kigezo tu Wakristu wanacho kushuhudia upendo wa Mungu duniani ni kupenda wengine kama ndugu. Tunampenda Mungu wakati tunampa mahali pa kwanza katika maisha yetu, kutafuta kwanza ufalme wake na haki yake, wakati sisi ni waminifu katika sala zetu kila siku, tunaposhiriki kwa makini katika sherehe ya sakramenti. Sisi huonyesha upendo kwa jirani wakati tunaweza kuhisi huruma mbele ya hali halisi ya huzuni na mateso ya wengine na tunapatikana kuwasaidia katika mahitaji yao. Katika maana hii, ilisemwa kuhusu Jimuiya za kwanza: “Oneni wanavyopendana”. Hata hivyo, iliwezekana tu kwa sababu walibaki pamoja katika upendo wa Mtu aliyewaita. Hitaji hilo lingalipo katika siku zetu na linaaminisha nguvu za uhai ya kazi yetu kama Wakristu.    

Fr. Ndega
Mapitio: Mwalimu Patrick