Kutafakari kutoka 2Sam 7: 1-5.8b-12.14a.16; War 16: 25-27; Lk 1: 26-38
Sisi tuko karibu
sana kwa kusherehekea tukio kuu ambalo linaleta mafanikio ya mpango wa Mungu
kwa dunia, yaani, Kuzaliwa kwa Yesu. Ndio wakati maalum wa kufungua moyo ili
kukaribisha na kushukuru, kwa sababu Mungu anaonyesha upendo wake mkuu kwetu, kwa
kufanya makao kati yetu na kuleta wokovu kwetu. Wokovu ni kazi ya Mungu, lakini
yeye hakutaka kuifanya peke yake; alipendelea kuuomba ushiriki wa binadamu.
Bikira Maria ndiye mmoja wetu aliyejibu kwa mwaliko wa Mungu kwa upatikanaji
kabisa. Uamuzi wa Mungu wa kumchagua mwanamke huyo mnyenyekevu unaonyesha
kwamba njia yake ya kutenda ni tofauti na yetu.
Katika
andiko la kwanza, tuko na andiko la kitabiri nje ya maandiko ya manabii. Bwana
Mungu anaonyesha hamu yake ya kukaa miongoni mwa watu wake lakini ana njia yake
mwenyewe wa kufanya hivyo. Kupitia ukoo wa Daudi, atamtuma mfalme mpya ambaye ataanzisha
ufalme imara na milele. Utabiri huu ulitimiza katika Kristo ambaye tangu mwanzo
wa maisha yake ya kidunia, alichukua ahadi na historia yetu na kujitambulisha
na hali yetu. Yeye ndiye Mungu pamoja nasi. Paulo anajiona mjumbe mwaminifu wa
injili ya Yesu Kristo ambaye alitabiriwa na manabii wote. Yeye ndiye ufunuo
mkuu wa upendo wa Mungu na kupitia yeye watu wote wanaalikwa kumwamini Mungu na
kukubali mipango yake katika maisha yao.
Andiko la Luka
hili linajulikana kama andiko la “Kupasha habari”. Ndilo tangazo la kuzaliwa
kwa Yesu Kristo aliye utimizaji wa ahadi za Mungu za Agano la Kale. Ndiye
Masihi aliyetarajiwa kwa muda mrefu na alikuwa hali halisi duniani kupitia
Bikira Maria. Makaribisho yako yalikuwa maalum kwa sababu aliishi matarajio ya
ujio wa Masihi kulingana na mapenzi ya Mungu na kabla ya kuzaa Yesu katika
tumbo lake, yeye alimzaa moyoni mwake.
Kama mwanamke
mwangalifu, alikuwa makini sana kwa hali ya dunia na mahitaji ya wanadamu.
Aliikataa mipango yake ya kibinafsi kama kijana ili aishi mpango wa wokovu wa
Mungu. Mariamu alipata kuishi wito wake kupitia kusikiliza Neno la Mungu na kutenda kulingana na neno hili kama tabia yake ya kawaida.
Mwinjilisti Luka anaongea kuhusu tabia hii akisema, “Mama yake aliyaweka maneno
hayo yote, akiyafikiri moyoni mwake”.
Hivyo, neno la kwanza la malaika ndio mwaliko
wa furaha kwa sababu maisha ya Bikira Maria yalimpendeza Mungu. Mariamu alishangaza
maana ya habari hii kwako kwa sababu ya unyenyekevu wake lakini yeye aliandaliwa na Mungu na kusaidiwa na neema yake kwa
ajili ya kuwa Mama ya Mwokozi. Tangazo la Malaika Gabrieli lilimwomba Mariamu uthibitisho
wa “ndio” ambayo yeye aliishi kama tabia ya kawaida.
Hivyo,
kama Mungu alitarajia jibu la ukarimu Bikira Maria alijibu kwa njia kamili.
Katika udogo na unyenyekevu wake tunaweza kuona ukuu wake, kulingana na maneno
yake mwenyewe: “Mungu anamwangalia mtumishi wake katika unyenyekevu wake...
watu wote wataniita amebarikiwa (Lk 1,48).” Maisha na chaguzi za Mariamu ni
tangazo kuu la maajabu ya Mungu. Kulingana na maisha yake, mtu ambaye huamini
katika ahadi ya Mungu ni mwenye furaha, kwa sababu Mungu anayeahidi ni
mwaminifu.
Maisha ya Bikira
Maria yanashuhudia kwamba Mungu hahitaji matukio makubwa kwa kujifunua
mwenyewe. Anakuja kututembelea katika maisha yetu ya kawaida naye ana mpango wa
upendo kwa kila mtu. Anachukua nafasi ya kutualika kama washirika katika kazi
zake na kutupa uwezo kwa kumjibu kwa upatikanaji kabisa kama Bikira Maria. Mungu
ndiye mwaminifu kwetu kama alivyokuwa kwa Bikira Maria. Furaha yetu ilianzishwa na uaminifu wake. Tunamshukuru Mungu
kwa tendo lake katika maisha yetu kwa njia ya Bikira Maria. Ukarimu na
upatikanaji wake kwa mapenzi ya Mungu unatuimarisha katika jibu letu la kila
siku kwa mwaliko wake na kutualika tuwatumikie wengine kwa furaha na shukrani
kama maonyesho halisi ya jibu letu la ukarimu.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário