Kutafakari kutoka Is 40, 1-5, 9-11; 2Pt 3, 8-14, Mk 1, 1-8
Maandiko haya yanatualika kuandaa
njia ya Bwana kupitia safari
ya kutubu, kwa kukubali mapendekezo ya Neno la Mungu na kutangaza habari njema kutoka uzoefu wa Neno
hili. Wale ambao waliongea kwa jina la Mungu walikuwa watu waliobadilishwa na Neno
hili kwa njia ya ndani na kwa hivyo, walikuwa mashahidi
wa kweli. Mtu anaweza kuwasaidia wengine watubu ikiwa yeye anaweza kuchukua kwa
umakini njia ya kutubu kwa nafsi yake kwanza.
Nabii Isaya alitabiri kuhusu wakati mpya kwa watu waliokuwa wakiteseka uhamishoni mwa Babeli na kuutarajia ukombozi. Mungu hakuwasahau watu wake na kutaka waonje hali
mpya. Hata hivyo ni lazima kuandaa njia ya
Bwana, yaani, maisha yao wenyewe. Kama kosa la uaminifu kwa Mungu lilisababisha
uhamisho, hakuna njia nyingine ya kuona maisha mapya ila uzoefu
wa huruma ya Mungu kwa kupitia kutubu. Mungu anaonyesha enzi yake hasa
anapoonea huruma. Hivyo, utukufu wake unadhihirishwa zaidi wakati
tabia yetu yabadilika kwa sababu ya mkutano na huruma hii. Hii ndiyo
habari nzuri ambayo yapaswa kutangazika.
Kwa watu
ambao walikatisha tamaa na kushindwa kuwa na matumaini kwa sababu ya kuchelewa
kwa ujio mkubwa wa Bwana, Petro aliwaelekeza maneno ya faraja
na ya kutia moyo akiwaomba waendelee wakisubiri ujio wa
Bwana kwa macho na kujitolea kwa manufaa ya jumuiya.
Kulingana na Petro, Mungu ni mvumilivu
na mwenye huruma. Hivyo, yeye hataki kuwaadhibu watu, bali atarajia waweze kutubu na kuokolewe.
Miongoni
mwa wainjilisti ndiye Marko peke yake ambaye
anaingiza injili yake kwa kutumia maneno
Habari njema wakati anapoongea kuhusu
Yesu. Maneno haya habari njema
yalijulikana wakati wa Yesu, lakini hayakutumia kwa maana ya kidini; yalitumia ili
kutangaza habari ya furaha, mfano, kuzaliwa kwa mfalme ama ushindi wake juu ya
maadui yake ama tena kutembelea kwa mfalme huyo kwenye sehemu fulani ya ufalme
wake. Tangazo la habari hii lilileta matarajio ya mabadiliko ya hali, lakini
baadaye mambo yote yakaendelea kama kawaida.
Nia ya
Marko ndiyo kujibu swali kuhusu utambulisho wa Yesu, yaani, Yesu ni nani? Kweli
katika mwanzo na mwisho wa injili hii tunakuta maneno ‘Mwana wa Mungu’ kumhusu
Yesu na mambo yote ambayo Yesu anatenda katika injili hii yaonyesha kwamba Yesu
anatoka kwa Mungu kweli. Basi, kulingana na Marko, habari inayoleta furaha ya
kweli kwa dunia hii ndiye Yesu aliye Mwana wa Mungu. Tofauti na tangazo lingine
kuhusu wafalme, habari hii njema ya Yesu inaleta mabadiliko kwa dunia nzima kwa
sababu habari hii ni Yesu mwenyewe.
Habari njema ya Yesu inaanza kupitia kazi ya Yohana Mbatizaji, ndiye nabii mkuu, kulingana na Yesu mwenyewe. Yohana
anajulishwa kama mfano kwa wote kwa sababu alitumia nguvu zake zote ili kuwaandaa watu wakaribishe Mwana wa Mungu, ndiye Yesu Kristo.
Yohana aliishi katika upweke wa jangwa na kufunguliwa
kabisa kwa msukumo wa Mungu.
Katika mahali hapo alijifunza jinsi
ya kushuhudia habari njema za wokovu. Ndilo jambo la
ajabu tabia yake ya unyenyekevu hasa kuhusu mavazi na chakula.
Ukuu wa Yohana ulionyeshwa katika uwezo wake wa kutambua
ukuu wa Bwana, akijifikiria mwenyewe kama sauti tu
ambaye huandaa njia
ya yule atakayekuja. Katika
ujumbe wake, Yohana alitangaza huruma
ya Mungu akiwaalika watu watubu: “Mmrudie Bwana! Mungu atawasamehe dhambi zenu.” Pamoja
na maneno haya, Yohana aliwabatiza watu kama ishara
halisi ya kutubu na makaribisho ya huruma ya Mungu.
Sababu ya uaminifu wa ujumbe
wa Yohana ilikuwa sio maneno yake
tu, bali pia unyenyekevu wake na njia ya kweli ya kuishi. Hata bila maneno, maisha yake
yalikuwa tangazo la kweli la hali mpya ambayo Yesu alikuja kuleta duniani. Maisha
ya Yohane yatuambia kwamba tunaweza kufanya tofauti maishani mwa watu, lakini
ahadi haiwezekani bila uzoefu wa jangwa, yaani, uzoefu wa ndani wa Mungu na wa
Neno lake. Ndio kutoka jangwa kwamba pendekezo la mabadiliko linakuja kwetu.
Tukiishi uzoefu wa mabadiliko tunaweza kuwa mashahidi wa habari
njema kwa uaminifu kwa sababu ushuhuda wa maisha ndio
ufanisi kuliko maneno. Uvumilivu na huruma ya Mungu ndiyo nafasi tunayohitaji
ili tuweze kumrudia yeye na kuwa wajumbe wake wa furaha.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário