Kutafakari kutoka Mdo 8,5-8.14--17; 1Pt 3,15-18; Yoh 14,
15-21
Kutoka maandiko haya tunaanza kuongea kuhusu nafsi
na kazi ya Roho Mtakatifu aliye upendo wa Baba na Mwana ametolewa ili aandamane
na kazi ya jumuiya ya wanafunzi ili wapate kujua kamili kuhusu ufunuo wa
Mwalimu wao kuwa ufanisi katika ushuhuda wao hata kati ya dhiki.
Kulingana na somo la kwanza baada ya mateso
dhidi ya Kanisa katika Yerusalemu, watumishi wengi walikimbilia maeneo mengine
ili kuinjilisha. Kwa sababu ya kazi nzuri ya Filipi kwenye Samaria Wasamaria
wengi walikaribisha neno la Mungu kwa furaha kubwa. Ishara za ajabu alizotenda Filipi
zilithibitisha ukweli wa maneno yake. Pedro na Yohana walifunga safari kutoka
Yerusalemu kwenye Samaria ili kukutana na Filipi na kumsaidia kama ishara ya
ushirika na wa Kanisa zima, linaloongozwa na Roho Mtakatifu, limejaa matunda
mengi kwa wokovu wa watu.
Uinjilisti hauna mipaka na kulenga kuondoa ukuta
wa utengo ambao hugawanya watu. Kazi hii inaimarishwa na Roho Mtakatifu aliyetolewa
sio kwa uzoefu umefungwa wa kikundi kimoja tu bali ni zawadi kwa wote. Kupitia
yeye waliomfuata Yesu wako tayari daima “kumjibu kila mtu awaulizaye habari za
tumaini lililo ndani yao”. Lakini hii ndiyo kazi ya kufanywa kwa upole na
heshima ili mapenzi ya Mungu yakafanyike. Wamisionari ni vyombo tu. Kweli ndiye
Mungu mwenyewe anayefanya kazi kwa Roho wake akisababisha mabadiliko na furaha
kubwa maishani mwa watu.
Katika injili tunaendelea na hotuba ya mwisho ya
Yesu. Yeye aliongea na wanafunzi wake moyo kwa moyo, akionyesha hisia zake za
ndani kwa ajili yao. Hotuba hii inadhihirisha uhusiano wa ndani kati ya Yesu na
Baba na pendekezo lake kwa wanafunzi wake ili waweze kuwa ufanisi katika utume
wao. Aliposema, “mkinipenda, mtazishika
amri zangu,” aliwaomba ahadi kwa ajili ya mafundisho yake, yaani Neno lake.
“Neno haliwezi kupunguzwa kuwa amri, hilo ndilo zaidi ya amri. Neno linafanya
kazi ndani yenu mnaoamini (1Ts 2, 13), linaumba, linazalisha, linawasha, linaufungua
upeo, linaziangazia hatua, linapanda uhai mashambani mwa maisha.”
Ugumu wa kufahamu maana ya ndani ya mafundisho
ya Mwalimu na kosa la ushirika kwa hisia zake (“Ikiwa mngalinipenda
mngalifurahi...” – Yoh 14, 28) linafanya moyo yao uwe na huzuni. Kisha, Yesu
kama kawaida anawasaidia kwa sababu ya magumu yao na kuwaimarisha kwa kuongelea
ujio wa Roho Mtakatifu maishani mwao. Roho huyo atatenda kama Msaidizi kwa
sababu ana jukumu la kutia moyo, kulinda, kufanya maombezi kwa ajili yao.
Lakini andiko linampa Roho Mtakatifu maneno ya
“Msaidizi mwingine”, kweli ni kwa sababu ndiye Yesu Msaidizi wa Kwanza. Tendo la
Roho litawaongoza hadi kuelewa kamili mambo yote Yesu aliyoyatenda na kuyafundisha
kama maonyesho ya upendo wake kwa hiari na kwa jumla ili kwa kupitia uzoefu wa
kupendana wao kwa wao waweze kuuonyesha uwepo wa Yesu kwa wengine. Hivyo, Roho
anatenda ili Yesu akae ndani yao nao upendo wao unamwonyesha kwa wengine.
Tunaishi katika ulimwengu ambao upendo
umepoteza maana yake ya kiasili, yaani mtu anasema, ninapenda ikiwa naweza
kuchukua nafasi juu ya mwingine” ama “napenda mpaka wakati fulani” ama
“nawapenda baadhi ya watu tu, lakini sipendi wengine”. Yesu anatuzungumzia sisi
kuhusu upendo tofauti; ndio upendo wa kweli. Ukweli wa upendo wa mtu unaonyeswa
na uwezo wa kujitolea na kutumikia bila kufanya ubaguzi wa watu. Mtu anayependa
kweli anataka tu manufaa ya mtu anayempendwa. Ndio kwa upendo huu ambao Yesu
anatualika siku ya leo nao ndio upendo huu unaotufanya kuwa wenye uhuru na watu
wa kweli.
Kumpenda Yesu kama anataka ni zawadi ambayo
tunapewa kupitia kulisikiliza Neno kwa uaminifu na kwa uvumilivu. Kupitia Neno
na tendo la Roho, Mungu Baba anafanya ndani yetu moyo wa Mwanawe ili tupende
kama Yeye. Huu sio upendo ambao unaniongoza kufanya lile ambalo linanipendeza
tu bali unaniwezesha kujisalimisha kwa ajili ya wengine. Ndio upendo ambao
unatufanya kuacha ubinafsi wetu na kuenda kukutana na wengine katika mahitaji
yao. Huu ni upendo ambao unafanya kazi yetu iwe ufanisi daima naye Roho
Mtakatifu peke yake anayeweza kuuimarisha upendo huu mioyoni mwetu. Kwa hivyo, tuombe
kwa amini, uje Roho Mtakatifu na kutufundisha kumpenda Yesu kama inavyopaswa!
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário