Dunia yetu inakabiliana na mgogoro mkubwa wa
thamani. Hizi (thamani) zimeshindwa kupata nafasi zao za kweli, yaani sisi
hatuwezi tena kufahamu tofauti kati ya kile kilicho muhimu sana na kilicho
muhimu kidogo tu. Kila mtu anahitaji mzani wa thamani ambao ni wa msingi ambao
kupitia juhudi za mtu unaweza kutoa mwelekeo kamili kwa maisha yake mwenyewe.
Wengi wetu hatujui thamani za msingi za maisha yetu wenyewe kwa sababu
tunaathiriwa kwa urahisi na mazingira ambayo tunaishi: familia, shule,
marafiki, jamii, nk. Bila shaka haya ni msaada wa kwanza ambao kila mmoja wetu
anahitaji. Lakini ni lazima tujiulize: ni thamani gani zinazoyahusu maisha
yangu sasa? Ni nini muhimu sana? Kwa njia hii, tunaanza kupanga mzani wetu wa thamani.
Kuwa na mzani wa thamani ni muhimu sana hata
tunaweza kumwambia mtu, “nionyeshe mzani wako wa thamani nami nitamwambia wewe
ni nani!” Kwa maana hii, “mzani wa Thamani ungepaswa kuwa kwa sikuzote za
maisha nao hauwezi kusukumwa na ulimwengu, lakini uwe matokeo ya utafutaji
makini, kwa sababu ubora wa maisha yetu na chaguo tunazochukua zinautegemea
mzani wa thamani wetu. Wale wanaoishi imani ya Kikristo anakiri kwamba ndiye
Kristo ambaye anaonyesha mzani wa kweli wa thamani. Mambo aliyotenda na
kuyafundisha, yaani thamani za injili, kinakuwa kipimo kwa ajili ya uzoefu wa
mtu yeyote duniani, hata kwa wasioamini.
Ninapodhani kuhusu Mtakatifu Yohane Calabria,
kwa mfano, ninamwona yeye kama mtu wa imani kuu, ambaye aliupanga mzani wake wa
thamani kutoka mpango fulani, yaani: “Utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki
yake, na hayo yote mtazidishiwa.” Hii ni usemi mmoja wa injili wa Mathayo (Mt
6:33). Mambo yote Mtakatifu huyo aliyodhani kwa ajili ya maisha yake na ya
Shirika lake linaloitwa Familia ya Kikalabria (Poor Servants of Divine
Providence) hupata msingi na uthabiti yake katika mpango huu. Kutokana na
mpango huu tuko na thamani kama ubaba wa Mungu, utunzaji, uaminifu, imani,
ujasiri, utambuzi, uamuzi, nk.
Tunapofikiri kuhusu thamani ya mtu mwenyewe,
hatuwezi kutumia kipimo cha kijamii, vinginevyo tutashawishiwa kumfikiria
kutoka uwezo wake wa kujitokeza, kuwa bora kuliko wengine, kushindana. Katika
injili, mashindano kwa ajili ya nafasi ya kwanza, kwa upendeleo na kwa umaarufu,
yalimfanyisha Yesu kusema, "kati yenu isitukie hivyo.” Kutoka kwake Yesu Tunaelewa
njia kamili ya uhusiano kati ya watu mambo muhimu ya kutafuta ili kutoa maana
ya kweli kwa maisha yenyewe. Mawazo ya Yesu ni mawazo tofauti na mawazo ya
kitupu ya binadamu, yaani kuwa wa mwisho ili kuwa wa kwanza; kuwa mtumwa wa
wote ili kuwa wakuu; kupoteza maisha ili kuyapokea tena; kufa ili kuishi. Mambo
yote yazitegemea chaguzi zetu.
Mwandishi fulani asema kwamba “njia ya furaha
na kutimiza kwa kibinafsi lazima inazihusu chaguzi tunazochukua.” Hatutaki
kuishi kwa kulalamika milele kwa sababu ya kile hatunacho, bali tuweze kutambua
vizuri kabla ya kuuchukua uamuzi wowote kwa sababu kila uamuzi huleta hasara na
faida. Heri aliyejifunza kulima maishani mwake thamani za kweli; hatavunjika
moyo katika wakati wa msingi wa kuwepo kwake. Nataka kumalizia kwa kuonyesha
kwako, msomaji, thamani zingine ambazo Maandiko Matakatifu hutupatia na ambazo zinaweza
kutusaidia sana katika mpango wa mzani wa thamani wetu ambao utatia msukumo kwa
maisha yetu, kwa mfano:
- AMINI: Mithali 3.5: "Mtumaini Bwana kwa
moyo wako wote.” Kuamini ni kuwa na hakika kwamba Mungu anatulinda na kwamba
Yeye huyaongoza maisha yetu.
- UKARIMU: Methali ya 11.17: “Wale ambao ni wakarimu
hupata faida daima.”
- UWAZI: Mithali 11, 20: “Bwana hapendi wale
ambao mioyo yao si ya haki, lakini anafurahia wale ambao njia zao ni halali.”
Mungu hapendi uwongo, anataka tuwe waaminifu, wa hiari, na wa kweli.
- UKWELI: Mathayo 7:12: “Yoyote myatakayo
mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo.”
- IMANI: Mathayo 9:29: "kisha Aliyagusa
macho yake na kusema, ' kwa kadiri ya imani yenu mpate!”
- UPATIKANAJI: Luka 1:38: “Mimi ndiye mtumishi
wa Bwana, na iwe kwangu kama ulivyosema.”
- UNYENYEKEVU: Matendo 2:46: “Wao walimega
mkate nyumba kwa nyumba na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa unyenyekevu
wa moyo."
- MSHIKAMANO: Matendo 4.32: “Walioamini
walikuwa na moyo mmoja na roho moja; walikuwa na vitu vyote shirika.”
- UPENDO: Matendo 9.36: “Yeye alikuwa amejaa
matendo mema na sadaka alizozitoa.”
- KUHUDUMIANA: 1Petro 4.10: “kila mmoja wenu kwa
kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana.”
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário