Matendo 2, 14a.36-41;
1Pt 2,20b-25; Yoh 10,1-10
Tunaadhimisha Jumapili ya Mchungaji
mwema na Jumapili ya miito. Jumapili hii inatualika kumshukuru Mungu kwa zawadi
kuu ya wito na kumwomba aendelee kulibariki Kanisa lake kwa miito mingi.
Pendekezo la Jumapili hili linatoka kwa Baba Mtakatifu Paulo wa VI. Yeye
alilialika Kanisa zima kuchukua ahadi kwa ajili ya wito. Maombi kwa ajili ya miito
ni pia utii kwa mwaliko wa Yesu ili tuombe kwa mwenye mavuno ili atume
wafanyakazi kwa mavuno yake kwa sababu mavuno ni makubwa, lakini wafanyakazi ni
wachache (cf. Mt 10, 37-38). Wito ni zawadi ya Mungu na ubatizo ni chemchemi
yake na familia ni mwanzo. Mungu anayemwalika
kila mtu hutarajia jibu kwa ukarimu kutoka kwa anayealikwa.
Katika somo la kwanza mitume wanatangaza
kwa shauku fumbo la pasaka ya Kristo kwa nguvu wa Mungu, kama mwaliko wa
mabadiliko ya maisha. Nguvu ya maneno yao yalitoka kwa Roho Mtakatifu akitenda
maishani mwao na kusababisha kutubu. Kwao kila kipindi kilikuwa nafasi mpya ya
kushuhudia maisha mapya aliyotoa Yesu kwa wote hata “kwa ajili ya wanaokaa
mbali na kwa ajili ya kila mtu ambaye Bwana Mungu wetu atamwita kwake”. Hakuna
hata mmoja anayekaa nje ya pendekezo hilo la uokovu.
Kulingana na Mtakatifu Petro, Mungu
hapendezwi na mateso ya watu bali anapendezwa na tabia ya uvumilivu ya mtu
mbele ya mateso. Ndiye Kristo ukamilifu wa ahadi za Mungu na kupitia yeye watu
wana uhakika wa kupata wokovu. Yeye ametufanya kuwa watoto wa Mungu naye kututunza
sisi kama anavyofanya mchungaji na kondoo wake. Tukiufuata mfano tufanye vivyo
hivyo kwa ajili ya wengine.
Katika injili, Yesu anajifunua kama
Mchungaji na mlango wa kondoo. Yeye anavitumia vitenzi kama kujua, kuita,
kusikiliza, kufuata, kuongoza na kutoa kwa ajili ya kuongelea tofauti kati yake
na wale waliokuja kabla yake. Yesu ndiye Mchungaji Mwema kwa sababu anawapenda wana
kondoo wake. Utayari wake wa kufa kwa ajili yao ni maonyesho ya upendo huu. Anawajua
wana kondoo wake na kuwaalika kuisikiliza sauti yake ambayo yanawaongoza kupata
ukamilifu wa maisha yao.
Akitumia mfano huu Yesu anataka
kuongelea uhusiano kati yake na wanafunzi wake. Msingi wa uhusiano huu ni amini,
upendo, upole nao unasababisha maisha kamili kwa wafuasi wake. Kama yeye
anawajua wana kondoo wake, anatarajia kwamba wako tayari kumjua na kuyafuata
mafundisho yake. Kosa la kujua njia na sauti ya mchungaji ni hatari kwa sababu
linaweza kusababisha mgawanyiko wa kundi na hasara ya utambulisho wa mfuasi.
Njia ya Yesu ya kuongoza na kutunza ni kipimo cha walio na jukumu la kuwaongoza
watu.
Yesu ni mlango wa uhusiano mwema kati
ya watu na Mungu. Mlango huu unamaanisha vipengele vitatu. Cha kwanza, Yesu
ndiye njia inayotuongoza kwa Baba; nafsi
yake inatuhakikishia mkutano na Mungu. Cha pili, Yesu ndiye ukweli wa Mungu kwa binadamu na ukweli
wote wa binadamu kwa Mungu; “kila mtu wa ukweli humsikiliza” (Yoh 18,37) na
kuruhusu kuongozwa naye kwa ajili ya kupata ukweli kamili. Yesu ndiye uhai unaotolewa kwa hiari na kwa wingi
kwa wote.
Katika Yesu aliye Mchungaji Mwema,
Mungu anaonyesha ulinzi na utunzaji wake kwa ajili ya watu wake. Upinzani dhidi
ya sauti ya Yesu ni upinzani wa kuyafanya mapenzi ya Mungu na kuishi uhusiano
wa upendo naye. Jibu yeye analotarajia kwa mwaliko wake siku hizi ndio
uangalifu kwa msukumo wake ili tuweze kutenda kwa hekima katika maamuzi yote tunayopaswa
kuchukua.
Yesu ni mchungaji mwema na ahadi yetu
kama kondoo wake ni kusikiliza sauti yake, yaani kuyafuata mafundisho yake.
Wito wetu unapata mafanikio yake wakati tunaweza kuitambua sauti ya Bwana kati
ya sauti nyingi zinazojaribu kutuongoza. Kupitia neno lake, sakramenti na
mafundisho ya wachungaji wetu Mchungaji Mwema Yesu anaendelea kuwaongoza na
kuimarisha kundi lake. Tunaalikwa kuruhusu kuongozwa kwa roho ya upole na
ushirika. Hata sisi pia kupitia ubatizo tuko na jukumu la kuwaongoza wengine
kwa kuwasaidia wachungaji wetu wafanye kazi yao vizuri. Tunaalikwa kutenda kama
wanafunzi wa kwanza, ambao waliuchukua wito kwa furaha na kwa hamu kwa manufaa
ya Watu wa Mungu na kundi la Yesu.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário